Mabeste alikuwa hafahamu kuwa ana mwanamke ambaye alikuwa amemzidi karibia kila kitu

Ukisikiliza zile clip zao utagundua kabisa Mabeste ni muongo wa kutupwa. Sababu alizozisema za yeye kuachwa na mke wake hazina mashiko kabisa, yani ni sababu za kitoto na inaonekana ni mtu ambaye hakuwa tayari kuingia kwenye majukumu ya ndoa.

Hebu imagine mwanaume analalamika eti mama watoto amewapeleka shule bila ya kuniuliza mimi tuwapeleke shule gani? Hivi kati ya mwanaume na mwanamke ni nani wa kuanzisha hii discussion? Halafu watoto kupelekwa shule ya gharama sio tatizo as long as wamelipiwa, kwa nini kama kweli una nia ya kuwalea wanao usichangie chochote?

Katika kitendo ambacho ni cha fedheha ni kile ambapo mke wake alimkopea mahari kwa rafiki yake kwa kuweka bond gari. Akaenda kulipa then wakairudishiwa ili wakakomboe. Hapa mama mkwe na mwanae walifanya hivi ili kuokoa jahazi maana mchizi alishaishiwa mbinu kabisa. Cha kusikitisha mpaka leo mchizi hajapeleka hiyo mahari na anajitetea kwa mama mkwe eti mwanae alimforce kumuoa yeye hakuwa tayari.

Yani Mabeste inabidi aje na utetezi mwingine, lkn kwa huo uharo alioongea hakuna wa kumuamini.

Unforgetable
 
Mapenzi ya miaka hii pasua kichwa hata wangeishi katika uchumba miaka 10 ndoa ingevunjika tu
 
Mabeste apige moyo konde tu asijaribu kumbembeleza affocuss kwenye mambo mengine japo mwanzo itaonekana ni ngumu sana ila hakika akikomaa atafanikiwa kuyaweka nyuma haya yaliyotokea na atajikuta mahali pazuri... god pulls us back to shoot us forward asisahau hilo
 
  • Thanks
Reactions: J C
Wanawake huwa wakitoaga hela zao kwaajili ya matumizi ya ndani huwa inawauma sana wao wanataka hela zao zibaki kuwa Za kwao na ikitokea umekwama atakukopesha na hiyo hela utailipa tu sasa ikitokea usimlipe e bwanae utasemangwa humo ndani mpaka utajuta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mambo meeeeeeeengi muda mchache...
Pombe naye kashafunga laini yangu,nimeamua kwenda nida nimekuta watu kama efu salasini hivi...
 
noiselessly hunter,
ni sawa mkuu tatizo inaboa inachosha unatunza mwenyewe af lenzio limeriraksi na basically ni jukumu lake apana kwakweli acha aachike tu
 
There are three sides to a story...His side,Her side and the Truth.
Pamoja na yote yaliyoongelewa ukweli wanao wao sie wengine tutabaki kua wapenzi watazamaji na wasikilizaji.
 
By Sangu J

Waswahili wanasema ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Filauni, nimebahatika kusikiliza mahojiano ya Mabeste na aliyekuwa Mke wake Lissa, ukiwasikiliza kuna baadhi ya vitu unagundua kulikuwa na vitu ambavyo nadhani hakuna hata mmoja ambaye alivigundua kwa mwenzake, ila tatizo ni KUTOKUJUANA.

Ukimsikiliza Mabeste anavyoeleza kuhusu kuachwa na Mkewe ni tatizo ni kutovumiliwa kwa tatizo lake kubwa la kiuchumi, ukimsikiliza Lisa anadai kuwa Mabeste alikuwa hafanyi majukumu yake kama Mwanaume ndani ya nyumba.

Mimi nadhani Mabeste alikuwa hafahamu kuwa anadate na mwanamke ambaye alikuwa amemzidi karibia kila kitu kuanzia, Ubunifu, Uwezo wa kujieleza uvumilivu wa Ndoa na kusimamia familia, na Mabeste kitu ambacho alimzidi Mke wake ni upole Upole.

Ukimsikiliza Mabeste hakuna sehemu hata moja anayoeleza namna alivyoipigania familia yake, huku akikiri kuwa alikuwa na hali mbali mbaya kiuchumi, japo mkewe yeye anaeleza alijaribu kueleza kila njia alivyopambana kuhakikisha familia hailali njaa, ndiyo maana alikubali kumpa muda Mabeste akae mbali na familia ili apate muda kutafuta lakini Mabeste hakufanikiwa, ila Lisa anasahau jambo moja suala la kulea familia ni la Mwanaume na mwanamke na si mtu 1.

Mabeste ameeleza jambo la kusalitiwa na Mke wake ila Lisa hakusema wapi ambapo Mabeste alimsaliti, labda nahisi kwa sababu Mabeste hakuwa vizuri kipesa ndiyo maana alishindwa kumsaliti mpenzi wake, lakini Mabeste anasahau angekuwa mpambanaji kama mkewe pengine hata usaliti usingekuwepo.

Ukimsikiliza mke alikuwa mbunifu sana kuhakikisha anafanya kazi kulea familia, ndiyo maana, alidai aliitunza familia karibia miezi 6 lakini Mabeste hakufanya chochote, haikuwa sawa lakini kusaidiana kwenye familia ni jambo la kawaida sana.

Mwisho hatuwezi kumlaumu Mabeste au Lisa kwa kilichotokea maana mambo ya Ndoa wanaojua ni waliokuwa ndani ya Ndoa,lakini kwa sisi wapenzi watazamaji unagundua kulikuwa na makosa ya pande zote mbili, Mabeste hakumjua mke alikuwa anahitaji nini kwa ajili ya familia, na Mke ia hakujua Mabeste alikuwa anahitaji nini kwenye familia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani hawa Mabeste na Lissa ni akina nani?
 
Huyu mwanamke alivumilia akijua jamaa iko siku atatusua kwenye mziki sasa game imekuwa tait anakuja kutoa siri za ndani.
 
Huyo mwanamke ni mpumbavu,kulingana na maelezo aliyetoa mleta hoja,yaani alikua anahesabu kwa miezi mingapi katunza familia?
Familia inatakiwa itunzwe na baba au mama Sasa Kama alitunza yet Kuna tabu gani?
Wanawake wengine vichwani kumejaa nyuki tu .

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli boss mbona wengine tunatunza miaka na miaka hatilalamiki?. Au kwakuwa ni jukumu la mwanaume?. Wanaume tuwe makini na wake zetu ni hatari kwa mwanamke kukuzidi kipato.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukisikiliza zile clip zao utagundua kabisa Mabeste ni muongo wa kutupwa. Sababu alizozisema za yeye kuachwa na mke wake hazina mashiko kabisa, yani ni sababu za kitoto na inaonekana ni mtu ambaye hakuwa tayari kuingia kwenye majukumu ya ndoa.

Hebu imagine mwanaume analalamika eti mama watoto amewapeleka shule bila ya kuniuliza mimi tuwapeleke shule gani? Hivi kati ya mwanaume na mwanamke ni nani wa kuanzisha hii discussion? Halafu watoto kupelekwa shule ya gharama sio tatizo as long as wamelipiwa, kwa nini kama kweli una nia ya kuwalea wanao usichangie chochote?

Katika kitendo ambacho ni cha fedheha ni kile ambapo mke wake alimkopea mahari kwa rafiki yake kwa kuweka bond gari. Akaenda kulipa then wakairudishiwa ili wakakomboe. Hapa mama mkwe na mwanae walifanya hivi ili kuokoa jahazi maana mchizi alishaishiwa mbinu kabisa. Cha kusikitisha mpaka leo mchizi hajapeleka hiyo mahari na anajitetea kwa mama mkwe eti mwanae alimforce kumuoa yeye hakuwa tayari.

Yani Mabeste inabidi aje na utetezi mwingine, lkn kwa huo uharo alioongea hakuna wa kumuamini.

Unforgetable
Wewe ni mwanaume au mwanamke?. Kama mwanamume bado hayajakukuta. Hivi mkeo anaweza peleka watoto shule ya gharama zaidi ya kipato chako pasipo kuwa na uhakika wa chanzo cha mapato kutoka kwa mwenza wako?. Kama anahongwa?. Kikubwa hapa ni wanaume kuwa makini na wanawake tunaoingia nao katika ndoa anapaswa kuwa yule unayemzidi ufahamu na msomamo la sivyo utatupwa kwa dust bin soon ubakie unalia lia kama huyu jamaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom