VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,800
Rasimu ya Katiba mpya iliyozinduliwa juzi na Makamu wa Rais wa Tanzania,Dr.Mohamed Gharib Bilal imeyazungumzia mabilioni ya vigogo,hasa viongozi wa umma. Ibara ya15, Ibara ndogo ya 2 inakataza kiongozi wa umma kufungua na kendesha akaunti ya benki nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania isipokuwa tu kwa utaratibuutakaoruhusiwa na sheria.
Ibara 15(2) ya Rasimu inasomeka:
(2)Mtumishi wa Umma -
(a)hatafungua au kuendesha akaunti ya benki nje ya Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kwa namna ambayo sheria za nchi zinaruhusu.(Msisitizo ni wangu)
Tume ya Jaji Joseph Sinde Warioba imeyakumbuka mabilioni yaUswisi, ambayo kwa siku za hivi karibuni yalikuwa maarufu na kujaribu kuyazungumzia kikatiba. Taarifa za ndani na nje ya nchi zinaonesha kuwa viongozi mbalimbali wa sasa na wa zamani wa umma wa Tanzania wanamiliki akauntiz enye mabilioni ya pesa katika nchi za Uswisi na kwingineko.
Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Zitto Zuberi Kabwe alishawasilisha Hoja Maalum Bungeni kutaka Serikali isaidie ili mabilioni ya Uswisi yarudi nchini kujenga uchumi wetu.Hatahivyo,hadi sasa Serikali iko kimya na Hoja ya Zitto iko ‘pending'.
Ni juzi juzi tu,Zitto amemuandikia barua Waziri Mkuu wa Uingereza,David Cameron kumuomba msaada wa kufanikisha kurejeshwa kwa mabilioni hayo toka Uswisi.
Waungwana,utekelezaji wa Ibara hii,kama ikipita kama ilivyo,utakuwaje? Jambo hili litawezekana kuwakataza ‘wenye nchi' kuficha ‘visenti'vyao nje ya Tanzania?
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam