"Mabomu" ya ajira ya Lowassa yameanza kulipuka Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"Mabomu" ya ajira ya Lowassa yameanza kulipuka Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by FUSO, Oct 22, 2012.

 1. F

  FUSO JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,867
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  Wakuu,


  Kuna vijana wengi hawana kazi, wanasubiri chochote kitakachotokea mtaani ili wachukulie faida (advantage), leo hii mimi nikitaka naweza kabisa kuwajaza ujinga vijana wa kimachinga wapiganie haki zao ikiwamo ardhi, elimu waliyonyimwa na taifa , makazi yaliyo bora n.k

  Hili ndilo bomu ambalo EL alilotabiri kwamba litalipuka, DR. Slaa pia ameshagusia jambo hili kwamba kuna siku hapa nchini hakutakalika,

  La juzi ni bomu la dini tu, lakini tunajua BOMU kubwa linakuja la kukosa ajira, maisha magumu mno kwa vijana. As of now vijana wameona hawana thamani tena na maisha yao, wako tayari kwa lolote lile na ndiyo maaana ni rahisi mno kuwatumia vijana kufanya chochote kile katika nchi hii.

  Hata mimi sina uwezo tu ningeanzisha taasisi nawapa vijana elfu tano tano nchi nzima project ambayo ingenigharimu kama mil 500 tu approx, kupigania ardhi yao iliyoporwa na wageni, migodi na hata wageni wanaofanya kazi ambazo wazawa wanaweza kuzifanya - hapa ndipo tulipofika.

  i MEAN unaweza kabisa kununua watanzania hasa vijana 20 - 45 kwa pesa kidogo tu na ukafanikisha lengo lako

  Baba wa taifa aliweka misingi mikuu kuhusu hili lakini kwa sasa hakuna kitu, kila mtu mwenye pesa au anapata pesa toka kokote duniani anaweza kufanya mambo haya. kama taifa lazima tutafakari, tuweke mjadala wa wazi tusitegemee serikali hii legelege - tutajichinja bila sababu za msingi wakati wote ni ndugu moja.

  Mimi sijawahi kuona waislam wenye jazba kama hizo, nafikiri kulikuwa na move at the background, serikali kama mzazi lazima waanzie hapo kufanya kazi yake rather than kutumia chombo chake aka jeshi la police ambalo lina tuhuma lukuki eti kuweka mambo sawa, tupo kwenye hali tete wakuu.
   
 2. Vijisenti

  Vijisenti JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2012
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 476
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Dah umeniweza sana mkuu, yaani nilishtuka maana kuna ndugu zangu wako chuoni huko Mbeya.

  By the way hata hili linaloitwa la udini linachochewa zaidi na ugumu wa maisha unaotokana na siasa Mbaya.

  WATU HAWANA CHA KUPOTEZA.
   
Loading...