Tabrett
JF-Expert Member
- Jun 5, 2013
- 522
- 338
Habari za asubuhi wanajamvi,wanafamilia tumejikuta katika njia panda baada ya mdogo wangu wa kike(mtoto wa bamdogo) anaishi na wazazi wangu kua rafiki yake ambae alikua Oman anafanya kazi katika salon ya kuchora hina amekuja kumchukua ili waondoke wote wakajiunge katika kazi hiyo.Wanafamilia wote hakuna anayeafiki hilo suala ila yeye ndio amekomaa na huyo rafiki yake anajaribu kutushawishi kua hakuna tatizo atakua katika mikono salama,sisi tunahofia maana binti ndio ana 20 yrs hana professional yoyote ni form four leaver tu.Wanajamvi najua humu kunawenye uzoefu na Oman katika hili naomba mnisaidie kunifunua macho kweli hili jambo liko salama kwa binti huyu?