Mabomu ya Marekani Mwezini Yashindwa Kuonyesha Cheche Zake

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,112
3299774.jpg

Watu waliokesha ili kuliona tukio hilo California, Marekani Saturday, October 10, 2009 1:37 PM
Baada ya kushindwa kurudi tena mwezini, Marekani ilipiga mabomu mawili mwezini katika utafiti wao wa kutafuta maji mwezini, lakini mambo hayakuwa kama wao walivyodhania yangekuwa. Mpango wa shirika la utafiti wa anga la Marekani, NASA, kuupiga mabomu mwezi ambao uligharimu kiasi cha paundi milioni 49 ( Zaidi ya Tsh. Bilioni 100) ulifanyika jana lakini haukuenda kama ulivyotarajiwa.

NASA ilitarajia mabomu hayo yangetimua vumbi la kifusi cha mwezi ambalo lingesambaa umbali wa kilomita 10 na hivyo watu wangeweza kuliona tokea duniani kwa kutumia darubini lakini mambo hayakuwa kama walivyotarajia.

Video iliyotolewa na shirika la utafiti wa anga la Marekani, NASA, kabla tukio hilo kuonyesha jinsi milipuko hiyo itakavyokuwa, ilionyesha kwamba baada ya milipuko hiyo maji na vumbi la ardhi ya mwezi yangerushwa juu na kuonekana Live lakini hali hiyo haikutokea, hakukuwa na chochote kilichoonekana na hivyo kuwahuzunisha mamilioni ya watu waliokesha usiku kushuhudia tukio hilo.

Picha za mwanzo toka mwezini hazikuonyesha dalili yoyote ya mlipuko kwenye mwezi pamoja na kwamba mabomu hayo yalilipuka kweli mwezini na kusababisha shimo kubwa kama ambavyo NASA ilitarajia.

Mamilioni ya watu waliangalia live tukio hilo kwenye internet wakati kombora la tani mbili linaloitwa Centaur lilipokuwa likiukaribia mwezi.

Awali NASA walikuwa wakitegemea kwamba kombora la kwanza lingetifua tani 350 za vumbi la kifusi cha mwezi na kuacha shimo kubwa lenye ukubwa sawa na robo tatu ya ukubwa wa uwanja soka.

NASA ilitangaza kwamba wataonyesha LIVE mlipuko huo utakavyotokea lakini mamilioni ya watu waliachwa wakiulizana maswali mengi baada ya kushindwa kuona chochote.

NASA ilitangaza kwamba mpango wao wa kupiga mabomu mwezi ulimalizika kwa mafanikio na nusu saa baada ya milipuko hiyo mwezini waliweka picha za tukio hilo kwenye tovuti yao.

Awali NASA ilitangaza kwamba matokeo ya utafiti wao kuthibitisha kama kuna maji au hamna kwenye mwezi, yangetolewa ndani ya lisaa limoja baada ya milipuko hiyo kutokea lakini hivi sasa wanasema kwamba itawachukua wiki mbili kuvifanyia uchunguzi vipimo vilivyopatikana kabla ya matokeo kamili kutangazwa.

Chini ni video inayoonyesha jinsi mabomu yalivyolipuwa mwezini jana.


VIDEO - Mabomu ya Marekani Mwezini Yashindwa Kuonyesha Cheche Zake http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3299774&&Cat=2







email.gif
 
Duh!! hadi mwezi tena wanaushambulia na mabomu!!
bora wange Drill-kama vipi wangechimba kisima...
O2 ya kutosha wame ipata wapi...??
 
Back
Top Bottom