Mtaalam
JF-Expert Member
- Oct 1, 2007
- 1,371
- 250
TIMU ya ngumi ya Tanzania iliyokwenda kushiriki michuano ya ngumi ya Ubingwa wa Afrika, wamekamatwa na dawa za kulevya aina ya heroin.
Waliokamatwa ni kocha wa timu ya taifa, Nassor Michael, bondia wa uzito wa feather Petro Mtagwa na bondia pekee aliyefuzu kucheza michezo ya Olimpiki, Emilian Patrick.
Hata hivyo, katika watu hao ambao picha zao zimewekwa kwenye mtandao huo, hawajaweza kutambulika majina yao.
Emilian Patrick ambaye anapigana kwenye uzito wa bantam (kilo 54) alipata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania kwenye michezo ya Olimpiki baada ya kupata medali ya fedha kwenye michezo ya kuzufu iliyofanyika mapema mwaka huu, Namibia.
Timu hiyo iliondoka Jumatano kwenda kushiriki michezo ya Ubingwa wa Afrika na walikabidhiwa bendera ya taifa Jumatatu iliyopita kwenye uwanja Uwanja wa Ndani wa Taifa.
Taarifa iliyotolewa na mtandao wa Le Défi Media Group wa Mauritius unaoandikwa kwa Kifaransa, umeripoti kuwa msafara huo ulikuwa na Watanzania sita wakiwamo mabondia wanne.
Mabondia hao walikamatwa na kikosi cha kupambana na dawa za kulevya cha nchini humo kwenye hoteli yao juzi usiku na dawa hizo zina thamani ya randi milioni 40 (sawa na takribani Sh milioni 600).
Taarifa hizo zinasema jana mchana wachezaji hao walitarajiwa kupandishwa kizimbani katika mahakama ya Mahébourg kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya.
Maofisa wa Shirikisho la Ngumi la Mauritius walikiri kukamatwa kwa mabondia hao na kuwa Tanzania imeondolewa kwenye michuano hiyo inayotarajia kuanza leo na kufikia kilele chake Juni 25.
Alipoulizwa Rais wa Shirikisho la Ngumi Tanzania, Shaaban Mintanga, alisema hana taarifa za kukamatwa kwa watu hao na kuwa alipowasiliana nao walimwambia kuwa wamefika salama. Alisema timu yake iliondoka Jumanne ikiwa na wachezaji wawili na kocha, wakati awali ulikuwa uondoke msafara wa watu watano na kuwa yeye na bondia Ali Kimwaga walishindwa kusafiri kutokana na uhaba wa fedha.
" Timu imeondoka na watu watatu; kocha Nassoro(Michael), Emilian(Patrick) na Petro(Mtagwa) na nimewasiliana nao juzi (Jumatano) na waliniambia wamefika salama.
"Sijui kama hayo unayoyasema ni kweli kwani nilipozungumza naye alisema hakukuwa na tatizo lolote zaidi ya kunieleza kuwa wameongeza gharama za malazi kutoka dola 40 mpaka 70.
Lakini mimi niliwaambia kuwa nitazungumza na Rais wa Shirikisho la Ngumi la Mauritius, lakini mawasiliano hayakuwa mazuri," alisema Mintanga na kutoa namba + 230 9129197 ambayo hata hivyo gazeti hili lilishindwa kupata mawasiliano.
Alipoulizwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Patrick Mombo alisema hana taarifa zozote za kukamatwa mabondia hao.
na Anastazia Anyimike
wa Daily News