Maboresho kutoka Wizara ya Afya juu ya kujikinga na COVID-19

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,637
2,000
Tanzania imeboresha hatua za kuchukuliwa ili kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya #CoronaVirus kwa Wasafiri na kujuisha hatua za usafirishaji wa bidhaa na huduma

Watanzania na wageni wanaoishi nchini wametakiwa kutosafiri kwenda nchi zilizoathiriwa kama hakuna ulazima. Wasafiri wote watakaoingia nchini watawekwa karantini kwa gharama zao

Baada ya siku 14 muhusika aliyewekwa Karantini ataruhusiwa kutoka na atatakiwa kuacha taarifa binafsi zitakazosaidia katika ufuatiliaji

Wasafiri wote watakaoingia nchini watafanyiwa ukaguzi wa kina pamoja na kuchukuliwa vipimo vya #Covid19 pale itakapotakiwa kufanywa hivyo

Mashirika ya ndege yanashauriwa kuwa na seti mbili za Wahudumu (crew) ili wabadilishwane watakapofika nchini na kuondoa ulazima wa kukaa Katantini

Endapo msafiri atapata dharura yoyote ya afya atatakiwa kupiga simu ya bure ya afya 199. Ushauri huu unaweza kuendelea kuboreshwa kulingana na mabadiliko na hali ya #CoronaVirus nchini

#JFCOVID19_Updates

1586003048369.png

1586003110741.png
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom