Mabilioni yanusuru wanafunzi kukosa madarasa na madawati mkoani Arusha

kalacha mateo

Senior Member
Sep 27, 2021
118
237
Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha, Hargney Chitukuro amesema kuwa mwaka huu hakuna mwanafunzi aliyekosa kuingia darasani kwa kukosa chumba cha darasa au dawati. Amesema wamefanikiwa kuepukana na adha hiyo kutokana na uamuzi wa serikali kutoa zaidi ya Sh. bilioni mbili kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na samani zake.

"Tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutumia fedha hizi ambazo kwa jiji letu tumejenga madarasa 100. kati yake 20 ni ya ghorofa ambayo yako sekondari ya Elerai vyumba vinne, Terati vyumba vinane na ungalimitedi vyumba vinane." alisema Bw. Hargney Chitukuro

Aidha aliongezea kuwa walipatiwa na serikali fungu lingine sh. milioni 940.9 kutoka mradi wa Boost. Wanazitumia kujenga vyumba kwenye shule za msingi Msasani, Muriet, Sinoni, Terati, Uhuru na Ukombozi.

Pesa nyingine zilipokelewa kutoka Hazina Sh. milioni 980 kujenga shule mbili za msingi Nafco na Korongoni pamoja na ujenzi wa vyumba tisa vya madarasa katika shule ya msingi ya mchepuo wa Kiingereza Arusha (3), Naura (2), Meru (2) na Ungalimitedi (2) ambao ujenzi wake unatarajiwa kukamilika Juni 30,2023.

Fj7iGt0XgAEepZA

 
Back
Top Bottom