Mabilioni ya shilingi yamwagwa kujenga barabara Kigoma

Sio mjuzi wa hii barabara ila ndio inayounganisha mkoa wa kigoma na jiji LA Mwanza Kwa njia ya Lami kupitia nyakanazi? Sababu navyojua hiyo bara bara ilikuwa na mkandarasi tayari, au ni nyingine?
Mkandarasi aliyekuwapo (Nyanza Contractors aka Magu) yeye anaishia hapo kijiji cha Kabingo, urefu wa kama 60km hivi kutoka Nyakanazi. Ila ameteseka sana na hiyo barabara tangu 2015 bado haijaisha! Hiki kipande wanachopewa Wachina kilikuwa kinasubiri uchaguzi mkuu. Kuisha kitategemea maamuzi ya wananchi wa Kigoma, wakitumia haki yao kikatiba haitaisha mpaka itafika 2025!
 
siwezi kupinga kwa sababu ni moja ya miradi nimepigia kelele maisha yangu yote ya Ubunge na ipo kwenye ilani ya ACT mwaka 2015 na pia African Development Bank niliwasumbua sana kuhusu Mradi huu.
Wala Mradi huu hautakuwa sababu ya watu wa Kigoma kuipa kura CCM kwani sio hisani bali ni Haki yetu
Nilikuwa nadhani utasema kwanini mradi huu uanze kutekelezwa wakati kampeni za uchaguzi zinakaribia na hivyo ni njama za CCM kuchukua jimbo lako la uchaguzi!
 
Hiko kipande cha Manyovu - Kasulu kitapita katika wilaya yetu ya buhigwe!
Ikikamilika kuna fursa nimezitega mitaa ile, hata ikichukua miaka mitano, nimeshaseti mitambo yangu.
Imana ishimwe chane!
 
Mkandarasi aliyekuwapo (Nyanza Contractors aka Magu) yeye anaishia hapo kijiji cha Kabingo, urefu wa kama 60km hivi kutoka Nyakanazi. Ila ameteseka sana na hiyo barabara tangu 2015 bado haijaisha! Hiki kipande wanachopewa Wachina kilikuwa kinasubiri uchaguzi mkuu. Kuisha kitategemea maamuzi ya wananchi wa Kigoma, wakitumia haki yao kikatiba haitaisha mpaka itafika 2025!
Hahaha, kumbe unajua magu ana mkono wake hapo! Nshaskia hii kitu bana!
 
Mkandarasi aliyekuwapo (Nyanza Contractors aka Magu) yeye anaishia hapo kijiji cha Kabingo, urefu wa kama 60km hivi kutoka Nyakanazi. Ila ameteseka sana na hiyo barabara tangu 2015 bado haijaisha! Hiki kipande wanachopewa Wachina kilikuwa kinasubiri uchaguzi mkuu. Kuisha kitategemea maamuzi ya wananchi wa Kigoma, wakitumia haki yao kikatiba haitaisha mpaka itafika 2025!
So cha nyanza wenyewe tayari au bado wanaendelea na ujenzi....pia mbona gharama za ujenzi kubwa sana? Au hiyo barabara INA milima mingi?
 
Vijito na mito ni mingi mno sehemu kubwa ya ukanda ule mikima ni kuanzia Kasulu Rusunwa hills ni balaa, kibigwa, heru juu mpaka Manyovu centre/Mnanila
 
So cha nyanza wenyewe tayari au bado wanaendelea na ujenzi....pia mbona gharama za ujenzi kubwa sana? Au hiyo barabara INA milima mingi?
Kipande cha Nyanza wapo wanamalizia. Nafikri kufika wakati wa kampeni watakuwa wanakabidhi sasa! Inawezekana ni hiyo miinuko mingi na kona nyingi nyingi kwenye hiyo barabara, ingawa miinuko yenyewe siyo milima yenye mawe!
 
ZITO, Ninachochua nikuwa Barabara na madaraj ni maendeleo ya Vitu amabvyo upinzani na baadhi wa wnaccm wanataka maendeleo ya watu. Kwani ni leo unasupport maendelo ya vitu kama Barabara na madaraja au kwa kuwa yanajengwa kwenda Kigoma il yakijengwa pengine inakuwa siyo maendeleo ya watu. Hebu dadavua
Acha Ujinga wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tangu lini barabara ya kigoma Nyakanazi ikapita Manyovu?
Hicho kipande cha Manyo-vu no kutoka Kasulu - Manyovu kupitia Buhigwe (wilaya mpya). Kikifika manyovu kinaungana na ile ya kwenda Kigoma kupitia Mwandiga! In ramani nzuri maana inatoa fursa na kwa watu wa Buhigwe kupata lami. Kumbuka ile ya Kigoma-Kasulu imeshakamilika, kwa hiyo zitaungana hapo Kasulu mjini!
 
