Mabilionea hawa watano wameisaidiaje Tanzania, pili unapata picha gani fikiri kwa makini

PISTO LERO

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2011
Messages
2,821
Points
1,195
PISTO LERO

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2011
2,821 1,195
WAFANYABIASHARA watano, Said Bakhressa Gulam Dewji, Rostam Aziz, Reginald Mengi na Ali Mufuruki, wametajwa na Jarida la Ventures Africa linalozungumzia masuala mbalimbali ya uchumi wa Afrika kuwa ndiyo matajiri zaidi nchini.

Anayeongoza katika orodha hiyo ni Bakhressa anayemiliki mali na fedha zenye thamani ya Dola za Marekani 620 milioni sawa na Sh992 bilioni (Dola moja Sh1,600) akifuatiwa na Dewji ambaye utajiri wake ni Dola 560 milioni (Sh896 bilioni).

Wengine na kiasi cha mali na fedha wanazomiliki kwenye mabano ni Rostam (Sh672 bilioni- Dola 420 milioni) Mengi (Sh448bilioni- Dola 280 milioni) na Mufuruki (Sh176 bilioni - Dola 110 milioni).Matajiri hao wamepatikana baada ya kuangalia nafasi zao kifedha, ufanisi wa kampuni zao katika soko la hisa, mfumo wa wanahisa katika soko la hisa na mtiririko mzima wa fedha katika akaunti zao kwenye benki mbalimbali.

Jarida hilo linalotoka mara moja kwa mwezi kutoka Afrika Magharibi, limesema matajiri hao wa Tanzania ni kati ya Waafrika wenye utajiri ambao ni mabilionea 4,800 kutoka mataifa 17.

Asilimia kubwa ya watu 1,523 ni mamilionea na wamo katika ripoti ya watu matajiri Afrika.
Jarida hilo linataja jinsi matajiri hao walivyokuwa wajasiriamali wadogo kabla ya kuibuka na kuwa mabilionea.

Said Salim Bakhresa
Jarida hilo limesema chanzo cha utajiri wa Bakhressa ni mapato yanayotokanana uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kwenye viwanda vyake.Mfanyabiashara huyo aliacha shule akiwa na umri wa miaka 14 na kuanzisha biashara zake. Alianza kuuza urojo Zanzibar na baadaye alifungua mgahawa miaka ya 1970.

Mgahawa huo ulipanuka na alitumia faida yake kufungua mashine ya kusaga pamoja kiwanda za usindikaji vyakula, huku akiunda Kundi la Makampuni ya Bakhressa.

Aliendelea kusindika vyakula mbalimbali na kutengeneza unga wa mahindi na baadaye kuanzisha kiwanda cha kuoka mikate na baadaye kutengeneza chocolate, ice cream, vinywaji na makasha ya kufungashia bidhaa.

Kutokana na shughuli hizo, kwa mwaka huingiza Sh800 milioni.

Kampuni zake kwa sasa zinafanya biashara mbalimbail katika nchi za Tanzania, Uganda, Malawi, Rwanda na Msumbiji na ameajiri zaidi ya wafanyakazi 2,000.

Gulam Dewji
Mfanyabiashara huyo ana utajiri unaokadiriwa kufikia Dola 560 milioni kutokana na kuzalisha bidhaa na kutoa huduma mbalimbali.

Ni mmoja wa mataikuni wa Tanzania tangu miaka ya 1970 na kazi yake kubwa ilikuwa kuingiza bidhaa mbalimbali kutoka nje.Alianza na kampuni ndogo aliyoiita Mohammed Enterprises Tanzania, ambayo kwa sasa ni kati ya kampuni kubwa Afrika Mashariki na Kati.

Miongoni mwa mali zake ni Kiwanda cha 21st Century Textiles, moja ya viwanda vikubwa vya nguo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Kampuni yake ina viwanda vinne, Tanzania na Msumbiji huku ikizalisha Dola 100 milioni kwa mwaka. Pia kampuni hiyo husindika juisi kwa matunda ya Tanzania, mafuta ya kula, sabuni na tishu.Kampuni hiyo pia inamiliki kampuni ya bima, makontena, kampuni za kuuza mafuta ya petroli na maduka ya kuuza bidhaa mbalimbali zaidi ya 100 Tanzania nzima.

Hata hivyo, Gulam alisema jana kwamba takwimu zilizotolewa zimekosewa. Alisema kwa sasa yuko nje ya Dar es Salaam na atatoa taarifa sahihi atakaporejea.

“Kuna baadhi ya tarakimu zimekosewa niko Morogoro kuangalia biashara zangu nikirudi Dar es Salaam nitazungumza,” alisema Dewji.

