Mabinti wa kibongo na Oman

Tabrett

JF-Expert Member
Jun 5, 2013
522
338
Habari za asubuhi wanajamvi,wanafamilia tumejikuta katika njia panda baada ya mdogo wangu wa kike(mtoto wa bamdogo) anaishi na wazazi wangu kua rafiki yake ambae alikua Oman anafanya kazi katika salon ya kuchora hina amekuja kumchukua ili waondoke wote wakajiunge katika kazi hiyo.Wanafamilia wote hakuna anayeafiki hilo suala ila yeye ndio amekomaa na huyo rafiki yake anajaribu kutushawishi kua hakuna tatizo atakua katika mikono salama,sisi tunahofia maana binti ndio ana 20 yrs hana professional yoyote ni form four leaver tu.Wanajamvi najua humu kunawenye uzoefu na Oman katika hili naomba mnisaidie kunifunua macho kweli hili jambo liko salama kwa binti huyu?
 
nawezekana kabisa ikawa ni salama
lakini inawezekana pia kuwa sio salama
akawa anapelekwa kujiuza huko kwa kujua au kutokujua...
 
wanawake wengi wanadhalilishwa sana oman na wengine wakishafika documents zao za kusafiri zinafichwa halafu wanendelea kuwa ma-slaves wa ngono na kazi za ndani!
 
Human trafficking naona kabisa famlia yenu inaenda kuchangia katika orodha ya machangudoa Oman.
 
Sasa kazi ya kupaka hina form four leaver atashindwa kuifanya kweli? au una wasiwasi na kitu kingine?

Mimi nina ndugu yangu yuko huko kaenda kufanya kazi za ndani, nilifika oman mwezi wa kumi kwa masaa machache japo nilimueleza juu ya ujio wangu aligoma kuja kunisalimia baada ya kudadisi nilichoambiwa wanayoyafanya hawa mabinti huko sababu na mimi nilikuwa na matatizo yangu nilimshukuru Mungu kwa kila kitu.
 
Kujiuza ni uamuzi wa mtu .

Sio uamuzi!! ni amazingira sometimes mtu anakuwa subjected to na hana njia! mfano akifika anakuta kila mtu ndo baishara na wanamuonesha pesa, na hawamsaidii!! unataegemea nini afanye uamuzi gani, ama hata akiktaa anakuwa raped!!
 
nawezekana kabisa ikawa ni salama
lakini inawezekana pia kuwa sio salama
akawa anapelekwa kujiuza huko kwa kujua au kutokujua...

tumejaribu kumuelekeza katika hilo rafikiye kang'ang'ana kua hakuna kabisa hiko kitu na kinapigwa marufuku huko wako strict kuliko hata huku bongo
 
wanawake wengi wanadhalilishwa sana oman na wengine wakishafika documents zao za kusafiri zinafichwa halafu wanendelea kuwa ma-slaves wa ngono na kazi za ndani!

mkuu hiko kitu ndio hata sisi kinatutia wasiwasi ila rafiki yake anapinga vikali sana kauli hiyo
 
Wanafamilia mnabidi mtoe msimamo kama wazazi....form 4 leaver...kwanini msiweke mkazo aendelee na masomo.Maana ana safari ndefu,ama hata shule hataki?
 
Sasa kazi ya kupaka hina form four leaver atashindwa kuifanya kweli? au una wasiwasi na kitu kingine?

Mimi nina ndugu yangu yuko huko kaenda kufanya kazi za ndani, nilifika oman mwezi wa kumi kwa masaa machache japo nilimueleza juu ya ujio wangu aligoma kuja kunisalimia baada ya kudadisi nilichoambiwa wanayoyafanya hawa mabinti huko sababu na mimi nilikuwa na matatizo yangu nilimshukuru Mungu kwa kila kitu.

Wasiwasi wetu ni kua je itakua kweli ni hina tu au ndo mwamvuli wa kufanyia ufirauni mwingine!
 
Sio uamuzi!! ni amazingira sometimes mtu anakuwa subjected to na hana njia! mfano akifika anakuta kila mtu ndo baishara na wanamuonesha pesa, na hawamsaidii!! unataegemea nini afanye uamuzi gani, ama hata akiktaa anakuwa raped!!

very true
 
Kwa wema gani wa kumchukua rafiki? Fungueni fahamu zenu! Kama kweli anapenda ndugu yenu apate maendeleo kama yeye (kama yapo), si ni vema aende na ndugu zake wa damu? Wema huu unaweza kuwa wa gharama kubwa huko mbele.
 
Wasiwasi wetu ni kua je itakua kweli ni hina tu au ndo mwamvuli wa kufanyia ufirauni mwingine!

Nyie mna mpango gani na huyo binti kama ataendelea kubaki hapa nyumbani? Heri nusu shari lakini...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom