Mabinti punguzeni ushamba mnapokuwa hotelini

Habari,

sina mengi ya kuongea ila kuna jambo moja huwa naliona kwa baadhi ya mabinti na binafsi naona kama ulimbukeni au ushamba fulani pale unapompeleka lunch sehemu zile kubwa kubwa.

Kuna tabia ya baadhi yao kuagiza vitu asivyoweza kutumia au asivyoweza kumaliza.

Kuna mmoja leo kanikera sana nimemuita maeneo fulani kaanglia menu kisha akaagiza leta hiki leta kile mara kile.

basi mzee mazaga zaga yote kaletewa kwa meza harafu kagusa guza tu kajifanya kushiba kumbuka hapo imeungua 100k kasoro.

Nikasema isiwe noma kaagiza maji na eneo lile maji makubwa ya kilimanjaro yanauzwa 5k kaonja tu kayaacha tukaondoka.

Kwa kweli wale wenye tabia hii iacheni mara moja usawa huu wa mjomba Magu agiza vile unavyoweza kumaliza na sio kuagiza usivyovijua wala kuvimaliza.

Huu ni ushamba na ulimbukeni badilikeni.
huyo sio trisha cute kweli maana ndio aliomba company weekend hii?
 
Back
Top Bottom