Rostam Aziz
Ameelezwa kuwa utajiri wake umetokana na kuendesha shughuli zake mbalimbali ikiwamo kampuni za mawasiliano ya simu, madini na biashara za usafiri wa meli.

Mwanasiasa huyo mwenye asili ya Asia, alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Mbunge wa Igunga mwaka 1993 na alishinda kwa vipindi viwili.Aliachana na ulingo wa siasa mwaka 2011. Anamiliki asilimia 19 ya Hisa za Kampuni ya Vodacom ambayo ina wateja zaidi ya milioni nane.

Ameelezwa pia kuwa anamiliki Kampuni ya Ujenzi ya Caspian na sehemu ya Bandari ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Kampuni ya Hutchison Whampoa ya Hong Kong.

Akizungumzia utafiti huo, alisema: “Umefanyika kwa umakini isipokuwa tu kwa upande wangu wanasemas ninamiliki asilimia 19 ya Kampuni ya Vodacom kitu ambacho si sawa kwani ninamiliki asilimia 35.”

Reginald Mengi
Mengi anakimiliki kampuni mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari, viwanda vinavyozalisha vinywaji baridi vya Coca-Cola na ana mgodi wa dhahabu.Mfanyabiashara huyo baada ya kufanya kazi ya uhasibu ambayo ndiyo taaluma yake, alifanya biashara ya kutengeneza kalamu za wino zilizopata soko kubwa Afrika Mashariki.

Leo hii, IPP Group ambayo Mengi ni mwenyekiti wake, inamiliki magazeti mbalimbali ikiwemo Financial Times, ThisDay na The Guardian, televisheni mbili kubwa Afrika Mashariki na Kati EATV na ITV na vituo vya redio. Anamiliki Kampuni za IPP Gold na Handeni Gold.

Ali Mufuruki
Utajiri wake unatokana na biashara mbalimbali za rejareja na za ushirika.

Ni mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji wa Tanzania Infotech Investment Group.

Kampuni hiyo inajumuisha Watanzania na Waganda kwa ajili ya kuuza bidhaa za Afrika Kusini za Woolworth.Infotech hufanya kazi ya uendelezaji makazi na ukodishaji, matangazo na shughuli za mawasiliano
 
A

August

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2007
Messages
4,801
Points
2,000
A

August

JF-Expert Member
Joined Jun 18, 2007
4,801 2,000
hawa mabilleonea wa tanzania ni mawakala wa viongozi, kuna yule msaga unga nk , kuna watu wamemuwezesha kupata mali za nmc, na wao wamo humo humo kuanzia wa awamu ya pili na awamu ya tatu, huyo kawaingiza mpaka viongozi wa nchi alikowekeza, na alikuwa anataka vp wa nchi jirani am-connect kwa kabila drc ili awekeze huko, mwingine ndiyo huyo msekwa alikuwa ananililia kuwa mwenye kiti wa bodi ya kampuni yake, wakati yeye ni supika wakati huo, na kupewa kwenye madini akiwashikia baadhi ya jamaa zetu, nao wana mpa nafuu ya kodi-tax exemption na tax holiday
 
Asante

Asante

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2009
Messages
2,050
Points
1,500
Asante

Asante

JF-Expert Member
Joined Dec 18, 2009
2,050 1,500
Tumejegewa viwanja vya michezo ..............
 
Mtanzania1

Mtanzania1

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2010
Messages
1,169
Points
1,170
Mtanzania1

Mtanzania1

JF-Expert Member
Joined Dec 30, 2010
1,169 1,170
Vitabu vya TRA vinasemaje????
 
MNYISANZU

MNYISANZU

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2011
Messages
7,053
Points
1,225
MNYISANZU

MNYISANZU

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2011
7,053 1,225
Wawasaidie ndugu zao Waislam kujenga shule na vyuo. Wanatia aibu nchini.
 
M

MKALIKENYA

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
1,197
Points
1,170
M

MKALIKENYA

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2012
1,197 1,170
simaanishi kujaza tumbo. Tao sababu za kimaendeleo
Bila kujaza hilo tumbo ungeweza kupata maendeleo emu tumia vizuri ubongo uliopewa bure hivi ukumbuki tumetoka kwenye kipindi ambacho unga wa ugali ulikuwa unaadimika nchi nzima, wanalipa kodi unajengewa barabara,wameajiri watu wengi sana.
 
sixgates

sixgates

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2011
Messages
3,974
Points
1,250
sixgates

sixgates

JF-Expert Member
Joined Mar 19, 2011
3,974 1,250
Wawasaidie ndugu zao Waislam kujenga shule na vyuo. Wanatia aibu nchini.
Dah jamaa yangu usiwe hivyo u will never become a great thinker m teling u..u know I can figure out your thinking framework...unajua nlivyokua nawasoma hawa mabilionea sikuwatizama katika hizo hesabu zako za kidini, ndo umenisababisha niiangalie upya iyo orodha!
 
kbm

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Messages
5,149
Points
1,500
kbm

kbm

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2012
5,149 1,500
... Je kuna mtu anakumbuka ule mradi wa SKUVI? Anaomba atujuze.
 
Pancras Suday

Pancras Suday

Verified Member
Joined
Jun 24, 2011
Messages
7,731
Points
2,000
Pancras Suday

Pancras Suday

Verified Member
Joined Jun 24, 2011
7,731 2,000
Hawa hawapaswi kuulizwa wameisaidia nini Tanzania, wanaopaswa kuulizwa hivi ni serikali ya ccm ambayo inakusanya ushuru kutoka kwa hawa watu kupitia kampuni zao, ila kama hawatoi ushuru na kutoa ajira kwa watanzania wanapaswa kuulizwa wanaisaidiaje Tanzania
 
BONGOLALA

BONGOLALA

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2009
Messages
15,739
Points
2,000
BONGOLALA

BONGOLALA

JF-Expert Member
Joined Sep 14, 2009
15,739 2,000
mengi hana kitu, biashara zake ujanja ujanja!hakuna faida ktk media!Somaiya kamzungukuka mikocheni kwa viwanda
 
Sangarara

Sangarara

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Messages
13,115
Points
2,000
Sangarara

Sangarara

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2011
13,115 2,000
Hawa venture wametumia vigezo gani kuwaidentify hawa watu? na wamepata vipi access ya information zao? Rostam Azizi ni mmoja ya binaadamu wanaofanya biashara zao kwa usiri usio na mfano, venture wamewazaje kutrack wealth yake? kwa mfano watanzania wote tunajua rostamu ndio mmliki wa KAGODA wameinclude investment hii kwenye majumuisho yao?
 
C.T.U

C.T.U

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2011
Messages
4,783
Points
2,000
C.T.U

C.T.U

JF-Expert Member
Joined Jun 1, 2011
4,783 2,000
mengi hana kitu, biashara zake ujanja ujanja!hakuna faida ktk media!Somaiya kamzungukuka mikocheni kwa viwanda
unajua elimu ya media na jinsi media kama radio, tv na magazeti zinavyopata faida?
Au unakurupuka tu ubongo wako umelala kama jina lako linavyosema? Fanya vizuri homework yako
 
C.T.U

C.T.U

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2011
Messages
4,783
Points
2,000
C.T.U

C.T.U

JF-Expert Member
Joined Jun 1, 2011
4,783 2,000
WAFANYABIASHARA watano, Said Bakhressa Gulam Dewji, Rostam Aziz, Reginald Mengi na Ali Mufuruki, wametajwa na Jarida la Ventures Africa linalozungumzia masuala mbalimbali ya uchumi wa Afrika kuwa ndiyo matajiri zaidi nchini.

Anayeongoza katika orodha hiyo ni Bakhressa anayemiliki mali na fedha zenye thamani ya Dola za Marekani 620 milioni sawa na Sh992 bilioni (Dola moja Sh1,600) akifuatiwa na Dewji ambaye utajiri wake ni Dola 560 milioni (Sh896 bilioni).

Wengine na kiasi cha mali na fedha wanazomiliki kwenye mabano ni Rostam (Sh672 bilioni- Dola 420 milioni) Mengi (Sh448bilioni- Dola 280 milioni) na Mufuruki (Sh176 bilioni - Dola 110 milioni).Matajiri hao wamepatikana baada ya kuangalia nafasi zao kifedha, ufanisi wa kampuni zao katika soko la hisa, mfumo wa wanahisa katika soko la hisa na mtiririko mzima wa fedha katika akaunti zao kwenye benki mbalimbali.

Jarida hilo linalotoka mara moja kwa mwezi kutoka Afrika Magharibi, limesema matajiri hao wa Tanzania ni kati ya Waafrika wenye utajiri ambao ni mabilionea 4,800 kutoka mataifa 17.

Asilimia kubwa ya watu 1,523 ni mamilionea na wamo katika ripoti ya watu matajiri Afrika.
Jarida hilo linataja jinsi matajiri hao walivyokuwa wajasiriamali wadogo kabla ya kuibuka na kuwa mabilionea.

Said Salim Bakhresa
Jarida hilo limesema chanzo cha utajiri wa Bakhressa ni mapato yanayotokanana uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kwenye viwanda vyake.Mfanyabiashara huyo aliacha shule akiwa na umri wa miaka 14 na kuanzisha biashara zake. Alianza kuuza urojo Zanzibar na baadaye alifungua mgahawa miaka ya 1970.

Mgahawa huo ulipanuka na alitumia faida yake kufungua mashine ya kusaga pamoja kiwanda za usindikaji vyakula, huku akiunda Kundi la Makampuni ya Bakhressa.

