Anna Nkya
Member
- Oct 21, 2021
- 69
- 341
Nimesoma Twitter, Zitto Kabwe akitoa maoni kuhusu umeme.
Zitto anasema katika miaka mitano iliyopita hatukuongeza uzalishaji wa umeme wa maji na ukweli ni kwamba uzalishaji ulipungua. HILO LILIKUWA BOMU LA KWANZA LA SERIKALI YA WAMU YA 5 ambalo lazima kuna siku lingelipuka. Hili hapa linalipuka, Rais Samia ndiye yuko madarakani
Wakati huo hatukuwa tunafanya ukaratabati wa miundombinu ya umeme. Hivyo tulikuwa tunatumia mbinu za muda mfupi kujikinga na janga. Namaanisha, tulikuwa hatukarabati kwa hofu kwamba ungekatika kwa wakati ule, lakini kukatika kule kungekuwa kwa muda mfupi tu. NI BOMU LINGINE, Linalipuka Rais Samia akiwa madarakani.
Tuwe wa kweli, ni kipindi kirefu hatujaona jua kali kiasi kilichopo sasa. Wenzetu waliopo Dar wanaweza kueleza zaid.
Jua kali hivi lazima liathiri vyanzo vya maji, na hivyo kauthiri uzalishaji wa umeme pamoja na upatikanajia wa maji majumbani. BOMU LINALOTISHA HAPA ni kwamba tumewekeza sana kwenye umeme wa maji. Kule Rufiji tuna mradi wa zaidi ya trilioni 6.
Je, tuna uhakika mradi ule hautapigwa na athari za mabadiliko ya tabianchi? NADHANI NI BOMU HILO kwa maana naamini Rais Samia angetumia fedha zilizoelekezwa Rufiji kuwekeza kwenye gesi na vyanzo vingine vya umeme. Lakini Serikali iliyopita ilishafika hatua ambayo Samia hana uchaguzi zaidi ya kukamilisha mradi ule.
IMANI YETU KUBWA: Rais Samia atategua vyema mabomu haya na tutavuka salama. Kila la heri Rais wetu mpenndwa.