Mabomu Gongo la Mboto: Mwinyi asema hajiuzulu

Rev Kweli jamaa kasema ukweli maana hawana uchungu na nchi hao, Tuchukue Tanganyika yetu maana tunajua uchungu wake sisi watanganyika na watu wetu...Mwinyi ni Mzanzibar kweli kwani uongo? Well said and kweli
 
mmmh...yaani Vuai na Mwinyi......hivi kumbe nilikuwa nimelala eeeh....asante kwa kuniamsha
 
Rev Kweli jamaa kasema ukweli maana hawana uchungu na nchi hao, Tuchukue Tanganyika yetu maana tunajua uchungu wake sisi watanganyika na watu wetu...Mwinyi ni Mzanzibar kweli kwani uongo? Well said and kweli

Mkuu kwa hiyo una taka kusema kwenye wizara hizo kunge kuwa na "Mtanganyika" baasi maafa kama ya Gongo la Mboto yasinge tokea? Mbona wizara zinazo ongozwa na "Watanganyika" nazo stori ni zile zile mfnao ni Nishati na Madini iliyo tuletea Dowans inaongozwa na Ngeleja.

Tukumbuke jamani kwenye serikali ya Muungano wengi ya viongozi ni kutoka huku huku bara kwatu lakini hatuoni tofauti yoyote. Chini ya serikali tuliyo nayo sasa mimi sioni tofauti za kiutendaji kati ya wizara zinazo ongozwa na Wabara na Wazenji.
 
Tuweke record sawa:

Wizara ya Ulinzi na ile ya Mambo ya Ndani; viongozi wao ni CDF na IGP respective mawaziri ni ceremonial title hawa wote CDF na IGP wako wana-report directly kwa Amir Jeshi Mkuu.

So it doesn't matter hizi wizara ziko chini ya waziri Mzanzibar, Mdanganyika, Mngazija... responsibel personnel are CDF and IGP respectively.
 
Baba yake Hussein, Raisi Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, alijiuzulu kwa mauaji ya vikongwe huko Shinyanga, kwa nini asimshauri mwanae aige nyao zake? Hussein Ali Hassan Mwinyi, ona aibu na jiuzuru hata kwa kwa heshima ya baba yako tu. Unang'ang'nia kugombea uraisi 2015? Nakuambia huupati hata kwa kuiba kura maana hazitakuwepo za kuibiwa.
 
WANANCHI HATUKO SALAMA TENA NA MALI ZETU, KIIO KILA LEO NA MAYATIMA
KUONGEZEKA HIVYO SERIKALI NZIMA IJIUZULU HATA KABLA YA MAANDAMANO
YA KUTETEA 'UHAI WA WENZETU' KUANZA KOTE NCHINI

Mheshimiwa Kikwete kama amiri jeshi mkuu ajiuzulu pamoja na serikali yake. Jukumu la msingi halijazingatiwa; wananchi hatuko salama!! Tusianze kuzungusha kiswahili hapa ni uhai umepotea kwa uzembe!!! Hawa mayatima wanahitaji sauti zetu!!

Hatutaki tena tume kwa hata kule Mbagala chombo kama hicho hakikutusaidia zaidi ya kuwapa wanasiasa na makampuni ya kibiashara kujinadi kwenye kioo cha televisheni mgongoni mwa msiba na damu kwa wengine.

Jukumu la kwanza la kuhitajika uwepo wa serikali katikati yetu NI KUHAKIKISHA USALAMA KILA MMOJA WETU NA MALI ZETU. Kwa mtaji hizi picha nilizoona, serikali nzima ya CCM ijiuzulu mara moja

Mauaji Arusha walitupuuza kana kwamba kuliuaua nzi tu. Kule kwenye mashamba ya mpunga wala hawakujishughulisha kitu kuwajibika mtu. Sasa kama kweli kuna JAMBO AMBALO KIUKWELI KABISA KINATUHITAJI KUANDAMANA MPAKA KUELEWEKE NI KATIKA KUTETEA UHAI WA WENZETU.

Kama tutaona vifo hivi kama vile ni ya 'akina wale' na kwamba sisi wengine hatuhusiki basi hapo ndipo kiama chetu kinapoanzia. Kwa vifo hivi vyote 17 taifa tumepata yatima wangapiii?????????????
 
Mkuu kwa hiyo una taka kusema kwenye wizara hizo kunge kuwa na "Mtanganyika" baasi maafa kama ya Gongo la Mboto yasinge tokea? Mbona wizara zinazo ongozwa na "Watanganyika" nazo stori ni zile zile mfnao ni Nishati na Madini iliyo tuletea Dowans inaongozwa na Ngeleja.

Tukumbuke jamani kwenye serikali ya Muungano wengi ya viongozi ni kutoka huku huku bara kwatu lakini hatuoni tofauti yoyote. Chini ya serikali tuliyo nayo sasa mimi sioni tofauti za kiutendaji kati ya wizara zinazo ongozwa na Wabara na Wazenji.

Mkuu sina maana hiyo kuwa wangekuwa watanganyika yasingetokea ila ni kwamba jamaa mwinyi kasema kule mbagala janga kama hili halitatokea tena maana tumejihadhari, je anakula matapishi yake? Aachie ngazi basi maana yalotokea ni zaidi ya mbagala hala wao na rais wake wanachekacheka tuuuu....
 