Aliendelea kusindika vyakula mbalimbali na kutengeneza unga wa mahindi na baadaye kuanzisha kiwanda cha kuoka mikate na baadaye kutengeneza chocolate, ice cream, vinywaji na makasha ya kufungashia bidhaa.

Kutokana na shughuli hizo, kwa mwaka huingiza Sh800 milioni.

Kampuni zake kwa sasa zinafanya biashara mbalimbail katika nchi za Tanzania, Uganda, Malawi, Rwanda na Msumbiji na ameajiri zaidi ya wafanyakazi 2,000.

Gulam Dewji
Mfanyabiashara huyo ana utajiri unaokadiriwa kufikia Dola 560 milioni kutokana na kuzalisha bidhaa na kutoa huduma mbalimbali.

Ni mmoja wa mataikuni wa Tanzania tangu miaka ya 1970 na kazi yake kubwa ilikuwa kuingiza bidhaa mbalimbali kutoka nje.Alianza na kampuni ndogo aliyoiita Mohammed Enterprises Tanzania, ambayo kwa sasa ni kati ya kampuni kubwa Afrika Mashariki na Kati.

Miongoni mwa mali zake ni Kiwanda cha 21st Century Textiles, moja ya viwanda vikubwa vya nguo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Kampuni yake ina viwanda vinne, Tanzania na Msumbiji huku ikizalisha Dola 100 milioni kwa mwaka. Pia kampuni hiyo husindika juisi kwa matunda ya Tanzania, mafuta ya kula, sabuni na tishu.Kampuni hiyo pia inamiliki kampuni ya bima, makontena, kampuni za kuuza mafuta ya petroli na maduka ya kuuza bidhaa mbalimbali zaidi ya 100 Tanzania nzima.

Hata hivyo, Gulam alisema jana kwamba takwimu zilizotolewa zimekosewa. Alisema kwa sasa yuko nje ya Dar es Salaam na atatoa taarifa sahihi atakaporejea.

“Kuna baadhi ya tarakimu zimekosewa niko Morogoro kuangalia biashara zangu nikirudi Dar es Salaam nitazungumza,” alisema Dewji.

Rostam Aziz
Ameelezwa kuwa utajiri wake umetokana na kuendesha shughuli zake mbalimbali ikiwamo kampuni za mawasiliano ya simu, madini na biashara za usafiri wa meli.

Mwanasiasa huyo mwenye asili ya Asia, alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Mbunge wa Igunga mwaka 1993 na alishinda kwa vipindi viwili.Aliachana na ulingo wa siasa mwaka 2011. Anamiliki asilimia 19 ya Hisa za Kampuni ya Vodacom ambayo ina wateja zaidi ya milioni nane.

Ameelezwa pia kuwa anamiliki Kampuni ya Ujenzi ya Caspian na sehemu ya Bandari ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Kampuni ya Hutchison Whampoa ya Hong Kong.

Akizungumzia utafiti huo, alisema: “Umefanyika kwa umakini isipokuwa tu kwa upande wangu wanasemas ninamiliki asilimia 19 ya Kampuni ya Vodacom kitu ambacho si sawa kwani ninamiliki asilimia 35.”

Reginald Mengi
Mengi anakimiliki kampuni mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari, viwanda vinavyozalisha vinywaji baridi vya Coca-Cola na ana mgodi wa dhahabu.Mfanyabiashara huyo baada ya kufanya kazi ya uhasibu ambayo ndiyo taaluma yake, alifanya biashara ya kutengeneza kalamu za wino zilizopata soko kubwa Afrika Mashariki.

Leo hii, IPP Group ambayo Mengi ni mwenyekiti wake, inamiliki magazeti mbalimbali ikiwemo Financial Times, ThisDay na The Guardian, televisheni mbili kubwa Afrika Mashariki na Kati EATV na ITV na vituo vya redio. Anamiliki Kampuni za IPP Gold na Handeni Gold.

Ali Mufuruki
Utajiri wake unatokana na biashara mbalimbali za rejareja na za ushirika.

Ni mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji wa Tanzania Infotech Investment Group.

Kampuni hiyo inajumuisha Watanzania na Waganda kwa ajili ya kuuza bidhaa za Afrika Kusini za Woolworth.Infotech hufanya kazi ya uendelezaji makazi na ukodishaji, matangazo na shughuli za mawasiliano
Wewe umeisaidaje tanzania so far
 
mgt software

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
11,351
Points
2,000
mgt software

mgt software

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2010
11,351 2,000
wamesaidia tanzania kujulikana kwa viwanda uchwara
 
Forum statistics

Threads 1,283,904
Members 493,869
Posts 30,805,639
Top