Imechukua muda mrefu sijasikia sauti ya Mabere Mkaubi wa ITV. Kwa Mikoa ya Kanda ya Ziwa Mabere Makubi amekuwa akiripoti habari kupitia kituo chenu habari ya uhakika na kwa kweli Mabere Makubi anapendwa sana na wananchi wa Kanda ya Ziwa kutokana na umahiri wake. Inawezekana kuwa kuna tofauti kati ya Mabere na mtu fulani lakini mnatakiwa mfuatilie chanzo cha tofauti na kulitolea uamuzi badala ya mtu kukaa kijiweni. Mabere ni mwandishi nguli na Kanda ya Ziwa tunampenda kutoa habari zake upitia kituo chenu cha ITV.