Ndugu wan JF,
Tangu madhara ya mabomu yalipowekwa jamvini, kumekuwa na michango ya kimawazo kutoka kwa wadau mbali mbali yenye tija na kufikirisha.
Kwa ujumla wetu sote tunakubaliana kuwa bomu kama kifaa haliwezi kulipuka endapo tu hakuna tatizo. Ni wazi kuwa kulikuwa na tatizo ndio maana mabomu yakalipuka. Mabomu yameua wananchi wasio na hati, raia waliokuwa wanandelea na maisha yao ya kila siku. Leo ni majonzi na simanzi miongoni mwetu, leo kuna walemavu wa kudumu kutokana na mabomu, leo kuna mayatima, leo kuna watu walioshinda na njaa kujenga nyumba zao,ghafla hawana nyumba.

Wito wetu kwa maoni ya wengi, lazima Mwinyi na mwingine awaye wawajibike. Wanawajibike bila ya shaka kwasababu ni mara ya pili uzembe huu unatokea machoni na madarakani mwao. Wawajibike kwasababu hatuna imani nao katika utendaji na hasa ulinzi na usalama wetu. Hatuwatuhumu kwa majina yao bali nyadhifa zao ambazo hatuwezi kuzitenga na majina yao.
Sauti zetu za pamoja zilenge kushinikiza haki itendeke.
Ninashangazwa na jambo moja na sijui kuwa ni watu binafsi au ni MoD aliyeamua hivyo. Thread ya Mwinyi (kutojiuzulu) ni kauli yake. Leo kuna thread nyingine imeunganishwa ''Wizara (mambo ya ndani na ulinzi) chini ya wazanzibar'' yenye mtazamo tofauti kabisa na Original thread. Sijui ni kwa makusudi au bahati mbaya, thread hii imelenga kutuondoa kwenye hoja ya msingi aliyotoa Waziri Mwinyi mwenyewe. Mjadala umehamia kwenye uzanzibar/Udini n.k. Nadhani kuna watu wamepewa kazi ya kuua fikra njema zenye nia njema na nchi yetu. Waathirika wa mabomu ni Watanzania na wala hatutaki kujua kabila zao au dini zao. Ni wenzetu wazee, vijana na watoto wanaopata mateso ambayo mwanadamu mwenye akili timamu hafai kuyafanyia mzaha au siasa.
Ninawaomba wale wenye lengo la kutuondoa katika mada muhimu ambayo ni Kumtaka Waziri Mwinyi na viongozi wenzake wajiuzulu, watupishe ili tuendelee kujadili mambo yenye heri na tija kwa mustakabli wa taifa leo. Uhuru wa mawazo upo na tunaomba waondoe thread yenye kutupotosha na waiweke mahali panapofaa ili kutoa nafasi kwa kila mtu kuchagua asome au achangie nini.
MoD tafadhali angalia jambo hili.
 
mkuu wa nchi alishaambiwa kuwa yanunuliwe mengine hayo ya mwaka 1972 yaondolewe jibu mnalijuwa!
Kudharau ripoti ya wataalamu wa amary kuwa mabomu yalitakiwa kuwa disposed safety, hivyo ililazimu kukodi wataalamu kutoka nje ya nchi kwa kushirikiana na wetu ili yateketezwe kwa kisingizio cha gharama! Kutokana na hilo maghala yaliyopo Ngerengere na Tabora yapo katika hatari kama ya Gongo la Mboto!
Unaruka majivu unakanyaga moto, unakwepa gharama ya kutegua mabomu unalipa gharama ya uharibifu wa mabomu pamoja na vifo ambavyo huwezi kufidiz!
 
Yeye ni mchoma sindano (Daktari), mambo ya ulinzi wapi na wapi?
Lazima aharibu kazi kwa sababu anajifunza kwanza badala ya kufanya
 
Atawajibikaje kama hawajibishwi? Dr. Slaa mbona yupo kimya? Neno moja tu la Slaa linaweza kubadilisha hali ya hewa.
 
Dr.Mwinyi ni daktari mzuri sana wa binadamu.
Kwanini asijiuzulu tuu akaenda kutibia raia wake, angeokoa maisha ya Watanzania wengi sana na Mungu angemlipa kuliko kuhusika na kashfa ya vifo vingi namna hii.

Ninavyofahamu baada ya kutoka ktk masomo ya udaktari,alikimbilia ktk siasa. Sasa kwamba ni daktari mzuri sijui hizo taarifa umezipata wapi? Kwa issue ya kujiuzulu,sidhani. Maana boss wake analipa fadhila. Alitolewa Liwale akateuliwa kuwa mbunge,na bdae akawa naibu waziri na mzee Mwinyi. Na sitashangaa kama boss wake anamuandaa kwa ulaji wa juu zaidi hapo 2015.
 
Mubaraka alibana kisha akaachia baada ya kuzidiwa na
nguvu ya uma sembuse huyu kifaranga wa ali, peoples
power is coming so mwinyi must go either he like or not.
 
Back
Top Bottom