Mabeste alikuwa hafahamu kuwa ana mwanamke ambaye alikuwa amemzidi karibia kila kitu

sangujoseph

Senior Member
Nov 30, 2015
164
183
By Sangu J

Waswahili wanasema ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni. Nimebahatika kusikiliza mahojiano ya Mabeste na aliyekuwa mke wake, Lissa. Ukiwasikiliza kuna baadhi ya vitu unagundua kulikuwa na vitu ambavyo nadhani hakuna hata mmoja ambaye alivigundua kwa mwenzake, ila tatizo ni KUTOKUJUANA.

Ukimsikiliza Mabeste anavyoeleza kuhusu kuachwa na Mkewe ni tatizo ni kutovumiliwa kwa tatizo lake kubwa la kiuchumi, ukimsikiliza Lisa anadai kuwa Mabeste alikuwa hafanyi majukumu yake kama Mwanaume ndani ya nyumba.

Mimi nadhani Mabeste alikuwa hafahamu kuwa anadate na mwanamke ambaye alikuwa amemzidi karibia kila kitu kuanzia, Ubunifu, Uwezo wa kujieleza uvumilivu wa Ndoa na kusimamia familia, na Mabeste kitu ambacho alimzidi Mke wake ni upole Upole.

Ukimsikiliza Mabeste hakuna sehemu hata moja anayoeleza namna alivyoipigania familia yake, huku akikiri kuwa alikuwa na hali mbali mbaya kiuchumi, japo mkewe yeye anaeleza alijaribu kueleza kila njia alivyopambana kuhakikisha familia hailali njaa, ndiyo maana alikubali kumpa muda Mabeste akae mbali na familia ili apate muda kutafuta lakini Mabeste hakufanikiwa, ila Lisa anasahau jambo moja suala la kulea familia ni la Mwanaume na mwanamke na si mtu 1.

Mabeste ameeleza jambo la kusalitiwa na Mke wake ila Lisa hakusema wapi ambapo Mabeste alimsaliti, labda nahisi kwa sababu Mabeste hakuwa vizuri kipesa ndiyo maana alishindwa kumsaliti mpenzi wake, lakini Mabeste anasahau angekuwa mpambanaji kama mkewe pengine hata usaliti usingekuwepo.

Ukimsikiliza mke alikuwa mbunifu sana kuhakikisha anafanya kazi kulea familia, ndiyo maana, alidai aliitunza familia karibia miezi 6 lakini Mabeste hakufanya chochote, haikuwa sawa lakini kusaidiana kwenye familia ni jambo la kawaida sana.

Mwisho hatuwezi kumlaumu Mabeste au Lisa kwa kilichotokea maana mambo ya Ndoa wanaojua ni waliokuwa ndani ya Ndoa,lakini kwa sisi wapenzi watazamaji unagundua kulikuwa na makosa ya pande zote mbili, Mabeste hakumjua mke alikuwa anahitaji nini kwa ajili ya familia, na Mke ia hakujua Mabeste alikuwa anahitaji nini kwenye familia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo sababu za Lisa ni kisingizio tu mbona Davido juzi kachapiwa mrembo wake pamoja na kumiliki kiwango kikubwa cha naira
 
Siku hizi ndoa zikifa, mwanamke ili kujitetea anasema tu alikuwa haridhishwi.... nakumbuka Mabeste alivyopigania afya ya mkewe halafu hili wala halisemi popote.

Njaa imeingia mke katunza familia miezi sita tu kasanda, mbaya zaidi kaenda kuliwa na rafiki wa Mabeste.... mke hana cha ziada kwenye ndoa ila ngono tu..!!
 
Nadhan mwanamke hakuwa Mvumilivu vya kutosha, nadhan ni wale aina ya wanawake wa mjini ambao Elimu na akili hakuna kichwani.
Wao wanataka wawe juu kila siku.

Wahenga walisema. " Filisika ujue tabia ya mkeo".
 
Back
Top Bottom