Mabomu yarindima Moshi ili kusafisha njia Lowassa apite

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,551
Jumapili tulivu.

Maeneo ya Bomambuzi unaendelea uchaguzi wa diwani ambapo leo jumamosi Mh lowassa ametia timu, watu ni nyomi ya hatari.

Wameanza kufyatua risasi za moto na mabomu ya machozi ili kutawanya umati.

=======

Kwa mujibu wa Mwananchi:

Polisi Mkoa wa Kilimanjaro wamelazimika kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchi kumwezesha mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kupata nafasi ya kupita mjini Moshi.

Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wametumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchi waliokuwa wamefunga barabara.

Takriban mabomu manne ya kutoa machozi yalifyatuliwa saa 10:30 jioni ya leo Jumamosi Novemba 18,2017 katika eneo la Soko la Manyema ambako Lowassa na msafara wake alikuwa apokewe ili kuelekea kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za udiwani eneo la Pasua Relini.

Kabla ya Lowassa kufika, vijana madereva wa bodaboda walipita katika Barabara ya J.K. Nyerere.

Vijana hao walipopita mzunguko wa magari wa Coca Cola saa 10:15 jioni, gari la polisi aina ya Toyota Land Cruicer likiwa na polisi wenye mabomu ya machozi lilionekana likiwafuata.

Haikupita dakika 15, ndipo kulisikika milio ya mabomu katika eneo la Manyema ambalo ni njia panda ya kuelekea eneo la mkutano.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema ambaye yuko katika msafara wa Lowassa, alisema eneo la Manyema lilikuwa halipitiki kutokana umati wa watu.

Lema alisema ni kutokana na hali hiyo, ili kumwezesha Lowassa na msafara wake kupita, FFU walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah alisema mabomu hayo yamepigwa ili kupunguza idadi ya watu waliokuwa wamefurika kwenye eneo hilo na kumuwezesha Lowassa kupita.

“Alikuwa hana njia ya kupita, watu walifurika kiasi kwamba hata Lowassa mwenyewe asingeweza kupita, tulifanya hivyo kuwapunguza na ameshapita ameenda zake kwenye mkutano,” amesema.
 
Lowassa MY PRESIDENT



HII NI ARUMERU
fdc49eb3760a14aedfc95de6766b902a.jpg


10ac8ce6c4d530e6af641467ca2fc866.jpg


NA HII NI LEO BOMAMBUZI MOSHI
45d0a9e9232a5d14b00d9ff5f36c8062.jpg



ALIYEMPA WAZO SIZONJE LA KUZUIA MIKUTANO ALIONA MBALI MAANA KAMA KAZUIA HALI NDIO HII JE ANGERUHUSU SI ANGERUDI BURUNDI
 
Jumapili tulivu.

Maeneo ya Bomambuzi unaendelea uchaguzi wa diwani ambapo leo jumapili Mh lowasa ametia timu.watu ni nyomi ya hatari.

Wameanza kufyatua risasi za moto na mabomu ya machozi ili kutawanya umati.

Makamanda hebu njoeni mumchukue mwenzenu atakuwa kazidiwa na chang’aa.
 
hivi babu Lowasa (mugabe) bado yupo kumbe? mpaka jeshi iingilie kati ndo apumzike siasa!!!!....Chadema kushney.
 
Jumapili tulivu.

Maeneo ya Bomambuzi unaendelea uchaguzi wa diwani ambapo leo jumapili Mh lowasa ametia timu.watu ni nyomi ya hatari.

Wameanza kufyatua risasi za moto na mabomu ya machozi ili kutawanya umati.
aisee kweli hii ni jumapili tulivu ya nov 18 2017
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom