Mabinti wa kilokole tafadhali pendezeni

Mkuu umeongea kaaa mfalme suleiman hapa, yaani hao dada zetu(mimi mweyewe nimeokoka nimemupatia yesu maisha yangu, ni mpendwa) lakini sina hata nia YEYOTE ya kuoa hao dada zetu ambao wanajiita wameopkoka LA KABISA.Yaani hata mvuto hawana, yaani kuvaa acha tu, mume kitu cha kwanza kuangalia katika binti ni sura, mavavi ndio ajue kaa atatupa maneno au la, sasa kwa kuvaa huko umetaja nani atapoteza muda wake na hao dada zetu.THEY MUST CHANGE, barikiwa sana kwa hii uzi, natamani wote hao dada zetu wapitie huu uzi wako mkuu, pewa fanta bill kwangu mkuu
We ni muasherati
 
Si ukawachukue hao hao wanaopendeza aisee msiwapangie watu maisha, kama unaona washamba achana nao kachukue wajanja wenzio ebooo wanawake wote hawa unashindwaje kupata chaguo lako?
 
Wapemdwa hata social media huku hawapiti, wameambiwa ni dhambi. Hivyo ujumbe haujafika
Oooooh kwamba ni mambo ya kishetani???
Mbona mapastor wao wamejaa kwenye magroup ya whatsapp
 
Eti binti kwasababu amempa Yesu maisha (ameokoka) basi ndo haelewekiiiiii,.. Uso alishaacha kupaka hata kapoda tu! Wanja ndo kabisa hagusi eti una mapepo, tehe;

Ukimkuta mdomo umepaukaaaaaa, eti lipshine zinatengenezwa na viungo vya watoto.. Paka basi hata Baby Care.. bado nayo ni shidaa????.

Binti mrembo kasuka nywele twende kilioni mistari mitatu anakaa nazo kichwani mwezi mzima,mara oh rasta zina mapepo haha.. sasa kwani kususka lazimaaa,
unaweza kuzikata nywele zako vizuri kwa muonekano mzuriii na ukapendeza;

Binti mlokole anajitetea eti mwanaume anaangalia tabia, ha ha mwanaume anakutana na sura yako na muonekano wako kwanza, baada ya hapo ndo anaanza kuchunguza tabia yako,..

Sasa wewe na sketi yako ya kijani ya marinda ndefu mpaka kwenye unyayo na blauz nyekundu muundo wa koti kama msaidizi wa alishabab, viatu vya njano tena vimoka vya juu juu kama "Yondo Sista" unategemea umpate nani? Rangi zimekushinda kupangilia utaweza kupangilia maisha yako na mumeo kwenye ndoa?

Eti wakati ukifika tu Bwana atanipa wangu; utasugua goti mpaka litoke unga, ha ha.. Mwili wako tu unakushinda kuupamba, nyumba utaiweza??? Na mume je! Bwana akupe mume wakati wewe mwenyewe umejishindwa!

Mwanaume anaweza akaoa mwanamke mwenye tabia yeyote na akam-set anavyotaka, lakini sura na muonekano wako ni muhimu bibi weeh…

Utaishia kusema oh ameoa mtu ambaye si mpendwa, wewe ulizaliwa mpendwa??!

Usisahau huyo unayemuita Bwana (Yesu) alikuwa very smart.. anavaa vzr, anapendeza. kanzu yake haikua na kiraka hata kimoja.. ilikua safi na ya kuvutia toka juu mpaka chini ndio maana ikagombaniwa baada ya kifo chake. Ikafika mahali ikabidi waipigie kura kwa jinsi ilivyokuwa inavutia.

Sasa wewe mwenzangu na kitenge chako haijulikani ameshona fundi wa nguo au wa kapeti kha!

Jamani hata kama ni mpendwa na sijui umeokoka basi jipende…

WEWE BINTI/MWANAMKE NI MTU WA THAMANI SANA, LAZIMA UJIHESHIMU LAKINI PIA UJITHAMINI NA UJIPENDE.






Very good bro!yani mdada unashindwa hata kutoka nae kwa sie marafiki zake kapaukaaa
 

Similar Discussions

13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom