Mabomu Mbagala/Gongolamboto, Mabomu Arusha May/June, Gorofa kuanguka 2008/2013, Kibanda/Ulimboka n.k | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabomu Mbagala/Gongolamboto, Mabomu Arusha May/June, Gorofa kuanguka 2008/2013, Kibanda/Ulimboka n.k

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mutabilwa, Jun 19, 2013.

 1. mutabilwa

  mutabilwa JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2013
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 305
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wa Jf napenda kuleta Thread hii tujadili jinsi Serikali hasa viongozi wasivyo na nia wala hata chembe ya kupima uwajibikaji wao hasa mambo maovu yanayowaumiza wananchi yanapotokea zaidi ya mara mbili. Tutakumbuka mabomu ya Mbagala yalivyowatesa wananchi na viongozi kuahidi yasingetokea tena lakini kilichisikitisha na kujirudia kwa tatizo hilohilo kule Ngongolamboto, Tutakumbuka Gorofa lililoanguka 2006 na tume kuundwa lakini tumeshuudia tena likitokea jambo kama hilo mwaka huu, tutakumbuka kuteswa na kujeruhiwa kwa ulimboka mwaka jana na tena mwaka huu kujirudia kwa kuteswa kwa Kibanda, tumeshuudia mambomu yalivyoua kule arusha mwezi jana Kanisani na kujirudia tena kwenye mkutano wa Chadema.
  Haya ni mambo tu machache niliyoweza kukusanya, lakiini kinachonisikitisha ni hatua zinazochukuliwa na viongozi wetu juu ya matatizo yanayowakumba wananchi, picha ninayoweza kuiweka kichwani Mwangu ni Ukosefu wa uwajibikaji na kujituma kwa Serikali juu ya mambo muhimu ya kitaifa ambayo kimsingi chanzo chake ni UDHAIFU MKUBWA nasema MKUBWA sana uliopo kayika serikali na chama Tawala CCM na ndipo ninapokumbuka maneno ya Mwl Nyerere alisema Chama LEGELEGE uzaa Serikali LEGELEGE.
  Hitimisho langu ni wananchi kubadilika na kuwa wakali juu ya serikali na kuwa na nguvu ya kuiondoa au kuiweka serikali itakayotekeleza matakwa ya wananchi.

  Asanteni!!!!!
   
Loading...