Mabondia wa tanzania waukana uraia

MABONDIA wawili Karim Matumla na Omari Kimweri waliotoroka mwaka 2006 baada ya michuano ya Jumuiya ya Madola wameukana Utanzania kwa kukubali kuchukuwa uraia wa Australia.

Sheria za Tanzania haziruhusu mtu yoyote kuchukua uraia wa nchi nyingine kabla ya kuukana Utanzania wako.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari, mabondia hao kwa sasa wana uraia wa Australia ambao waliupata mara baada ya kuachiwa huru baada ya kukamatwa.

Karim Matumla ambaye alikuwa nahodha wa timu ya Taifa ya ngumi za ridhaa, aliingia mitini mjini Melbourne, akiwa bondia wa pili kufanya hivyo baada ya Kimweri.

Matumla kwa sasa amepewa namba 418456 ambayo inatambuliwa katika mchezo wa ngumi za kulipwa kama Global ID.

Katika wasifu wa bondia huyo kupitia njia ya mtandao, Matumla ametajwa kuwa bondia wa Australia mwenye asili ya Tanzania aliyezaliwa Desemba 9, 1978 na kwa sasa anajulikana kwa jina la utani kama Karim Maboota.

Bondia huyo ni wa 805 kati ya mabondia 1426 huku makazi yake ni Belbourne, Victoria.

Wasifu huo umeonyesha kuwa bondia huyo ni mzaliwa wa Dar es Salaam, Tanzania ambapo wakati wa kuzaliwa alipewa jina la Karimu Nyamwela Matumla.

Mbali ya hayo, wasifu huo umeonyesha rekodi yake ambapo kwa sasa amepigana mapambano mawili na kushinda yote ikiwa kwa pointi.

Pambano lake la mwisho lilikuwa dhidi ya bondia Manu Emerly ambaye alizichapa naye Mei 22 mwaka jana na kushinda kwa pointi 40-35, 39-37 na 40-35.

Mwaka 2007, bondia huyo alishinda pambano dhidi ya Arnel Balicuatro kwa kujikusanyia pointi 40-35, 40-36 na 40-35.

Kwa upande wa Kimweri yeye amepewa namba ya utambulisho 395556 na amezaliwa Septemba 22, 1982 na kwa sasa anapigania uzito wa bantam.

Bondia huyo ni wa 147 kati ya mabondia 861 wa uzito wake na makazi yake ni Blackburn, Victoria, Australia.

Mbali ya kutajwa amezaliwa Dar-Es-Salaam, kwa upande wa uraia ametajwa kama bondia wa Australia.

Rekodi yake ni mapambano saba, ameshinda matano na kupoteza mawili.

Mmoja wa wana familia ya Karim, bondia maarufu, Rashid Matumla amesema kuwa hawana taarifa ya ndugu yao kubadili uraia.

"Katika familia yetu hakuna taarifa hiyo, lakini ndugu yetu amekuwa ana maamuzi yake, na hakuna mtu anayeweza kumzuia," alisema Matumla.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Joel Bendera alisema kuwa hawana taarifa hiyo zaidi ya ile ya kukamatwa kwao baada ya kuzamia wakati wa michezo ya Jumuiya ya Madola.

"Tulipata taarifa hiyo tu, hatujui kama wamebadili uraia kwani walileta aibu kubwa sana baada ya kukimbia, hatujafuatilia tena baada ya kukamatwa kwao,"alisema Bendera.

Ni haramu kumsingizia mtu jambo ambalo hajalifanya. "Kukana" ni kitendo "verb/action" ambayo hutekelezwa kwa aidha maneno, maandishi(na signature) au vitendo kuashiria yaliyomo ndani ya moyo na akili (conscience) ya mhusika. Nani ana ushahidi wa kwamba vijana hawa wamefanya moja kati ya hayo kuhusiana na utanzania???? Nia zao je, nani amezi-scan???

MAFISADI wanaukana uTanzania. Yes, !!! Vitendo vyao, maneno yao, maandishi yao (na sahihi zao) na kwakuwa huyafanya hayo chini ya kiapo cha kutoyafanya, basi hiyo inasema kwa mapana na marefu yaliyo moyoni na akilini mwao. Najisi, uvundo na haramu kwa Tanzania.

