Ikiwa katiba itaheshimiwa na kuhakikisha sheria, kanuni na taratibu zinafuatwa ipasavyo na kila mmoja wetu ( yaani sekta binafsi na serikalini). Sote tukalipa kodi stahiki na kuzuia mianya yote ya upigaji, amini nawaambia tutaandamana kwa madai maisha ni magumu sana.
Hata wewe na mimi bila kujali ulipo unaishi ukiogelea katika dimbwi la wizi, rushwa ndio maana unaweza kuishi kwa mshahara mdogo.
Si kweli. Watanzania wengi tunaishi kwa vipato vyetu halali, ndio maana wengi wetu ni maskini. Hao unaowasema wewe ni wafanyakazi wa serikali na mashirika yake, pamoja na wengine wachache ambao wanaishi kwa kujinufaisha na mali za umma kwa njia za ufisadi. Nakwambia tena hao ni wachache sana.