Mabomu ya machozi yarindima Dodoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabomu ya machozi yarindima Dodoma

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by LWAKAPISI, Apr 7, 2011.

 1. LWAKAPISI

  LWAKAPISI Member

  #1
  Apr 7, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ilikuwa majira ya saa 6.30 mchana leo,katika viwanja vya bunge mjini Dodoma,kama ilivyotangazwa kuwa leo mkoani hapa wananchi wafike ukumbi wa P.Msekwa ili kutoa maoni yao juu ya muswada wa katiba mpya.Wito huo uliitikiwa na watu wengi hasa wanafunzi wa vyuo vikuu.Katika hali isiyotarajiwa ilitolewa taarifa kuwa ukumbi umejaa,kitu kilichowafanya wananchi hao kuoji iweje ukumbi ujae wakati tangazo lilitoka likiwakaribisha watu wote.Baadhi ya wanaosadikiwa kuwa ni wanavyuo waliokuwa kama mia200 walianza kupiga kelele za kutaka kuingia huku wakiimba nyimbo na kudai wamechakachuliwa.Baada ya mabishano ya muda na polisi ndipo alifika mkuu wa mkoa na ghafla aliamuru F.F.U wakaanza kupga mabomu ya machozi hewani na kusababisha watu kukimbia ovyo.Taarifa zilizotolewa na kituo cha televisheni ya taifa cha tbc1 zinadai walioanzisha shelabela hilo ni wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma(UDOM)
   
 2. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #2
  Apr 7, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Wamepiga ya machozi tu, wanafunzi wakakimbia ina maana hawajayazoea tu...
   
Loading...