Manyerere Jackton
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 2,436
- 4,429
Ndugu zangu, matukio ya vurugu na mauaji katika Taifa letu sasa yamefikia hatua mbaya. Tararibu, tumeiona amani ya Tanzania ikizikwa kwa nguvu.
Kumekuwapo kurushiana maneno makali tangu kuanza mtiririko wa mabomu katika Jiji la Arusha. Kwenye tukio la Kanisani kukawapo maneno kwamba huenda ni Waislamu, lakini hoja hiyo ikapungua nguvu kutokana na taarifa kwamba kijana mwendesha bodaboda aliyempakia mlipuaji, ni Mkristo. Hapo kidogo mambo yakanywea.
Sasa limekuja hili la mkutanoni. Chadema na CCM sasa wanakaribia kutoana macho. Kila upande unadai upande ule ndiyo uliohusika. Polisi nao wameingizwa kwenye kadhia hii wakidaiwa kwamba walirusha mabomu na risasi za moto. Kuna ushuhuda wa hayo. Mwenyekiti Mbowe, naye hakwenda mbali na nadharia hiyo.
Ndugu zangu, tangu bomu lile la Kanisani, na sasa hili la kwenye mkutano wa hadhara wa Chadema, naanza kuungana na mtoa mada mmoja hapa JF aliyesema inawezekana "mhusika yuko pembeni anachekelea".
Kauli ya mtoa mada huyo ni ya msingi sana.Mimi najiuliza, kwanini mabomu yawe Arusha?
Nashawishika kwenda mbali kidogo na mtazamo wa wengi. Mimi nadiriki kuwatilia shaka ndugu zetu Wakenya kwamba isije ikawa hii ni vita ya kiuchumi.
Mtakumbuka kwamba Kenya wamekuwa mbele sana kuhakikisha Tanzania hatufanikiwi. Ujenzi wa barabara ya Mto wa Mbu-Musoma ni Wakenya waliokuwa wa kwanza kusimama kidete duniani kote kuendesha kampeni ya kuipinga. Wamefanikiwa.
Mtakumbuka suala la uuzaji mano ya tembo. Kenya walihakikisha wanatumia rasilimali zao zote kukwamisha mpango huo. Wakafanikiwa.
Ni Kenya hawa hawa ambao wamepinga ujenzi wa kiwanda cha magadi huku kwetu kwa kigezo kwamba kitaathiri mazingira ya hilo ziwa tulilogawana nao.
Kana kwamba haitoshi, Kenya wamehakikisha muda wote Loliondo haitulii. Wamediriki kuwaleta CNN, Al Jazeera na mashirika makubwa ya habari ndani ya loliondo kuandika kile wanachodai kwamba ni kuhamishwa kwa ndugu zetu Wamasai. Ikumbukwe kuwa kutokuwapo kwa amani Loliondo kunawasaidia kuendelea kunufaika kiuchumi kwa kuingiza mifugo yao na kuendesha mambo wanayoyataka.
Kenya wana hasira wakitaka mpaka wetu wa Ngologonja uliofungwa tangu enzi za Mwalimu, ufunguliwe. Serikali yetu, walau kwenye hili imekuwa imara. Imegoma.
Ndugu zangu, Kenya kwa sasa utalii wao umeathirika sana. Mabomu ya magaidi wa Al Shabab yameharibu sana utalii wao. Wameona watalii wengi wanamiminika Tanzania. Isije ikawa kwamba wameamua kuharibu huku kwetu na wakati huo huo wakiendelea kuvutia watalii kwao.
Ikumbukwe hapa kwamba sasa vyombo vya habari vya Kenya havitoa umuhimu mkubwa kwa matukio ya ugaidi nchini humo licha ya ukweli kwamba kila siku kuna mabomu yanalipuliwa na magaidi.
Ombi langu kwa Watanzania, isije ikawa tunashikana uchawi hapa wenyewe kwa wenyewe, ilhali mchawi mwenyewe yuko pembeni anatucheka.
Nayasema haya kwa sababu uchunguzi wa awali wa tukio la bomu Kanisani, umebaini kuwa bomu na wahusika walitoka Kenya. Taarifa hizi zipo ndani ya vyombo vyetu vya ulinzi na usalama. Pengine hawataki kuziweka wazi kwa hofu ya kuvuruga ujirani wetu.
Bado akili ya kawaida hainitumi kuamini kwamba CCM wamekuwa wabaya kiasi cha kuamua kuwaua Chadema. Tena basi, sidhani kama kweli kuna mwana CCM anaweza kutoa amri kwa polisi kulipua bomu ndani ya mkutano kwa mazingira yake tuliyoyashuhudia.
Isitoshe, napata shaka kweli kuamini kuwa bomu limerushwa na Chadema kwa madai hafifu kwamba waliona wanashindwa kwenye uchaguzi wa udiwani, hivyo walitumia bomu kuahirisha uchaguzi kama njia ya kukwepa aibu ya kushindwa! Haya yote yananipa shida kuyaamini.
Tuwe watulivu na tutumie busara sana kwenye mambo haya. Ushiriki wa Wakenya kwenye sakata hili si jambo la kupuuzwa. Tena tukumbuke kuwa hata M23 ambao tunapambana nao sasa, wanaweza kuwa na mkono wao. Tukianza kulaumiana wenyewe kwa wenyewe tutakuwa tunampa kicheko adui yetu.
Huu ndiyo mtazamo wangu.
Nawasilisha.