Mabilioni yatengwa kulipa malimbikizo ya mishahara ya Watumishi

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Serikali imeahidi kulipa malimbikizo yote ya mishahara ya Watumishi wa Umma, na kwamba tayari shilingi bilioni 20 zimetengwa kulipa madai ya Watumishi ambao maombi yao yamekwishaidhinishwa.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi Rasilimali Watu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ibrahim Mahumi wakati akizungumza katika Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) jijini Dar es salaam.

Kuhusu kuchelewa kulipwa kwa malimbikizo hayo, amesema kumetokana na Mfumo wa Rasilimali Watu (LAWSON) kulemewa na madai ya Watumishi yaliyoanza kupokelewa kwa wingi kufuatia Serikali kukamilisha zoezi la kuhakiki taarifa za watumishi (kuondoa watumishi hewa na wasiokuwa na elimu stahiki kulingana na ngazi zao).

Pia amesema baadhi ya Watumishi hawajalipwa malimbikizo yao kwa sababu maombi yao hayajapokelewa, lakini ameahidi kuwa wote wenye madai halali watalipwa kwani tayari Serikali imeanza kutumia mfumo mpya wa kushughulikia malimbikizo.

Mahumi ametumia jukwaa hilo kuwakumbusha Watumishi wa umma kuzingatia maadili sehemu za kazi ikiwa ni pamoja na kufahamu nani anatakiwa kutoa taarifa fulani kutokana na kuzuka kwa tabia ambayo kila mmoja anataka kuwa msemaji wa shirika au taasisi.

Ameongeza kuwa mitandao ya kijamii imechangia kumomonyoka kwa maadili kwa sababu wapo Watumishi wasio waaminifu wanaovujisha taarifa za siri za Serikali mitandaoni.
 
malimbikizo ya mshahara ni haki yao ya msingi haipaswa kucheleweshwa hata kidogo! jasho lao halipaswi kukauka.

hakuna dhambi mbaya kama kuchelewa kumlipa mtu ujira wake, walipeni malimbikizo yao na wao wafurahi ili neema ziongezeka.
watendaji ktk wizara ya fedha acheni urasimu shughulikieni haki za watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ujanja ujanja tu,mtu anadai tokea 2014,hajalipwa leo mnakuja na mbwembwe et bil 20 zimetengwa,msiwafanye wafanyakazi mbumbumbu na hawana akili,wanalitumikia taifa kwa jasho jingi,vitisho vingi likija swala la maslahi yao mnakunja mikia,jasho la mtu haliliwi!
 
Serikali imeahidi kulipa malimbikizo yote ya mishahara ya Watumishi wa Umma, na kwamba tayari shilingi bilioni 20 zimetengwa kulipa madai ya Watumishi ambao maombi yao yamekwishaidhinishwa.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi Rasilimali Watu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ibrahim Mahumi wakati akizungumza katika Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) jijini Dar es salaam.

Kuhusu kuchelewa kulipwa kwa malimbikizo hayo, amesema kumetokana na Mfumo wa Rasilimali Watu (LAWSON) kulemewa na madai ya Watumishi yaliyoanza kupokelewa kwa wingi kufuatia Serikali kukamilisha zoezi la kuhakiki taarifa za watumishi (kuondoa watumishi hewa na wasiokuwa na elimu stahiki kulingana na ngazi zao).

Pia amesema baadhi ya Watumishi hawajalipwa malimbikizo yao kwa sababu maombi yao hayajapokelewa, lakini ameahidi kuwa wote wenye madai halali watalipwa kwani tayari Serikali imeanza kutumia mfumo mpya wa kushughulikia malimbikizo.

Mahumi ametumia jukwaa hilo kuwakumbusha Watumishi wa umma kuzingatia maadili sehemu za kazi ikiwa ni pamoja na kufahamu nani anatakiwa kutoa taarifa fulani kutokana na kuzuka kwa tabia ambayo kila mmoja anataka kuwa msemaji wa shirika au taasisi.

Ameongeza kuwa mitandao ya kijamii imechangia kumomonyoka kwa maadili kwa sababu wapo Watumishi wasio waaminifu wanaovujisha taarifa za siri za Serikali mitandaoni.
Upuuzi mtupu.
 
isiishie tu kutenga 20 billion, bali waanze kuwalipa mara moja kuanzia mwezi huu, watendaji acheni urasimu na pia msiwachonganishe na serikali yao kwa kuchelewa kushughulikia na kutatua kwa wakati madai yao.
tubadilike, yuache kufanya kazi kwa mazoea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali imeahidi kulipa malimbikizo yote ya mishahara ya Watumishi wa Umma, na kwamba tayari shilingi bilioni 20 zimetengwa kulipa madai ya Watumishi ambao maombi yao yamekwishaidhinishwa.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi Rasilimali Watu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ibrahim Mahumi wakati akizungumza katika Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) jijini Dar es salaam.

Kuhusu kuchelewa kulipwa kwa malimbikizo hayo, amesema kumetokana na Mfumo wa Rasilimali Watu (LAWSON) kulemewa na madai ya Watumishi yaliyoanza kupokelewa kwa wingi kufuatia Serikali kukamilisha zoezi la kuhakiki taarifa za watumishi (kuondoa watumishi hewa na wasiokuwa na elimu stahiki kulingana na ngazi zao).

Pia amesema baadhi ya Watumishi hawajalipwa malimbikizo yao kwa sababu maombi yao hayajapokelewa, lakini ameahidi kuwa wote wenye madai halali watalipwa kwani tayari Serikali imeanza kutumia mfumo mpya wa kushughulikia malimbikizo.

Mahumi ametumia jukwaa hilo kuwakumbusha Watumishi wa umma kuzingatia maadili sehemu za kazi ikiwa ni pamoja na kufahamu nani anatakiwa kutoa taarifa fulani kutokana na kuzuka kwa tabia ambayo kila mmoja anataka kuwa msemaji wa shirika au taasisi.

Ameongeza kuwa mitandao ya kijamii imechangia kumomonyoka kwa maadili kwa sababu wapo Watumishi wasio waaminifu wanaovujisha taarifa za siri za Serikali mitandaoni.
Angekaa kimya tuuu.sababu kauli kama hizo tumeanza kuzisikia muda mrefu. yaani,alaniwe aliyeleta huu msamiati unaoitwa "MCHAKATO"
 
Kwa nini awe kimya wakati kweli serikali imeamua kuwalipa malimbikizo yao ya mshahara?!! ni suala tu la watendaji kutekeleza kulipa haki za watu
 
Back
Top Bottom