Mabomu Gongo la Mboto: Mwinyi asema hajiuzulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabomu Gongo la Mboto: Mwinyi asema hajiuzulu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nguruvi3, Feb 18, 2011.

 1. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #1
  Feb 18, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,219
  Likes Received: 7,338
  Trophy Points: 280
  Nimemsikia waziri wa Ulinzi Mh Hussein Mwinyi akihojiwa na VoA swahili. Pamoja na maswali mengine ameulizwa kuhusu kuwajibika kwa kujiuzulu.
  Mwinyi: Kujiuzulu kunatoka na makosa yaliyofanywa na mamlaka iliyoko chini ya mtu kama itadhihirika. Tusubiri tume itakayoundwa na tupate matokeo yake kwanza.

  My Take:
  1. Hili ni tatizo la pili kutokea. Tume ni ya nini ikiwa ile ya kwanza hatukujua nini kilifanyaka?
  2. Tunajua kuwa njia rahisi ya kiongozi asiyeweza kupambanua mambo ni tume ili kutengeneza mazingira ya kutengeneza hadithi.
  3. Mh Mwinyi anataka kutufanya Watanzania mbumbumbu sana.
  Dhana(concept) ya kuwajibika ina maana zaidi ya moja.
  a) Kuwajibika kwa makosa ya watendaji kisheria kama alivyosema yeye Mwinyi.
  b) Kupisha uchunguzi halali usioingiliwa na wale wanaochunguzwa
  c) Kuonyesha machungu au kutoridhika kwa kile kilichotokea, na hapa ni vifo huku
  kiongozi husika akiwa na dhamana.(sympath)

  Zote (a), (b), (c) zinamgusa Mh Mwinyi moja kwa moja. Wakati leo kuna watu wana misiba mizito majumbani kwao, wengine wapo mahospitalini, watoto hawajui wazazi wapo wapi, mali zimeharibiwa na watu hawajui nini cha kufanya, makazi hakuna watu wapo kwa majirani, hivi kweli hata kama kifungu (a) na (b) hapo juu hakimhusu kiongozi, je kifungu (c) cha kuonyesha huruma na machungu nacho pia kiongozi hawezi kukifanya!!! Yaani hata huruma ya madhara yatokanayo hakuna!!, eti kwasababu tu mtu abaki kuwa waziri.

  sad!!!
   
 2. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Hii nchi bwana acha tu maskini tunazidi nyanyasikia
   
 3. Double X

  Double X Senior Member

  #3
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  UYU waziri wa ulinzi ni ovyo kabisa anasubiri tume itoe majibu mbona tume ya mbagala hamjatuambia ilichogundua, shame on u!!!
   
 4. n

  niweze JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ooo tume ije ili Mwinyi ageuze ukweli kuwa uongo. Thats how "Truth Flip in Tanzania" huyo Mwinyi mwenyewe ndiye atakuwa na input on all these"
  Ukweli, wamemuandaa Mwinyi kuwa raisi na hataki kuchafuliwa jina ili awadanganye tena. Kwani Lowasa si alijiuzuru na leo si anaongoza kamati ya usalama na mambo ya nje?

  [​IMG]
   
 5. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #5
  Feb 18, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tanzania hakuna uwajibikaji!
   
 6. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #6
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hussein Hassan Mwinyi mtoto wa Ally Hassan Mwinyi - open your mind!!!
   
 7. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #7
  Feb 18, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Naanza kujihoji kama huyu jamaa ni mtoto wa mzee A. H. Mwinyi. kama ndivyo ina maana hakurithi hata kidogo ka-busara kutoka kwa baba yake. Mbona baba yake alijiuzulu na baadae akaja kuwa rais?
   
 8. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #8
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hadi mtakapojua kuwa nyie ndiyo wenye mamlaka ya kumweka mtu madarakani au kumtoa. Kwa vile bado nyie masikini mmegeuka watumwa wa watala, hakuna lolote mnaloweza kulifanya!

  Very sad!
   
 9. t

  toxic JF-Expert Member

  #9
  Feb 18, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 773
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  He can't bcoz he is a FAILURE.
   
 10. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #10
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kujiuzulu au la kunategemea na boss. Kwa dizaini ya boss tuliyenaye ambaye hajui A, B wala C ya nini anatakiwa kufanya, suala kama hilo la kujiuzulu ni ndoto za alinacha. Labda wenye mamlaka waamue kufanya kweli kama alivyofanya yule machinga wa Tunisia!
   
 11. d

  dotto JF-Expert Member

  #11
  Feb 18, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  mkuu wa nchi alishaambiwa kuwa yanunuliwe mengine hayo ya mwaka 1972 yaondolewe jibu mnalijuwa!
   
 12. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #12
  Feb 18, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Tumerogwa hatuna uthubutu
   
 13. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #13
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,467
  Likes Received: 4,126
  Trophy Points: 280
  Jamaa anang'ang'ania nini? Na tume ya nini wakati inaonyesha kabisa kuwa kuna uzembe ulifanyika. Huyu jamaa ana matatizo sana, milipuko yote imetokea chini yake halafu anasema eti tusubiri tume....
   
 14. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #14
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 280
  Tanzania a country full of cowards.
   
 15. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #15
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Kama yeye Mwinyi na Mwamnyange hawataki kujiuzuru, JK anatakiwa awe bold na kuwafukuza kazi leo hii na wala siyo kesho
   
 16. regam

  regam JF-Expert Member

  #16
  Feb 18, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 268
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kaazi kweli! Nchi hii ni rahisi sana kuiongoza maan wananchi wake ni wapole, wakarimu nk. Tunaonyesha kukerwa na uwajibikaji wa viongozi wetu lakini kwa sababu ya upole tunaishia kusema " aaah Mungu anajuwa bwana!" Tunaendelea kuumia tuu.
  Hizo tume hazileti chochote maana zinateuliwa na haohao waliowaweka sasa unategemea nini? Tume zooooote za hapa kwetu huwa si huru kabisa, zinajengwa na dhana ya kulindana.
  Cha kujiuliza ni kwamba hivi ni tume gani iliyowahi kuundwa na kutoa ukweli? (Ukiondoa tume ya Richmond)
  Tutabaki kuumia tuu. Hata wale wanaodhani suluhisho ni 2015 wasahau. Kura zitachakachuliwa na itaundwa tume ya kuchunguza.
  Kutokana na uoga na unafiki tuliokuwa nao ya egypt hatuyawezi. Yaani pamoja na matatizo na mapungufu ya serikali yetu kuna mijitu bado inadhani tuko kwenye kampeni! Tutakufa bila kelele. Yaani huwa nakasirika sana!
   
 17. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #17
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,467
  Likes Received: 4,126
  Trophy Points: 280
  Yaani wanamuandaa yeye kuwa rais!!!! Wala hafai hata kidogo....
   
 18. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #18
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,173
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  anajiandaa kuwa rais.

  suala la kujiuzulu halipo kwenye list yake.
   
 19. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #19
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,467
  Likes Received: 4,126
  Trophy Points: 280
  Na Kikwete hawezi kuwafukuza kazi kwa sababu hatuna utaratibu huo, na tumetawaliwa na uswahiba sana....
   
 20. s

  seniorita JF-Expert Member

  #20
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  kama watu hatutaamka nchi hii, every day the truth will be twisted to another completely different story...."a fake truth" which is expected all to understand and take it....at the expense of peoples' life, jamani...why? and for how long?
   
Loading...