Mabilioni ya fedha za watanzania zakutwa nchini uswiss | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabilioni ya fedha za watanzania zakutwa nchini uswiss

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Msemakweli, Jun 27, 2012.

 1. Mzee Msemakweli

  Mzee Msemakweli Senior Member

  #1
  Jun 27, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 159
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Watanzania sita wenye account Nchini Uswiss wamekutwa na jumla ya Tzs 300.00 Billion. Fedha ambazo kama zingetumiwa vizuri; zingeweza kutatua matatizo mengi wanayoyalalamikia Madaktari na kupunguza hali ngumu kwa Watanzania. Hainiingii akilini kuona fedha zetu walipa kodi zinachukuliwa na kikundi cha watu wachache sana na tuliowengi tunabakia mikono mitupu. Natamani kuona siku moja tunatangaza vita na hawa wanasiasa. Ikibidi tuanze kuwapiga mawe wapitapo barabarani na hata kwenda majumbani kwao kuchukua mali zao tuzirudishe mikononi mwa Watanzania.
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Jun 27, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Hao ni wezi taslimu, zingekuwa za halali wangewekeza nchini. Wanatakiwa wakanyongwe fedha zirudishwe benki kuu.
   
 3. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #3
  Jun 27, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Wanapoambiwa tunarais dhaifu na serikali legelege wanakataa nn! Bado zile trilion tatu za general Shimbo
   
 4. d

  dada jane JF-Expert Member

  #4
  Jun 27, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nchi hii ni vituko tu. Body ya mikopo ya vyuo vikuu inakata deni lao hata kabla watu hajabadilishiwa mishahara yao. Wakati kuna watu wanajibebea hela za walala hoi. Mishahara ya walimu ni kichefuchefu.
   
 5. Kakulwa P

  Kakulwa P JF-Expert Member

  #5
  Jun 27, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu wanaJF, inasikitisha sana kuona matukio haya yanaendelea nchini bila kukemewa na wale tuliowaweka watusemee kwa niaba yetu.
  Pesa kutoroshewa nje umekuwa ni utamaduni ambao unalindwa na wakubwa wala siyo vinginevyo, watu wenye nia njema wanafichua madhambi ila hakuna utekelezaji wowote unaofuata baadaye.
  1. Nianze na pesa za Andrew Chenge walisema yakaisha maana ulikuwa ni upepo.
  2. Pesa za rushwa ya RADA sijasikia waziri husika anleta hoja bungeni kwa ajili ya kuidhinishwa matumizi yake inawezekana zimeishanunua saruji.
  3. Leo asubuhi nimemsikia waziri Nchimbi anahojiwa Radio One kuhusu wauza madawa ya kulevya na hatua zinazochukuliwa dhidi yao, amesema 'Kama kuna mwananchi anayewajua wahusika awaambie Polisi au aelekeze walipo ili wakamatwa maana hawajulikani' kauli hii tata sana maana Rais wetu alishapewa orodha na Amina Chifupa R.I.P kabla ya mauti yake, lakini pia watu wanakamatwa ushaidi unaonekana ni unga wa muhogo.
  5. Juzi kipindi cha dakika 45 ITV mkurugenzi mkuu TAKUKURU alisema wamewashtaki NYANGUMI watano wa rushwa na wengi ambao ni VIDAGAA lakini akasema hawezi kusema majina yao mpaka mahakama iwatie hatiani, kauli nyingine ambayo ni TATA maana inawezekana wasipeleke ushahidi ili watu wao waachiwe huru.
  Watanzania tukiwa macho na kauli hizi tata na UDHAIFU wa watawala wetu tutachukua hatua stahiki ili kwenye chaguzi tuachane nao na kuwachagua wale wenye dhamira ya kweli.
  Tuungane kuwasema sana hawa watawala huenda wakafunguliwa masikio na macho kuona.
   
 6. K

  Kiti JF-Expert Member

  #6
  Jun 27, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 228
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hayo ni ya Uswisi. Tutajuaje kama kuna waliowekewa fedha nchi nyingine? TAKUKURU itabidi wasiangalie Uswisi pekee. Chunguzeni na nchi nyingine!
   
Loading...