Nani miongoni mwetu humu ambae badala ya kuwa amechagua tu Mwenyezi Mungu azaliwe katika nchi, wazazi na wakati wa alipozaliwa (Tanzania) yeye ameapishwa wakati wowote ule wa maisha yake na kukabidhiwa uTanzania??? Mimi siajawahi hata siku moja, na mapenzi, huruma na uzalendo nilionao juu ya Tanzania hauna kipimo(measurement) kwa maana hauna limit wala dimension, labda tu kama lile tukio la mimi kuzaliwa katika nchi ile, na wazazi wangu, miongoni mwa familia yangu, ndugu na jamaa hata majirani zangu, na miongoni mwa jamii na watu wangu na katika ardhi (nchi) yangu, lifutike. Kitu ambacho WANASIASA (MAFISADI na WASIO MAFISADI), mmoja mmoja au hata kwa pamoja na mavi yao wanayokunya kila siku hawataweza kamwe.

Na kama kupewa kadi ya uraia ambayo sijawahi kuiona na ambayo kusema kweli haimaanishi lolote kuhusiana na uzalendo, mapenzi na huruma tulizonazo juu ya nchi yetu, basi hawakuja kunichukuwa kutoka kwengine(nchi nyengine) na kunipa kadi, la hasha !!! walinikuta Tanzania, na ni kutokana tu na taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa matakwa na maamuzi ya nchi yetu, walibidi wanipe, watake, wasitake, niwe nakubaliana nao wanipe, niwe napingana nao wanipe. Haki yangu, sio yao. Na sijawahipo kuomba au kupewa kadi.

Mnafiki gani aliyekuwepo wakati hawa vijana 1) Wanakabidhiwa kadi za uraia wa Australia. 2) Wakati wa mauziano, yaani kujaza fomu za maombi, kulipia manunuzi ya bidhaa hiyo (uraia wa nchi nyengine, iwe Australia, Marekani, Ugiriki,nk, nk) na kuona kama sharti moja au zaidi la manunuzi hayo ni "kuukana" uTanzania??? au kuwaona wanajaza au kuandika wasia au wametamka kwamba wameukana uTanzania???. Wapumbavu Wanasiaisa Mafisadi wanaofikiri mtu kuukana utaifa wake ni jambo la kirahisirahisi kama wao wanavofanya. Ndio wao wanaofanya watu wawe na "ill feelings, grudge na resentment" na nchi yetu.

Kutoruhusu ni maana ya "kuzuai". Je ni wapi sheria za Tanzania zikawe na haki ya kutomruhusu/kumzuai mtu kufanya jambo lenye faida na maisha yake, familia yake, ndugu na jamaa zake na kama sio MAFISADI na UFISADI wao, basi kwa nchi yake Tanzania???

Kwa kifupi, Kimweri na Matumla HAWAJAUKANA uTanzania, walilolifanya ni kununua tu uraia wa Australia kutokana na kutaka kuboresha maisha yao. Sio kisiasa, sio kidini, na anaenadi kwamba eti hii ni kwa kutoipenda Tanzania, yaani kutokuwa na uzalendo, basi ni mhalifu, fisadi aliye wazi, unless kama wahusika wenyewe wameashiria hivyo. Na kwa Taarifa yenu, wanapopigana ulingoni huwaaomba waTanzania wenzao kuhudhuria kwa wingi wakiwa na bendera za Tanzania sio za Australia. Na InshaAllah Mwenyezi Mungu awape ushujaa ku-defy the odds kwa kuipeperusha bendera yetu sambamba na ya Australia hata wanapoiwakilisha Australia, kitu ambacho kitahitaji moyo mkubwa mbele ya kadamnasi ya waAustralia hasa ukizingatia kwamba kwa bahati mbaya Mafisadi wetu ndio wasemaji wetu, na wao ndio wanawa-let down kwa kuwasingizia kwamba wameukana utanzania.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom