Maboresho katika elimu yatakayomsaida mwanafunzi kujiendeleza kimaisha pindi amalizapo elimu au akwamapo njiani kabla ya kumaliza

humphreykweka

New Member
Jan 11, 2018
1
0
Ni wazi kwamba mifumo wa elimu yetu hapa nchini Tanzania haijaweza msaidia mwanafunzi kujisimamia na kuendesha maisha yake bila utegemezi wa wazazi/walezi au kuajiriwa.Kwa kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira kwa vijana na kutokuwa na thamani ya elimu yetu ya msingi na sekondari katika ajira zinazotangazwa sehemu tofauti katika taifa letu,inanipa nafasi ya kushauri na kutoa mawazo yangu katika mfumo wa elimu hapa nchini Tanzania.

Tukianza na elimu ya msingi inayomchukua mwanafunzi miaka 7 shuleni,ilipaswa ithaminiwe na kuchukuliwa uzitomkubwa sana kwa mwanafunzi maana ni miaka mingi katika ukuaji wa mtoto na kujitambua yeye ni nani na anataka kuwanani katika maisha yake, na sio kupuuzia na kuchukulia kama ni elimu ya ukuaji mtoto.

Ni wazi elimu hii ya msingi haimpi mwanafunzi nafasi ya kuweza kujiajiri au kupata ajira mahali popote katika nchi yetu japo ni elimu inayochukuwa miaka mingi kwa mwanafunzi awapo shuleni kuliko elimu nyingine zinazotolewa hapa nchini.

Yapo mambo mengi sana yanayosababisha wanafunzi wengi kuishia katika daraja hili la elimu ya msingi hapa nchini na kusababisha kuwapo na kiwango kikubwa cha vijana wasiweza kujiajiri au kuajiriwa mahali popote pale na kwanafisi yoyote ile ya ajira.

Wapo walikosa watu wa kuwaendeleza kutokana na wazazi/walezi kutokuwa na uwezo,wapo walioopoteza wazazi/walezi na kupoteza pia sifa za kuendelezwa,wapo waliorubuniwa na kupewa ujauzito na kuishia katika daraja hilo na wapo ambao hawakuweza kuchakuliwa katika kiwango ambacho serikali imekiweka kwa ufaulu na kuendelea na masomo katika shule za sekondari za Serikali na mbio zao kuishia hapo.Hili ni kundi kubwa sana la vijana ukiangalia ni vijana wangapi wanahitimu elimu hii ya msingi na wangapi wanauwezo wa kuendelea na elimu ya sekondari.

Ningeiomba serikali itazame upya mfumo huu wa elimu ya msingi kutoka kwenye elimu ya kusoma na kuandika tuu kwa miaka 7 na kufundisha vijana hawa namna ya kuweza kuendesha maisha yao pindi wamalizapo elimu hii ya miaka 7 kwa vitendo.

Ushauri wangu naomba ujikite katika mambo yafuatayo,kuwepo na elimu ya computer katika elimu ya msingi itakayo mwezesha kijana kujifunza technology mpya inayoenda kasi duniani na kuweza kujiajiri au kuajiriwa baada ya kumaliza masomo na kushindwa kuendelea na elimu ya sekondari.

Mfano wa ajira ni secretarial office ambazo huchapisha nakala,kutengeneza matangazo kwa uchapishaji, na mengine mengi yanayofanywa katika ofisi hizo.Utekelezaji huu uendane na sera ya serekari ya kusambaza umeme nchi nzima haswa kwa kipindi hiki wanapomalizia kusambaza umeme katika vijiji vyote vya Tanzania.

Elimu ya vifaa vya elecronics,hii ni elimu iliyoinua nchi nyingi duniani kwa vijana kutosubiri kuajiriwa na kuweza kujiajiri kwa kurepear au kuunda vitu vyao wenyewe na kuongeza ushindani wa kibiashara na nchi nyingine duniani.

Kilimo kisiishie katika mbogamboga bali waalimu waende mbali kwa kuwafundisha vijana umuhimu wa kilimo na kuwaonyesha jinsi kilimo kinaweza inua maisha yao kwa mazao ya chakula na biashara na kuwapa mifano hai ikiwemo kutambua aina za udongo,mbolea na mazao husika.

Michezo isiwe kipindi cha dakika 45 tuu kwa week ambapo hudumaza vipaji vya watoto na kushindwa kuendelea mbele maana hawana muda tena wa kutekeleza hilo,nikiwa na maana mtoto anaingia shule asubuhi na kutoka jioni na akitoka ana kazi za nyumbani na za shule kama home work na kukosa muda wa kutunza kipaji chake mpaka ifikapo siku1 ya week yenye dakaka 45 tuu.Kambi za michezo kwa watoto zifufuliwe na kwa malengo na uangalifu mkubwa ili kukidhi haja za kumjenga mtoto katika kuweza kujiajiri mapema na kutambua kipaji chake,hapa nalenga kambi za umitashunta na umisenta.

Kwa elimu ya sekondari bado kuna wimbi kubwa la vijana wasio na ajira na wasiona uwezo wa kuajiriwa shemu yoyote na hii ni kutokana na elimu yao pia kutothaminika kwa maana ya utendaji na utekelezaji wa jambo.Hii ni wazi pia mtaala unatumika haukidhi mahitaji ya kijana kuweza kujisimamia na kufanya kitu bila ya kusimamiwa kwa mahitaji yao binafsi yaani kujiajiri. Vijana wengi wamekuwa wakifundishwa tuu kufaulu na wanakuwa na material kichwani ya kufaulu na sio kuweza kutekeleza jambo kwa ukamilifu japo wamekaa shuleni kwa muda mrefu toka elimu ya msingi hadi sekondari.

Naishauri serikali kuangalia mitaala hii kwa haraka mno maana vijana wasio na ajira na waliomaliza elimu ya sekondari ni wengi mno na hawana sifa ya kujiunga na vyuo vikuu,hawawezi kujiajiri wala hawana sifa ya kuajiriwa kutokana na uwezo wao wakutambua mambo na kuyatekeleza kwa vitendo.

Ushauri wangu kwa wizara husika ya elimu na serikali kwa ujumla,kuangalia fani zote zinazomwezesha kijana wa sekondari aweze kujiajiri au aweze kujitambua na kuweza kutekeleza jambo kikamilifu na kuwa na uwezo wa kuajiriwa,ziingizwe katika mitaala ya elimu yao ili kupunguza hili wimbi la vijana wasio na ajira mitaani.

Hapa nazungumzia masomo ya Computer,Electonics,Languages(Hapa isibaki kuwa English na Kiswahili tu).Na ziada kama sio la msingi ni zaidi ya kuwa na maabara tuu katika shule zetu za sekondari twende mbele zaidi na tuwe na workshop ili vijana wajifunze ufundi tofauti ili hali wakimaliza na wakashindwa kuendelea na vyuo vikuu basi watajiajiri au kuendelea na vyuo vya ufundi maana watakuwa na ideas kwa kile walijifunza sekondari.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom