Mabinti wa sasa acheni kukurupukia ndoa

Vaislay

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
4,532
1,822
Habari za muda huu wapendwa katika bwana. Naomba niseme hili kwa uchache tu.

Mabinti wengi wamekuwa moto mno na kujikuta wanangukia pua wakitangaziwa ndoa na hawa watoto wetu wa kiume wenye mikakati yao, bila kuchukua muda wa kumsoma na kumfahamu muoaji, mwisho wa siku wanatutesa wanandugu.

Wifi yangu wa miaka 22 alikutana na kijana akamjaza upepo wa ndoa, walifahamiana kwa muda mchache sanaa, baada ya kuleta taarifa za ndoa aliulizwa sanaaa kama kijana anamfahamu vizuri na kama kweli yuko tayari kungia kwenye ndoa hiyo.

Ndoa iliandaliwa na kufana sana, kwakua ndoa inafungwa upande wa mwanamke kulingana na dini, kuna sintofahamu zilitokea ambazo ziliashiria kabisa kijana muoaji ni changamoto na kuleta hofu huko binti aendako kama utakuwa na usalama. Ni miezi miwili sasa tunajua hata ajira ya kijana aliyomwambia binti sio ya kweli pamoja na vitu kibaaaaoooo.

Michango inauma jamani, mnatesa familia pia, unapokutana na changamoto hata familia inaingia kwenye simanzi, mara zote familia hutakia heri pale jambo la baraka kama ndoa likitokea. Chunguza mtu, mfahamu vizuri, usiolewe kwa kuonyesha mashost au kuwarusha roho, maisha unaenda kuishi wewe, cha moto utakiona wewe sisi washereheshaji tu.

Tunalaumu ndoa ni ngumu kumbe ni nyinyi wenyewe ndio chanzo cha ugumu. Ndoa nyingi ikifika miezi sita tu iko ICU. Maamuzi sahihi hayafanyiki, kukurupuka ni kwingi, kila jambo linakuwa na taa nyekundu lakini mnapuuzia. oooh atabadilika mbeleni, ashindwe kumbadilisha mama yake mzazi wewe ndio utaweza?

Mabinti wa ndoa, mtulize mishono na viherehere.
 
Mpe pole ndugu yako kwa kuingizwa mkenge, vijana nao wameshajua akija ukweni kiunyonge atanyiwa mke.

Hivyo wengine hulazimika kufake maisha ili kuwa-win wakwe Ili wachukue mke mapema.

Umemaliza vizuri sana hapo kwenye kuchunguzana mwenye masikio na asikie.
 
Tatzo wamejisahau sana hawajui nn maana ya ndoa wanafurahia kuvaa shera na kuvishwa pete ili wapate picha za kupost wanasahau kuwa kuna maisha baada ya kuvishwa pete na kuvua shera. Ukimbilia ndoa ili kufurahisha watu na kwakufata mkumbo
 
Ahsante, ni kweli inabidi kufahamiana vizuri kabla ila inabidi umfahamu mtu kwa muda gani? Je akiamua kupretend kipindi hicho chote hadi mkiingia kwa ndoa ndiyo akaonyesha true colors je? Nadhani ipo complicated kiasi mtu akidhamiria kumpata mtu hashindwi kupretend na usigundue🤔
 
Samahani mkuu....
Hivi haya unayo yasema hapa, umesha mwambia huyo wifi yako..??
Na hata ninyi mnamatatizo, hivi kweli mliwezaje kumuoza binti wa miaka 22..??

Kinsingi kijana ama binti wa miaka 22 bado hajakomaa kiakili, na kwa umri huo huyo binti alikua hajatosha kujifanyia maamuzi yeye mwenyewe.

Kwahili mimi ninawalaumu ninyi kwa kukubali kuchukua mahari na kumsaidia muoaji kwenda kumfanyia ndugu yenu ukatili.
 
Habari za muda huu wapendwa katika bwana,
Naomba niseme hili kwa uchache tu.

Mabinti wengi wamekuwa moto mno na kujikuta wanangukia pua wakitangaziwa ndoa na hawa watoto wetu wa kiume wenye mikakati yao, bila kuchukua muda wa kumsoma na kumfahamu muoaji, mwisho wa siku wanatutesa wanandugu.

Wifi yangu wa miaka 22 alikutana na kijana akamjaza upepo wa ndoa, walifahamiana kwa muda mchache sanaa, baada ya kuleta taarifa za ndoa aliulizwa sanaaa kama kijana anamfahamu vizuri na kama kweli yuko tayari kungia kwenye ndoa hiyo.

Ndoa iliandaliwa na kufana sana, kwakua ndoa inafungwa upande wa mwanamke kulingana na dini, kuna sintofahamu zilitokea ambazo ziliashiria kabisa kijana muoaji ni changamoto na kuleta hofu huko binti aendako kama utakuwa na usalama
Ni miezi miwili sasa tunajua hata ajira ya kijana aliyomwambia binti sio ya kweli pamoja na vitu kibaaaaoooo.

Michango inauma jamani, mnatesa familia pia, unapokutana na changamoto hata familia inaingia kwenye simanzi, mara zote familia hutakia heri pale jambo la baraka kama ndoa likitokea,
Chunguza mtu, mfahamu vizuri, usiolewe kwa kuonyesha mashost au kuwarusha roho, maisha unaenda kuishi wewe, cha moto utakiona wewe sisi washereheshaji tu.
Tunalaumu ndoa ni ngumu kumbe ni nyinyi wenyewe ndio chanzo cha ugumu. Ndoa nyingi ikifika miezi sita tu iko ICU
Maamuzi sahihi hayafanyiki, kukurupuka ni kwingi, kila jambo linakuwa na taa nyekundu lakini mnapuuzia....oooh atabadilika mbeleni, ashindwe kumbadilisha mama yake mzazi wewe ndio utaweza?

Mabinti wa ndoa, mtulize mishono na viherehere...
Kweli kabisa,yani ameshindwa kubadilishwa na waliomzaa au kumlea,bado akashndwa kubadlishwa na Mungu ndio akawe mtu baki tu!
 
Samahani mkuu....
Hivi haya unayo yasema hapa, umesha mwambia huyo wifi yako..??
Na hata ninyi mnamatatizo, hivi kweli mliwezaje kumuoza binti wa miaka 22..??
Kinsingi kijana ama binti wa miaka 22 bado hajakimaa kiakili, na kwa umri huo huyo binti alikua hajatosha kujifanyia maamuzi yeye mwenyewe.
Kwahili mimi ninawalaumu ninyi kwa kukubali kuchukua mahari na kumsaidia muoaji kwenda kumfanyia ndugu yenu ukatili.
Kwa upande wetu wanaume 22 nakubali bado akili huwa hazjakomaa,lakin kwa mabnt unazan n kuanzia umr gan wanakomaa kias cha kuanzsha famlia
 
Samahani mkuu....
Hivi haya unayo yasema hapa, umesha mwambia huyo wifi yako..??
Na hata ninyi mnamatatizo, hivi kweli mliwezaje kumuoza binti wa miaka 22..??
Kinsingi kijana ama binti wa miaka 22 bado hajakimaa kiakili, na kwa umri huo huyo binti alikua hajatosha kujifanyia maamuzi yeye mwenyewe.
Kwahili mimi ninawalaumu ninyi kwa kukubali kuchukua mahari na kumsaidia muoaji kwenda kumfanyia ndugu yenu ukatili.
Kijana anakomaa kiakili akiwa na miaka mingapi?
 
Kuna jamaaangu kaoa akiwa na miaka 22 ni mtu wa swala 5 yeye na mkewe.
Mke wake kachaguliwa na wazee wake.
Now wana mtoto mmoja

Wazee wake wana akili sana. Waarabu na wahindi wanafanya sana hii style.

Kama hela ipo mwanao muozeshe mapema. Aanze kuzaa mapema na kujiepusha na magonjwa ya ngono
 
"Ndoa si kucheza kwaito na kukata keki"

Aliandika mwana JF mmoja katika uzi wa mambo ya ndoa.

Wanafikiri ndoa ni kupiga picha za relationship goals na kupost instagram,na kumnyoa mtoto utadhani mwanamuziki wa bongo fleva.
 
Back
Top Bottom