Maboresho kwenye kuchangia M4C kwa njia ya M-Pesa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maboresho kwenye kuchangia M4C kwa njia ya M-Pesa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tuko, Jul 24, 2012.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Jul 24, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Nimekuwa mchangiaji wa mara kwa mara kwenye M4C kwa njia ya m-pesa. Hata hivyo siku za karibuni nimejikuta naacha taratibu kutokana na kujiuliza bila majibu maswali yafuatayo;
  - Hivi bado tunahitajika kuchangia?
  - Ela zimetosha?
  - Tumeshachangia sh ngapi?
  - M4C kwa sasa inahitaji sh ngapi, na ngapi wanazo?

  Naomba viongozi wa CDM, kama wanahitaji michango kutoka kwetu wanachama, watujibu maswali hayo hapo juu
  Naomba niwape ushauri ufuatao, namna ya kujibu maswali hayo...

  1. Waweke matangazo ya kuhamasisha uchangiaji, na kukumbusha namna ya kuchangia kwenye vyombo vya habari kama TV, redio na magazeti
  2. Waombe nafasi JF, kuwe na sticky thread inayokuwa updated mara kwa mara juu ya hali ya uchangiaji, nini kimechangiwa, kimechangiwa na watu wangapi, nini kinahitajika, na kuhamasisha watu wachangie
  3. Mtu akichangia kwa m-pesa, ajibiwe kwa msg, ikionyesha hadi wakati huo ameshachangia kiasi gani (hiyo namba yake), akaunti ina kiasi gani, kimechangiwa na watu wangapi, na akaribishwe na kuombwa kuendelea kuchangia
  4. Afisa habari, ama ikiwezekana katibu mkuu awe anaongea na waandishi wa habari, angalau mara moja kwa mwezi, akitoa taarifa, pamoja na mambo mengine, progress ya M4C (wamefanya mikutano mingapi, wanachama wangapi wapya wamejiunga, nini malengo ya sasa na ya baadae juu ya M4C, atoe almanac ya mikutano kwa kipindi cha mwezi mmoja unafuata), lakini pia atumie wasaa huo kuhamasisha wananchi wachangie M4C.

  Nimetoa ushauri wangu tu kama mtaalamu wa mambo ya harambee, nikijua kuwa moja wapo ya namna ya kumhamasisha mtu achangie, ni kwa kuonyesha kutambua na kutahmini mchango wake, kuonyesha mchango wake ni sehemu gani ya kilichochangwa/kunachohitajika, kuonyesha ni watu wangapi wanachangia n.k.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jul 24, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mawazo yako ni ya kimapinduzi na kiwango!
  Unaonyesha wazi nia yako ni kuboresha utaratibu ili uhamasishe watu zaidi!
  Wapo wahusika kibao hapa, lakini nanyaro ni mtu makini, atawapelekea salamu mapema kabisa!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #3
  Jul 25, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ni kweli kabisa mkuu, tunao viongozi wengi wa CDM hapa, naamini watayafanyia kazi..
   
 4. R

  Ramos JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2012
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Shukrani sana ndugu yangu kwa kuikumbushia hii issue maana tulichangia kwa mda, but hatukupata feedback. Hata ivo ni vizuri ukawa unaisema ndani ya vikao kama wewe ni mwanachama...
   
 5. H

  Hiraay Member

  #5
  Jul 25, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sikuwa na habari kuwa naweza kuchangia M4C kwa njia ya M-Pesa. Nataka nitoe mchango wangu sasa hivi, nipeni hiyo namba ya kutuma au utaratibu wenyewe.
   
 6. R

  Ramos JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2012
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hilo ndilo tunalowaomba CDM wafanye. Maana mkuu hata nikikuelekeza hapa, ni watanzania wangapi wasiosoma huu uzi wanataka hiyo elimu?
   
 7. O

  OPTIMUS TZ JF-Expert Member

  #7
  Jul 25, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 391
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  vifaa vya M4C kama kofia ,skafu,gwanda na bendera kubwa na ndogo hatuvioni mtaani tununue visambazeni kwa wingi wakuu vinaweza kusaidia mfuko na hiyo number ya mpesa itangazeni vituo vya reido na Tv hatuiju wadau kutoa chochote kil siku hat Ths 100 iwe ndo slogan haba na haba ........................gamba tutalingoa
   
 8. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Hongera mwanzisha mada.
  Hii ni changamoto kwa viongozi na wale wanaohusika kuweka mambo wazi ili kuleta hamasa na uwajibikaji.
  Viongozi au wahusika kushindwa kufanya hivyo inadhihirisha ni namna gani hawathamini wanachama wao na mchango wanayoomba. Pia anaonesha kukosa uwajibikaji kwa wanachama na wananchi kwa jumla.
   
 9. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Makene na Makamanda wengine mupo?Tuko ana hoja ya msingi.....tiririkeni
   
 10. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #10
  Jul 25, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Mimi toka nimesikia kuna mtando wa wa kuingialia mawasiliano, SPOOFING SMS NIMESTOP MĄNA INAWEZEKANA TUMESHALIZWA CHADEMA WATUPE FEEDBACK YA TULICHOCHANGIA KWANZA.
   
 11. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #11
  Jul 25, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Ni vema kwa chama cha CDM kufuatilia hili ilikujua kama michango tunayoichangia inafika salama au tayari mfumo umeshaingilia na sms spoofing.

  Ni vema chadema waka wakalifuatlia kwa undani.

  Wanakilisha.
   
 12. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #12
  Jul 26, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Mi naamini viongozi wa CDM ni wasikivu, na tukiendelea kulisisitiza hili watatujibu. Ukombozi wa hii nchi ni jukumu letu Watanzania, na CDM wamebeba tu dhamana ya kutuongoza. Wawe makini
   
 13. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #13
  Jul 26, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  By the way..., Tuliahidiwa na viongozi baada ya ile harambee ya siku ile kuwa muda sio mrefu tutapewa utaratibu wa kuchangia kwa tigo pesa na airtel money. Mbona kimya?
   
 14. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #14
  Aug 10, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Kamanda Mbowe, leo unapoelekea Serena kufanya hii kazi, naomba uzingatie huu ushauri
   
 15. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #15
  Aug 11, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Takwimu za makusanyo ya jana pale serena pia zisisahaulike
   
Loading...