View attachment 1365779

SERIKALI ya Tanzania imetiliana saini mkataba na wakandarasi wanne wa kampuni ya ujenzi ya China kwa ajili ya barabara ya kiwango cha lami kutoka Kabingo wilayani Kakonko hadi Manyovu wilayani Buhigwe yenye urefu wa kilometa 260 kwa gharama ya Sh bilioni 584.7.

Waziri wa Ujenzi, Isack Kamwelwe aliongoza viongozi wa Serikali ya Tanzania kushuhudia utiaji saini huo ambao Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (Tanroads), Patrick Mfugale aliongoza utiaji saini huo kwa Serikali ya Tanzania ambao unafanyika kutokana na mkopo wa riba nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) huku Serikali ya Tanzania ikitoa kiasi cha Sh bilioni 58 kuchangia ujenzi huo.

Akizungumza kabla ya utiaji saini, Kamwelwe alisema ujenzi huo wa barabara ni matokeo ya ahadi aliyotoa Dk John Magufuli wakati wa kampeni za urais mwaka 2015. Alisema aliona ukanda wa magharibi una changamoto kubwa. Akitoa taarifa kabla ya utiaji saini huo, Mfugale alisema mradi huo wa ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami umegawanywa kwenye vipande vinne kuwezesha ujenzi wake kufanywa kwa haraka na katika kipindi cha miaka mitatu barabara hiyo inapaswa ianze kutumika.

Aliwataja wakandarasi hao kuwa ni Zhejiang Communication Construction Group Co. Ltd iliyopewa kipande cha Manyovu hadi Kasulu kilometa 68.2 kwa gharama ya Sh bilioni 76.1 na Sinohydro Corporation Ltd iliyopewa kipande cha kuanzia Kasulu Mjini hadi Mvugwe wilayani Kasulu kilometa 70.5 kwa gharama ya Sh bilioni 83.7.

Wengine ni STECOL Corporation iliyopewa kipande cha kuanzia Kijiji cha Mvugwe hadi eneo la njia panda ya Kambi ya Wakimbizi Nduta wilayani Kibondo kilometa 59.3 kwa gharama ya Sh bilioni 84.7 na China Hennan International Cooperation Group (CHICCO) kilometa 62.5 iliyopewa kipande cha kuanzia njia panda ya Kambi ya Wakimbizi ya Nduta hadi Kijiji cha Kabingo kwa gharama ya Sh bilioni 95.5.

Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema atasimamia kwa karibu kuhakikisha fedha za utekelezaji wa mradi huo zinatolewa kwa wakati ili kuwezesha kutekelezwa kwa muda huo uliopangwa.

Dk Mpango alisema ujenzi wa barabara hiyo siyo muhimu kwa uchumi wa Mkoa wa Kigoma na watu wake pekee, bali kwa Taifa kutokana na mkoa kuwa kitovu cha uchumi kwa nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa barabara la Afrika; na kuongeza kuwa lazima Tanroads waoneshe weledi wao katika kusimamia utekelezaji wa mradi huo kwa viwango na wakati huku akionya wakandarasi kutoyumbisha na kuomba kuongezewa muda bila sababu.

Naye Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alisema barabara hiyo ni tukio muhimu kwa mkoa huo kwani kuna watu ambao hawajawahi kuona lami hivyo kwao jambo hilo lilileta manung’uko makubwa na kujiona kama siyo sehemu ya Tanzania.

Akitoa neno kwa niaba ya wananchi wake, Mkuu wa mkoa, Emmanuel Maganga alisema kwao mradi huo ni moja ya miradi iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu kutokana na umuhimu wake kiuchumi kwa wananchi wa mkoa huo kwani ni mkoa wa kimkakati kwa ajili ya soko la Ukanda wa Nchi za Maziwa Makuu. Aliwataka wakandarasi kuzingatia kuajiri vijana kutoka mkoani humo katika kazi ambazo hazihitaji utaalamu.
Zittoooooo

Njoo huku wanajenga barabara ya mkoani kwako mwaka wa uchaguzi ili ushindwe ubunge. Tafadhari nenda wingereza na ujerumani upinge mradi huu kwani ni mbinu mbovu ya kukuondosha katika ubunge. Hii ni rushwa kwa wapiga kura.

Serikali ya miundo mbinu katika ubora wake
 
Huku ndio hela zinatakiwa kwenda sio kwenye ma dreamliner

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom