Mabomu yalipukia Nyumbani kwa WAZIRI Mkuu.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabomu yalipukia Nyumbani kwa WAZIRI Mkuu..

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kituku, Feb 20, 2011.

 1. Kituku

  Kituku JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 239
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Makombora yatua nyumbani kwa Pinda Send to a friend Sunday, 20 February 2011 09:00 0diggsdigg

  MWANANCHI LASHUHUDIA, ASKARI WAFUTA PICHA KWENYE KAMAERA
  Ibrahim Bakari na Hussein Issa
  AMA kweli mabomu hayana macho, wala hayaogopi cheo cha mtu. Hilo limedhirika baada ya makombora mawili yaliyoruka hewani naada ya milipuko kutokea katika maghala ya silaha ya kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Gongo la Mboto, jijini Dar es Salaam kutua nyumbani kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, eneo la Pugu.

  Hata hivyo, milipuko hiyo ilipotokea usiku Jumatano iliyopita na kuua watu zaidi ya 40 na kuwacha wengine majeruhi zaidi ya 300, Pinda alikuwa kwenye bungeni mjini Dodoma.

  Siku ya Alhamisi, Mwananchi Jumapili lilishuhudia mabaki ya kombora moja yaliyosababisha kiwewe kwa waliokuwawemo ndani ya nyumba hiyo iliyopo Kimani, Pugu karibu na machimbo ya mchanga lakini waandishi walipoenda juzi walikuta askari wa JWTZ wameyachukua na kuacha alama mahali yalipofiga.

  Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana, Msaidizi wa Shughuli za nyumbani kwa Waziri Mkuu, Pascal Mnally alisema makombora hayo yalitua nyumbani hapo kati ya saa 3:00 usiku na saa 4:00 usiku.

  Mnally alisema baada ya makombora hayo kuangukia hapo yalizua taharuki na kiwewe kwa familia ya Waziri Mkuu huyo.

  "Baada ya kishindo cha mabomu, familia yake ilitoka nje na kuanza kukimbia bila mwelekeo maalumu, lakini yeye alibakia ndani kusubiri kitakachotokea,” alisema Mnally na kusisitiza:

  "Mimi sikukimbia, majira ya usiku nilipigiwa simu na Mzee (Waziri Mkuu) akiniulizia hali yangu na familia yangu, nikamwambia tuko salama, isipokuwa mama (mke wangu) amekimbia na sijui wamekimbilia wapi.

  "Mzee akaniambia, kuwa hatukupaswa kukimbia ovyo na alitutaka tusiondoke kwa sababu tukikimbia ovyo tunaweza kupata madhara makubwa”.

  Akionyesha mahali yaliangukia, Mnally alisema: "Kwa kweli hali ilikuwa inatisha. Kwenye saa 3:00, 4:00 usiku hivi ndipo makombora yakaanguka hapa. Moja lipiga hapa (alionyesha na tawi la mwembe uliokatwa kwa kombora hilo) na lilikuwa kubwa kweli kweli.

  "Lingine lililoangukia hapa (anaonyesha shimo) lakini lilikuwa dogo tofauti na na la pale”.

  Kurudi familia
  Baada ya hapo Mnally alimwonyesha mtoto wake aliyekimbi: "Huyu naye karudi jana asubuhi, alisema walikimbilia Vigama mbele ya Stesheni ya Reli ya Tazara."

  Alifahamisha saa 10:00 alfajiri siku Alhamisi alikuwa peke yake nyumbani bila ya kujua familia yake ilala wapi, lakini baadaye waliokimbia walirudi nyumbani wakiwa salama.

  Alisema askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania walifika nyumbani juzi kuyaondoa makombora hayo, lakini wakawapa tahadhari kuwa wasiende maeneo ya msitu mdogo uliopo jirani na nyumba hiyo ambalo ni eneo la Waziri Mkuu pia kwa sababu ya usalama wao kwa vile kuna uwezekano kukawa na mabomu mengine kuangukia huko.

  Askari wanyang’anya kamera

  Katika hali isiyo ya kawaida, waandishi wa habari wa Mwananchi Jumapili ilifika kupiga picha katika nyumba hiyo, askari waliokuwepo eneo hilo walimnyang'nya kamera mpigapicha na kufuta picha zote zilizopigwa zikiwemo za matukio mengine.

  Askari hao kuwaamru waandhi hao kuondoka mara moja katika eneo hilo kwa kuwa hakuwa na mwaliko wa kuingia katika nyumba hiyo ya Waziri Mkuu.

  Wananchi milimani
  Siku ya tukio wakazi wa maeneo hayo ikiwamo Pugu Kigogo Fresh, Kwa Chanza na Pugu Stesheni ya Tazara walikimbilia milimani ikiwemo katika eneo hilo la Waziri Mkuu huku wengine wakijibanza kwenye mahandaki ya mashimo ya kokoto na mchanga yaliyopo Golani.

  Usiku huo, Mwananchi Jumapili iliyokuwa eneo la tukio, ilishuhudia makombora zaidi ya 20 yakitua kwenye msitu uliopo karibu na nyumbani kwa Pinda.

  Hata hivyo, wakati wananchi wanaanza kurejea nyumbani kwao saa 6:48 usiku siku hiyo, Mwananchi Jumapili iliona gari moja aina ya Toyota Land Cruiser lililokuwa na usajili wa namba za STK likiwa mwendo kasi kuelekea nyumbani kwa Waziri Mkuu likiwa lina watu kadhaa.

  Wakati uharibifu na vifo vikitokea maeneo ya Gongolamboto, kombora moja lilitua nyumbani kwa Athumani Chabwalika maeneo ya Pugu kwa Chanzi na kusababisha nyumba yote kuteketea kwa moto.

  Makombora mengine aliangukia Kitunda, machimbo, Kisarawe, Mbagala, Kigamboni, Tabata Segerea, Kimanga, Pugu Kichangani, Mwisho wa Lami na Pugu Kwalala, Majohe na Kipunguni.

  Kwa mujibu wa JWTZ, jumla ya magahala ya silaha 23 yaliteketea kwa moto na kwamba sasa wanafanya kazi ya kukusanya mabaki ya mabomu yaliopo katika makazi ya watu.
   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,391
  Trophy Points: 280
  lingetua pale masaki coco beach anapoishi sasa!
   
 3. Kituku

  Kituku JF-Expert Member

  #3
  Feb 20, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 239
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Naona hapo bendera ingepepea robo mlingoti
   
 4. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #4
  Feb 20, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Kweli hakuna haki hapa duniani...
  Badala ya mabomu kupiga siku Pinda yupo maskani kwake yamepiga wakati hayupo...
  Unajua haya mabomu yangeangusha angalau kigogo mmoja wa JK lazima mtu angewajibishwa kwa kujiuzulu. Lakini ndo hivyo tena roho za watu zimepotea, tumeahidiwa sanda, majeneza na gharama za mazishi na mkwere kwa msisitizo kasema HAKIKISHENI MNAGHARIMIA USAFIRI WA MAREHEMU WAKAZIKWE KOKOTE NDUGU WANAKOTAKA. Tayari stori imeisha, baada ya wiko moja hakutakuwa hata na headlines katika magazeti halafu tunasahau jumla tunarudi katika business as ussual
   
 5. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #5
  Feb 20, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hivi hata maombolezo hayajatangazwa na utawala wetu ama SIJASIKIA!
   
 6. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #6
  Feb 20, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Hiyo ndiyo imetoka tungoje ya Ubungo!!
   
 7. Kituku

  Kituku JF-Expert Member

  #7
  Feb 20, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 239
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tusubirie mlipuko wa Lugalo labda watasema maombolezo ya kitaifa... maana wanaita janga la kitaifa ila kwa kuwa limeondoka na watu 17-35 hakuna maombolezo... labda lingemuangukia kigogo mmoja ndo lingeitwa siku ya maombolezo!!!
   
 8. Kituku

  Kituku JF-Expert Member

  #8
  Feb 20, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 239
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  Wamekufa watu wa vipato vya chini... serikali haina maombelezo kwa wanyonge...labda lingegusa familia ya kigogo
   
 9. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #9
  Feb 20, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Safari hii nasikia hakuna hata askari aliyedhurika jambo linatoleta maswali zaidi.

  Halafu askari wa kibongo hawana tofauti na mbwa, no brain kabisa.
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Feb 20, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Inawezekana walikuwa na habari za ki intelligensia kwamba kukaa kambini kila jumapili sio busara! Wakahama kwa ujumla wao...
   
 11. P

  Pokola JF-Expert Member

  #11
  Feb 20, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  A very interesting observation. Do you know what "Phasing Out" means? Well, that is it. Not a very complicated Military Jargon!
   
 12. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #12
  Feb 20, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,826
  Likes Received: 553
  Trophy Points: 280
  hili nalo neno....coz wao ni muhimu mno kuliko sisi walala hoi.Vifo vya walalahoi angalau 100,ndivyo vinavyoweza kusababisha kupepea bendera nusu mlingoti,lakini 20 wachache mno!
   
 13. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #13
  Feb 20, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Interesting...naona watu wanahasira mpaka wanatamani ubungo substatpion ilipuke na mitambo ya do! Once
   
 14. S

  Samat Member

  #14
  Feb 20, 2011
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mmh, kumbe waziri mkuu ana makazi na pugu pia? me nilijua masaki/oysterbay
   
 15. chipanga

  chipanga JF-Expert Member

  #15
  Feb 20, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 661
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 60
  Mh! ...huyu jamaa si alisema hana nyumba!? kwamba hata akienda kwao likizo huwa anafikia nyumbani kwa baba yake kwenye kile kile chumba alichokuwa analala akiwa mtoto..? KUMBE ana mansion pugu!!
   
 16. beatrixmgittu

  beatrixmgittu Senior Member

  #16
  Feb 20, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 113
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lingekuwa tetemeko la ardhi wangefuta picha?? Hii nchi bana!!
   
 17. menyidyo

  menyidyo JF-Expert Member

  #17
  Feb 20, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 1,339
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  hajafA COMED
   
 18. Seto

  Seto JF-Expert Member

  #18
  Feb 20, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 961
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Haya mabomu nayo hayasikii kilio chetu mi nilijua kombora limfumue mkerewe pale ikulu tufanye uchaguzi upya mwaka huu.
   
 19. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #19
  Feb 20, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Anaulizi wa Sheikh Yahaya....
   
 20. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #20
  Feb 20, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  mpaka afe kiongozi ndio utasikia maombolezo. Hata Spika alisema hii siyo dharula kwa hiyo ccm wameendelea na utaratibu wao wa kupuuza maisha ya raia wa nchi hii.
   
Loading...