Mabingwa wadhibiti ‘kemikali’ za hatari - Utulivu afya ya Dk. Mwakyembe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabingwa wadhibiti ‘kemikali’ za hatari - Utulivu afya ya Dk. Mwakyembe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 24, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Utulivu afya ya Dk. Mwakyembe


  Mwandishi Wetu - RaiaMwema...


  [​IMG]


  Dk. Harrison Mwakyembe


  MADAKTARI bingwa wa Hospitali ya Apollo nchini India, wamefanikiwa kudhibiti ‘kemikali' hatari zilizobainika katika ute ute (bone marrow) ndani ya mifupa ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, zisiendelee kujizalisha na kuzidi kushambulia chembe hai za ngozi na maeneo mengine ya mwili kama ilivyokuwa awali, Raia Mwema, limeelezwa.

  Katika toleo lake namba 227 la Februari 22 hadi 28, mwaka huu, gazeti hili la Raia Mwema liliripoti taarifa za kupandikizwa kwa ‘kemikali' iliyokuwa na uwezo wa kujizalisha ili kushambulia chembe hai za mwili, hususan ngozi katika mwili wa Dk. Harrison Mwakyembe, kemikali ambazo zimezua mjadala mkali kitaifa, wengine wakiamini ni sumu iliyotengezwa kwa kushirikisha fomula maalumu za kikemia na kibaiolojia.

  Ni wakati huo ambao gazeti hili limeripoti habari hiyo, ndipo Dk. Mwakyembe alisafiri kurudi Hospitali ya Apollo, India kwa ajili ya uchunguzi wa maendeleo ya afya yake, baada ya awamu ya kwanza ya matibabu madaktari bingwa kubaini ‘kemikali' (sumu?) hizo na kubuni namna kwanza ya kudhibiti zisiendelee kujizalisha lakini pia kuziangamiza kabisa.


  Madaktari Hospitali ya Apollo, India

  Hatimaye madaktari bingwa wa Hospitali ya Apollo nchini India wamefanikiwa kudhibiti kemikali (kitu/sumu?) zilizokuwamo kwenye bone marrow.

  Dk. Mwakyembe mwenyewe amethibitisha kuimarika kwa afya yake, Jumatatu ya wiki hii, alipofika ofisini kwake jijini Dar es salaam kuanza kazi, ambapo kuwasili kwake ofisini siku hiyo kulivuta hisia za watu mbalimbali wakiwamo waandishi wa habari kutoka vyombo tofauti vya habari waliofika kwa ajili ya mahojiano naye.

  Dk. Mwakyembe amekuwa katika matibabu katika Hospitali ya Apollo nchini India akitibiwa ugonjwa usio wa kawaida tangu Oktoba, mwaka jana ambapo hii ilikuwa safari yake ya pili kwenda nchini humo kwa uchunguzi na matibabu.

  Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Dk. Mwakyembe hakuingia kiundani kuhusu ugonjwa wake akisema suala hilo linachunguzwa na vyombo vya dola, hivyo ni vema vikaachwa vifanye kazi yao bila kuingiliwa.


  Udhibiti wa ‘kemikali' za hatari

  Vyanzo vyetu vya habari vya uhakika vinabainisha kwamba, madaktari bingwa katika Hospitali ya Apollo wamefanikiwa kupunguza kwa kiwango kikubwa ‘kemikali' iliuokibainika kuwamo kwenye bone marrow na hata kukidhibiti kisiendelee kujizalisha kama ilivyokuwa awali.

  Kudhibitiwa kwa kemikali hizo, inaelezwa na watalaamu hao kuwa ni mafanikio makubwa katika mchakato mzima wa matibabu ya Dk. Mwakyembe, na inatarajiwa kwamba afya yake itaimarika zaidi katika kipindi cha miezi ya miezi miwili.

  Kuimarika kwa afya ya Dk. Mwakyembe kunajibainisha vile vile katika mabadiliko ya mwili wake, hususan ngozi iliyokuwa imeathirika kwa kiwango kikubwa.

  Mwili waanza kurejea hali yake

  Tofauti na wakati wa kipindi kigumu cha kuzidiwa kwa ugonjwa, kwa sasa Dk. Mwakyembe amepata mabadiliko makubwa.

  Mabadiliko hayo ni pamoja na ngozi yake kuanza kuwa laini na hata kurudi katika hali ya kawaida. Awali ngozi ya Dk. Mwakyembe ilikuwa kavu.


  Mabadiliko mengine ni kuchipuka kwa kucha mpya zenye sura halisi, kuota kwa vinyweleo, nyusi na nywele, pamoja na kufunguka kwa matundu ya kutolea jasho.

  Awali, kutokana na kemikali husika kushambulia ngozi ya Dk. Mwakyembe, vinyoleo vilishambuliwa na kuondolewa, pamoja na matundu madogo ya ngozi kuziba na hivyo, mwili wake kushindwa kutoa jasho.

  Ni maendeleo makubwa katika afya ya kiongozi huyo ambaye, kemikali ilibainika kuwamo kwenye bone marrow, ilibadili kabisa mfumo wa mwili wake.


  Katika uchunguzi wa madaktari hao wa Apollo wamefanikiwa kwenda mbali zaidi katika kubaini kiini hasa cha ugonjwa unaomsumbua waziri huyo kwa kubainisha tatizo hilo ambapo kiutalaamu, kama lilivyotajwa na Dk Mwakyembe katika mkutano wake na waandishi wa habari kuwa, Popular scleroderma.


  Hata hivyo, wataalamu wanabainisha kuwa bado sio rahisi kwa mtu wa kawaida kuelewa kutokana na ukweli kwamba hilo ni jina la kiujumla.


  Matundu katika mwili wa binadamu ni muhimu katika kuufanya mwili upumue na
  inaelezwa kwamba kitaalamu matundu hayo ndimo vinapochomoza vinyweleo.


  Kwa mtu mzima, inaelezwa kuwa mwili wa mtu mzima una nywele na vinyweleo takriban milioni tano.

   
Loading...