Mabondia wa tanzania waukana uraia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabondia wa tanzania waukana uraia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jan 23, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,169
  Likes Received: 5,594
  Trophy Points: 280
  MABONDIA wawili Karim Matumla na Omari Kimweri waliotoroka mwaka 2006 baada ya michuano ya Jumuiya ya Madola wameukana Utanzania kwa kukubali kuchukuwa uraia wa Australia.

  Sheria za Tanzania haziruhusu mtu yoyote kuchukua uraia wa nchi nyingine kabla ya kuukana Utanzania wako.

  Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari, mabondia hao kwa sasa wana uraia wa Australia ambao waliupata mara baada ya kuachiwa huru baada ya kukamatwa.

  Karim Matumla ambaye alikuwa nahodha wa timu ya Taifa ya ngumi za ridhaa, aliingia mitini mjini Melbourne, akiwa bondia wa pili kufanya hivyo baada ya Kimweri.

  Matumla kwa sasa amepewa namba 418456 ambayo inatambuliwa katika mchezo wa ngumi za kulipwa kama Global ID.

  Katika wasifu wa bondia huyo kupitia njia ya mtandao, Matumla ametajwa kuwa bondia wa Australia mwenye asili ya Tanzania aliyezaliwa Desemba 9, 1978 na kwa sasa anajulikana kwa jina la utani kama Karim Maboota.

  Bondia huyo ni wa 805 kati ya mabondia 1426 huku makazi yake ni Belbourne, Victoria.

  Wasifu huo umeonyesha kuwa bondia huyo ni mzaliwa wa Dar es Salaam, Tanzania ambapo wakati wa kuzaliwa alipewa jina la Karimu Nyamwela Matumla.

  Mbali ya hayo, wasifu huo umeonyesha rekodi yake ambapo kwa sasa amepigana mapambano mawili na kushinda yote ikiwa kwa pointi.

  Pambano lake la mwisho lilikuwa dhidi ya bondia Manu Emerly ambaye alizichapa naye Mei 22 mwaka jana na kushinda kwa pointi 40-35, 39-37 na 40-35.

  Mwaka 2007, bondia huyo alishinda pambano dhidi ya Arnel Balicuatro kwa kujikusanyia pointi 40-35, 40-36 na 40-35.

  Kwa upande wa Kimweri yeye amepewa namba ya utambulisho 395556 na amezaliwa Septemba 22, 1982 na kwa sasa anapigania uzito wa bantam.

  Bondia huyo ni wa 147 kati ya mabondia 861 wa uzito wake na makazi yake ni Blackburn, Victoria, Australia.

  Mbali ya kutajwa amezaliwa Dar-Es-Salaam, kwa upande wa uraia ametajwa kama bondia wa Australia.

  Rekodi yake ni mapambano saba, ameshinda matano na kupoteza mawili.

  Mmoja wa wana familia ya Karim, bondia maarufu, Rashid Matumla amesema kuwa hawana taarifa ya ndugu yao kubadili uraia.

  "Katika familia yetu hakuna taarifa hiyo, lakini ndugu yetu amekuwa ana maamuzi yake, na hakuna mtu anayeweza kumzuia," alisema Matumla.

  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Joel Bendera alisema kuwa hawana taarifa hiyo zaidi ya ile ya kukamatwa kwao baada ya kuzamia wakati wa michezo ya Jumuiya ya Madola.

  "Tulipata taarifa hiyo tu, hatujui kama wamebadili uraia kwani walileta aibu kubwa sana baada ya kukimbia, hatujafuatilia tena baada ya kukamatwa kwao,"alisema Bendera.
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2010
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ......Maslahi zaidi si lingine, tz kungewekwa mazingira mazuri ya vijana kama hao kuprosper, sidhani kama wangefanya maamuzi hayo........!
   
 3. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Yeah, waacheni watafute greener pasture..,nawatakia kila la kheri huko walipo
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Safi sana vijana. Tunawatakia maisha mema na mkumbuke mlikotoka.
   
 5. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hata ningekuwa mimi ningefanya the same.
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Siwalaumu......
   
 7. D

  Darwin JF-Expert Member

  #7
  Jan 23, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Bongo watapata nini pamoja nakuwa watu wanaojituma?

