Mabomu, risasi za 2015 bado hazijatumika

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898
MWIGULU Lameck Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi amesema kuwa kutokana na ugumu wa uchaguzi wa mwaka jana, serikali ililazimika kujiandaa kwa lolote, ikiwemo kununua vifaa vya kijeshi na kiusalama hata hivyo vyote hivyo havikutumika, anaandika Dany Tibason.

Kauli hiyo imetolewa na waziri huyo alipokuwa akizungumza na viongozi wa dini wakiwemo maaskofu na wachungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilitheri Tanzania (KKKT) mkoani Dodoma.“Kwa hofu ya uchaguzi, serikali ilinunua magari ya washawasha na mabomu na vifaa vingine vya kiusalama huku mataifa ya nje yakiwa yakiwa yanatazamia kuwa lolote linaweza kutokea ikiwa ni pamoja na kutokea kwa vurugu na kupotea kwa amani.

Jambo la uhakikika ni kuwa vifaa hivyo havikutumika hata kidogo. Vipo na havijafanya kazi, ni ukweli usiopingika kuwa amani iliyopo inatokana na maombi ya viongozi wa dini kwa kutumia muda wao mwingi kuliombea Taifa,” alisema Waziri Mwigulu.

Sambamba na hilo, Mwigulu alisema kuwa, serikali inategemea sana taasisi za dini katika kuhamasisha amani nchi hivyo inatopotokea migogoro ndani ya taasisi hizo na kusababisha Jeshi la Polisi kuingilia kati serikali inajikuta katika wakati mgumu.

“Serikali inasimama au kupata amani kutokana na maombi ya viongozi wa dini hivyo si jambo jema ndani ya taasisi za dini kujiingiza katika migogoro hadi kufikia hatua ya Jeshi la Polisi kuwarushia mabomu,” alisisitiza.

Kwa upande wake Dk. Frederick Shoo, Mkuu kanisa la KKKT, alisema kanisa linatimiza majukumu yake ya kuwahudumia watu kimwili na Kiroho.

Hata hivyo, aliitaka serikali kutowaingilia viongozi wa dini pale wanapoishauri au kuikemea.

“Viongozi wa dini, tupo kwa ajili ya kuwajenga watu kimwili na kiroho lakini pale ambapo tunawakosoa hata kama msipopenda inabidi mkubali na si kutushukia au kutuambia kuwa tusichanganye dini na siasa kwani huo ni wajibu wetu,” alisema Dk. Shoo.

Chanzo: Mwanahalisi
 
Watu wakishapata madaraka wanajisahau sana, kiongozi mzima anaongea kwa kurahizisha eti silaha hazijatumiaka...

Huwezi kuamini kuwa anamaanisha hizo silaha hazijatumika kwa mama zake, Baba zake, Dada zake, Kaka zake Bibi Na Babu zake.

Viongozi wetu waache ulevi wa madaraka kujiona wao ndio bora kuliko wananchi wa kawaida.

Hizo silaha zikianza kutumika hata wao wenyewe Na familia zao hawatakua salama, unaweza kumkimbiza mke Na watoto wako nje ya nchi lakini Baba,mama, Dada,shangazi,na Ndugu wengine watakua wahanga wa hizo silaha unazojivunia.

Kovu ambalo litamuumiza Na yeye kwa kipindi cha uhai wake wote.
 
Amani ya nchi yetu imesababishwa na busara na utulivu wa vyama vya upinzani, na uvumilivu huo na Busara vimesababishwa na maombi ya viongozi wetu wa dini. Lakini ule upande wa pili uko tayari kuua na ndio maana umejiandaa kwa silaha za kijeshi.
 
Watu wakishapata madaraka wanajisahau sana, kiongozi mzima anaongea kwa kurahizisha eti silaha hazijatumiaka...

Huwezi kuamini kuwa anamaanisha hizo silaha hazijatumika kwa mama zake, Baba zake, Dada zake, Kaka zake Bibi Na Babu zake.

Viongozi wetu waache ulevi wa madaraka kujiona wao ndio bora kuliko wananchi wa kawaida.

Hizo silaha zikianza kutumika hata wao wenyewe Na familia zao hawatakua salama, unaweza kumkimbiza mke Na watoto wako nje ya nchi lakini Baba,mama, Dada,shangazi,na Ndugu wengine watakua wahanga wa hizo silaha unazojivunia.

Kovu ambalo litamuumiza Na yeye kwa kipindi cha uhai wake wote.
MBONA MAISHA HUKU MTAANI YANAWASHAWASHA NA HAYA TUTAWASHWA MPAKA 2020
 
Ametoa kauli isiyofaa kabisa, Amani haijengwi kwa kununua SILAHA ili kupambana na Wananchi, Viongozi mliokuwa mmejiandaa kutumia hiyo njia mlikosea sana na mnatakiwa kutuomba Watanzania msamaha kwa mlichotaka kutufanyia
 
Mwenyezimungu huwa anajibu dua za wote wanaomuomba hata kama siyo kiongozi wa dini.
 
Hawa ndo aina ya viongozi tulionao....hata hawajisumbui kupima athari ya maudhui ya watakayoyanena....
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom