Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,195
- 23,033
Baada ya kuvunjika kwa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mnamo mwaka wa 1977, hatima ya watanzania waliokuwa wafanyakazi wa jumuiya hiyo imekuwa tata hadi leo miaka zaidi ya thelathini baadaye.
Mwaka 1984 Serikali ya Tanzania ilikabidhiwa mamilioni ya fedha kwa pound za Uingereza (British Pound Sterling) zilizokuwa ni pensheni za wastaafu hawa baada ya ugawaji wa mali za jumuiya, iliyosimamiwa na mwakilishi wa Benki ya Dunia, Dr. Victor Umbricht, kukamilika. Wakati fedha hizi zikikabidhiwa serikali, Pound moja ya Uingereza ilikuwa na thamani ya Tsh.14.3. Hii pensheni ambayo ilitokana na makato ya mishahara ya wafanyakazi hao awali ilitunzwa kwa maajenti Uingereza waliojulikana kama Crown Agents..
Jumuiya pamoja na kuwa na taratibu zake za malipo ya pensheni, ilielekeza wastaafu wake walipwe kwa kutumia formula maalum na pia kulingana na thamani halisi ya dola (wakati wa malipo) kwa kuwa pound ya Uingereza kwa wakati huo ilikuwa inayumba sana. Dola moja kwa wakati huo ilikuwa Tsh. 8.3.
Pamoja na madai ya wastaafu hao ya muda mrefu, serikali kwa sababu zisizoeleweka haikuwa tayari kulipa hizo fedha. Ghafla mwaka wa mwisho wa utawala wa awamu ya tatu, serikali hiyo hiyo iliafiki kuwa ingelipa. Mwaka uliofuata 2006 (miaka 30 baada ya kuvunjika kwa jumuiya), wastaafu wachache walilipwa bila kutumia formula ya pensheni ya jumuiya kama ilivyotumika kwa nchi za Kenya na Uganda, kiasi ambacho hakikuweza kufika hata asilimia 10% ya madai yao.
Tuwasaidie namna gani ndugu zetu kupata haki zao. Hizi fedha za wastaafu ambazo hazikuwa hata za serikali, zilipotea wapi. Ama ndio mkono wa UFISADI , duh.