  Saaaafi sana. wakishindana kwenye Olympic nitachukua bendera yangu ya TZ kisirisiri nakusema Go uncles!!!!
   
 8. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #8
  Jan 23, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  mambo ya Milk and Honey!
   
 9. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #9
  Jan 23, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Really? Sheria gani hiyo? Na inasemaje specifically?

  Halafu huu mji wa Belbourne Australia uko wapi?

  Kama mtu hawezi kuupata mji, tena mji mkubwa kama Melbourne ambao huhitaji hata atlas kujua spelling zake tu correctly, unategemea atapata the intricacies za story kama hii?

  Waandishi makajanja hawana credibility.
   
 10. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #10
  Jan 23, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Big up sana vijana bongo mngeozea hapahapa tafuteni maisha
   
 11. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #11
  Jan 23, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  heri kuwa masikini uliye huru ndani ya nyumba na usiyekosana na Mungu.... kuliko kuwa tajiri katika chumba cha mtu harafu hupani na Mungu...hapo siwaungi mkono
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Jan 24, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  riziki popote... tuwatakie maisha mema na mungu awasaidie ili waweze kurudisha nyumbani chochote wanachoweza; maana maisha ya bongo ni magumu sana
   
 13. g

  gudlack Member

  #13
  Jan 24, 2010
  Joined: Oct 11, 2009
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Good na msiangalie nyuma hata kidogo huku hakuna matumaini kabisa, na msishangae mtakapofanikiwa wakajitokeza watu kuanza kujivunia mafanikio yenu ndo nature ya watanzania sikuhizi
  nawatakieni kila la kheri na maisha mema msalimieni Mr Paul
   
 14. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #14
  Jan 24, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,609
  Trophy Points: 280
  Wana haki ya kufanya hivyo hapo kwetu kuna nini zaidi ya kupata sifa huku unakufa njaa,serikali yetu itajuwa sasa Umuhimu wa kuwaruhusu Raia wake kuwa na Uraia wa nchi mbili ni aibu na ni vizuri walivyofanya hapo kwetu hakuna Maendeleo yoyote kazi kubwa ya viongozi wetu ni Ufisadi na kula rushwa tu hata kama ni mimi ningekimbia tu Hongera walivyofanya hao vijana wawili.
   
 15. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #15
  Jan 25, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Ukiwa na mawazo ya chipukizi wa TANU utadanganya wanao bure, heri uwe maskini kwenu utaomba mpaka chupi kwa baba! Ili mtu upate mafanikio unahitaji kuexplore,kutafuta opotyuniti. Ukizoea kunyonya kwa mama mbona utamnyonya mpaka afe, Vijana wanatafuta maisha, kwa kazi yao hapa bongo ni uwongo-kazi hiyo inawalipa huko awalipo, na kuukana uraia wa Tanzania haina maana kuwa hawataruhusiwa tena kuingia nchini. Fanyeni kazi wazee, Msiisikilize Hii Mitanzania Mingine, do it for you and your family, Hawa watu wanaoishikilia bongo kwa mabavu kwa hawana lolote la kujivunia kkutoka kwenu, kama Australia inatahamini mchango wenu kuna haja gani kkuhangaika na nchi hii ya majambazi?
   
 16. Absolute

  Absolute JF-Expert Member

  #16
  Jan 25, 2010
  Joined: Jan 19, 2007
  Messages: 335
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wameonesha njia, wengine wafate mkondo...
   
 17. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #17
  Jan 25, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Mmh
   
 18. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #18
  Jan 25, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...safi sana,

  kama madakitari na wahadhiri wanaingia mitini itakuwa mabondia?...
  shibe kwanza, mengine yatafuatia...

  wakishakuwa maarufu utawasikia hawa wanaowaita 'traitors' ooh, "vijana wetu wale"
   
 19. Mtoto wa Kishua

  Mtoto wa Kishua JF-Expert Member

  #19
  Jan 25, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 818
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Bora, kuliko hapa Bongo wanamichezo na wasanii wanavyo baniwa ... hongera sana , ningefanya the same!
   
 20. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #20
  Jan 26, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  :D:D:D:D:D:D:D

  Safi sana na Mungu awatangulie ninawatakieni kila la kheri!
   
Loading...