Mshombsy
JF-Expert Member
- Mar 15, 2013
- 372
- 180
Ni muda mrefu sasa watu wanapita huku na kule eti wanafuatilia mapesa uswiss. Kwa watu wasiojua mfumo wa kufuatilia uhalifu au mhalifu nje ya eneo la kimamlaka ya lilipotendeka kosa ataamini.
Mimi si wale wanaoamini mtu mmoja binafsi anaweza kufuatilia makosa yaliyoko chini ya jamhuri. Tukubali tu mtu anayepitapita akisema anafuatilia mabilioni hayo anatafuta umaarufu wa kisiasa pengine angetueleza ni njia zipi anazitumia?
Suala la kuficha pesa nje ni serikali tu inayoweza kulishughulikia na kama serikali haiwezi kwa kukosa nia ya kulishughulikia basi bunge linaweza kuisimamia serikali kuzifatilia.
Nahuzunika ninapoona mbunge mmoja mmoja akisema anazifatilia wakati hata bunge kama taasisi halina mamlaka ya kufanya hivyo. Bunge si muhimili huru kiasi kwamba maamuzi yake yanaweza kutekelezwa na serikali. Ni mapendekezo tu.
Katiba ya sasa imelinyima bunge meno kwa rais kulivunja likikataa bajeti ya serikali, likikataa muswada ambao rais anaona unafaa, na anaweza kulivunja hata likiua turufu ya rais.
Kwa maelezo hayo sioni mbunge mmoja akifuatilia mabilioni na ukizingatia bank katika nchi walikoweka hizo pesa zinafuata sheria za nchi husika. Kwa utaratibu tu ni serikali yetu tu inayoweza kuiomba serikali ya kule kuipa taarifa za watu walioficha pesa huko ili kuona kama walifuata sheria za nchi.
Marekani mwaka huu wamesaini mkataba na uswiss na hata wiki jana wamesaini na cayman islands na costa rica mkataba kupeana taarifa ikiwa mmarekani ataweka pesa nchi hizo kiasi kinachozidi dola elfu 50.
Hii yote ni kutokana na sheria iliyopitishwa mwaka 2010 na US congress inayoitwa Foreign Account Tax Compliance Act (FATCA). Mkataba huo utaisaidia hizo nchi kuzilazimisha bank kutimiza wajibu wake wa sheria za kimataifa kuzuia fedha haramu. Suala hili liko chini ya wizara zao za fedha na sheria.
Mimi nilitegemea mbunge yeyote anayejitapa kufuatilia hela akishawishi wabunge wenzake kupitishwa sheria zitakazoilazimisha serikali kuingia mikataba na nchi nyingine na vilevile kumshawishi rais asaini hizo sheria na kuhakikisha wote walioficha hizo fedha hasa viongozi wa umma wanachukuliwa hatua.
Uswiss kuna bilioni 330 hivi lakini juzi wahisani wameitaka serikali kuzirudisha dola mil 600 ( bilioni 700 za kibongo) zilizochukuliwa na watumishi wa serikali sasa sijui hizi mbona hashikiwi bango tena ziko kwenye eneo letu la kimamlaka.
UPOTOSHAJI:
Mtu mmoja anapopita kila sehemu akisema anafuatilia pesa anawaaminisha watu kwamba silaha zote zipo za kufuatilia hizo pesa na uhalifu mwingine wa kimataifa kumbe hakuna.
Hii inaleta mgongano na watu tunaotaka mageuzi ya utawala wa nchi, tunaotaka mihimili mitatu huru.
Bunge kama taasisi haina silaha za kuhakikisha mabilioni yanarudi na hii ingeingia akilini watuhumiwa wengine ni wabunge.
Sasa mbunge mmoja akisema anazifuatilia anatutoa kwenye mstari wanamageuzi. Tunataka umma uelewe kwamba bunge na wabunge hawana mamlaka yoyote juu ya hilo wanatoa tu mapendekezo. Tunataka umma uelewe hivyo na uwe tayari kwa mageuzi.
Yeyote anayesema anazifuatilia aje JF atoe njia anazotumia ukiachilia mbali serikali yenye mamlaka hayo