Mabinti wanabakwa

papaa2015

JF-Expert Member
Jul 12, 2012
411
100
wapendwa habari zenu!

Jana usiku nikiwa njiani natokea kwenye sherehe mida ya saa 6 usiku nilipita mitaa ya Buguruni,kilichonishangaza ni kwamba nilikuta mabinti wadogo chini ya umri wa miaka 18 wakiwa wamesimama pembeni.Badae nilielezwa kwamba wale ni mabinti wanaojiuze katika hiyo ambayo iko jirani na mataa ya Buguruni na Mandela,kilichonihudhunisha ni umri wa wale mambinti na hapo ndipo nilipopatwa na haya maswali;

Je,wale mabinti ni kweli wote hawana shughuli nyingine ya kuwaingizia kipato zaidi ya kujiuza katika umri mdogo na kuhatarisha maisha yao?

Je,mwenye bar hatambui kuwa ni kinyume na sheria kuruhusu watoto wadogo kuwa bar usiku wa manane na kuwauzia pombe pamoja na kuruhusu kuingia guest na wanaume?

Je,vijana wanaotarajia kuoa,hawa ndo wachumba watakaojenga nao maisha?

Nini hatma ya vita dhidi ya ukimwi na maisha ya vijana?

Lakini,kwa wanaume wanaotembea na hawa mabinti hawajui kwamba wanawabaka kulingana na umri wao kuwa mdogo kisheria kuweza kufanya makubaliano?

BONGO ZAIDI YA NIIJUAVYO......
 
Hilo nalo neno. Sasa unapendekeza nini kifanyike kamanda maana wataalamu wanatwambia kujua kuwa lipo tatizo ndo mwanzo wa kufikia ufumbuzi. Hao Bwana wanasubiria maisha bora kwa kila Mtanzania, kama sikosei chama tawala kilisema kitatoa ajira kwa vijana.

Sasa hapo ndo ukumbuke maneno ya Mwl. kwamba Ikulu ni mahala patakatifu, ukipita barabarani watu wana njaa huo ni mzigo wako, ukipita huko watu hawana nguo huo ni mzigo wako.

Kama unataka kushangaa kuliko hii ya Buguruni Nenda Dodoma wakati huu wa Bunge kabla halijaisha ndo utashangaa, wote wakuu wetu wa kaya wako huko.

TAFAKARI!!!!!!!!!!
 
Japo kuwa wazazi tunajitahidi kwa kila njia kuhakikisha tunayengeneza maisha mazuri kwa watoto wetu wapo watu ambao hawataku kuona maisha ya watoto wetu yakifanikiwa.

Kuna watu ni wazazi katika familia zao, hao wanataka watoto wao wapate elimu ilihali wao wao ndio wanao warubuni watoto wa wenzao. Japo wengine watasema ni "tamaa a mwanao" ila naamini kama yale anayomfanyia mtoto wa mwenzie yangefanyiwa kwa mwanae naamini angepiga kelele zisizo mithilika

Tatizo halipo tu kwa watoto bali kwa jamii inayowazunguka watoto hao. Kama jamii ingeficha makucha yake na kuwaacha watoto wasome kwanza naamini mambo yangekuwa mazuri kwa kila kizazi.
 
mi sa nyingine huwa najiuliza where are we going.......
things are rotten.....
sometimes I look at my kids na kumuomba mungu aepushie mbali....
 
Hilo nalo neno. Sasa unapendekeza nini kifanyike kamanda maana wataalamu wanatwambia kujua kuwa lipo tatizo ndo mwanzo wa kufikia ufumbuzi. Hao Bwana wanasubiria maisha bora kwa kila Mtanzania, kama sikosei chama tawala kilisema kitatoa ajira kwa vijana.

Sasa hapo ndo ukumbuke maneno ya Mwl. kwamba Ikulu ni mahala patakatifu, ukipita barabarani watu wana njaa huo ni mzigo wako, ukipita huko watu hawana nguo huo ni mzigo wako.

Kama unataka kushangaa kuliko hii ya Buguruni Nenda Dodoma wakati huu wa Bunge kabla halijaisha ndo utashangaa, wote wakuu wetu wa kaya wako huko.

TAFAKARI!!!!!!!!!!

mkuu,sheria ziko wazi nachodhani tatizo liko katika usimamizi wa sheria,ni wakati sasa serikali isimamie hizi sheria na watu wafikishwe mbele ya sheria.Suala si kuwakamata machangudoa tu bali tufike mbali kuwakamata hata wenye guest zinazotumika ktk biashara hii hasa zinazowahusisha watoto
 
Ni kweli tatizo linaanzia kwa jamii nzima,kuanzia malezi.Na mbaya zaidi ni pale unapokuta wateja ni watu wazima wanaostahili kuwa wazazi wa hao mabinti
 
Rais yupo singapore kujifunja namna ya kuanzisha Veta ili vijana wajifunze ufundi
 
Umri wao uliujuaje? Umri wa mtu haujulikani kwa kumtizama sura.

Yale mambo hayaihitaji umri wala nini, kama ana uwezo wa kumiliki jukwaa kuna tatizo gani?

Wengine hawataki shule, kuliko kukaa tu nyumbani si bora wakajishughulishe.
 
Rais yupo singapore kujifunja namna ya kuanzisha Veta ili vijana wajifunze ufundi

Hapo raisi anahusika vipi? Unataka raisi akufundishe malezi ya familia Yako.

Hao wengine wanatumwa na wazazi wao.
 
Umri wao uliujuaje? Umri wa mtu haujulikani kwa kumtizama sura.

Yale mambo hayaihitaji umri wala nini, kama ana uwezo wa kumiliki jukwaa kuna tatizo gani?

Wengine hawataki shule, kuliko kukaa tu nyumbani si bora wakajishughulishe.

kwa hiyo hakuna namna nyingine ya kujishughulisha zaidi ya kujiuza mkuu?watafute shughuli halali
 
Back
Top Bottom