Mabere Marando awania Uspika kupitia CHADEMA

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,695
1,696
Yule Mwanasiasa machachari wa mageuzi Mpiganaji Mabere Nyaucho Marando, amechukua form ya kugombea Uspika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano kupitia CHADEMA.

Pamoja na yeye kuna vijana wengine kama watatu waliojitokeza kupitia CHADEMA. (Source: ITV News Bulletin)

Kama muujiza ukitokea na Marando akawa Spika wa Bunge, basi Katiba Mpya iko mbioni kupatikana kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015. Pia itakuwa ni pigo kubwa kwa Mafisadi wote.
 
habari njema hii!:smile-big:
 
Niliwahi kusikia Mbowe akisema Dr. Slaa akikosa Urais basi atagombea Uspika. Au mipango imebadilika?

Pia Dr. Slaa amesikika akiwaambia wananchi kuwa atawatumikia akiwa Katibu Mkuu CHADEMA.

Imekaaje hii?
 
CCM hawawezi kufanya kosa kama hilo

Mtu Mmoja, CCM mpaka sasa tayari wana candiadtes 12 tofauti na miaka yote. Ushindani Mkubwa unaonekana utakuwa kati ya majina makubwa kama: Samuel Sitta; Andrew Chenge. Anna Abdalah na Anna Makinda.

Kama ushindani ukiwa mkubwa na ukaweka makundi ambayo hayavunjika, kuna hatari ya kupiga kura za chuki na kuupa upinzani ushindi.

Hata hivyo hili linaweza kutegemea na upinzani kama utakubaliana kutoa candidate moja.

Kama nilivyosema, kama muujiza huu utawezekana, then Tanzania yenye neema, ile ya Asali na Maziwa inaweza kuzaliwa!
 
Niliwahi kusikia Mbowe akisema Dr. Slaa akikosa Urais basi atagombea Uspika. Au mipango imebadilika?

Pia Dr. Slaa amesikika akiwaambia wananchi kuwa atawatumikia akiwa Katibu Mkuu CHADEMA.

Imekaaje hii?

Kwa maoni yangu, Dr. Slaa ni vema ashughulike na kuimarisha chama. Asijaribu kugombea tena Uspika ambao nafasi ya kushinda ni finyu sana.

Kuna thread niliona mdau moja amesikia tetesi kuwa EL na RA na Felix Mrema wamechanga zaidi ya USD 1 Million ili zifanye kazi ya kumpigia kampeni Andrew Change.

Moja kati ya issue moto inadaiwa ni kumkinga Massawe wa TANROADS.
 
Yule Mwanasiasa machachari wa mageuzi Mpiganaji Mabere Nyaucho Marando, amechukua form ya kugombea Uspika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano kupitia CHADEMA.

Pamoja na yeye kuna vijana wengine kama watatu waliojitokeza kupitia CHADEMA. (Source: ITV News Bulletin)

Kama muujiza ukitokea na Marando akawa Spika wa Bunge, basi Katiba Mpya iko mbioni kupatikana kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015. Pia itakuwa ni pigo kubwa kwa Mafisadi wote.

cha cha cha! Kaka usitoe siri, yaache hayo mavuvuzela ya kijani yajichanganye wampe marando uspika halafu ndio wapate bakora yao! Otherwise thank you for the good news!
 
Mtu Mmoja, CCM mpaka sasa tayari wana candiadtes 12 tofauti na miaka yote. Ushindani Mkubwa unaonekana utakuwa kati ya majina makubwa kama: Samuel Sitta; Andrew Chenge. Anna Abdalah na Anna Makinda.

Kama ushindani ukiwa mkubwa na ukaweka makundi ambayo hayavunjika, kuna hatari ya kupiga kura za chuki na kuupa upinzani ushindi.

Hata hivyo hili linaweza kutegemea na upinzani kama utakubaliana kutoa candidate moja.

Kama nilivyosema, kama muujiza huu utawezekana, then Tanzania yenye neema, ile ya Asali na Maziwa inaweza kuzaliwa!

huko pia wanweza kuchakachua kivingine vingine, bongo hii mkuu!
 
Duh! Mkuu toka asubuhi nilikuwa sijacheka, thanks for making my day though a bit late.

Endelea kuomba makundi yawe so strong kisha zipigwe kura za chuki.
 
cha cha cha! Kaka usitoe siri, yaache hayo mavuvuzela ya kijani yajichanganye wampe marando uspika halafu ndio wapate bakora yao! Otherwise thank you for the good news!

hashwaaaa!! tuwakaushie kwanza wapate supraizzz
 
huko pia wanweza kuchakachua kivingine vingine, bongo hii mkuu!

Hakuna kisichowezekani Tanzania. Only in Tanzania Uchakachuaji unaweza kufanyika na maisha yakasonga mbele kama kawaida kama vile hakuna kilichotokea.
 
hashwaaaa!! tuwakaushie kwanza wapate supraizzz

Piga picha ifuatayo ya safu ya hoja Nzitto kwa maslahi ya taifa:

1. Spika - Marando - (Muunda Kamati)
2. Tindu Lissu - Hoja binafsi ya Katiba
3. Mwakyembe - Mwenyekiti wa Tume Maalumu ya Kuunda Katiba Mpya
4. Zitto Kabwe - Mjumbe wa Kamati
5. Halima Mdee - Mjumbe wa Kamati na Katibu wa Kamati
6. Anne Kilango - Mjumbe wa Kamati
7. Freeman Mbowe - Mjumbe wa Kamati
8. Hamadi Rashidi - Makamu Mwenyekiti wa Kamati
.
.
.

Hebu nimalizieni kamati hii ya watu 10 itakayoleta Tanzania Mpya . . . . Mmmh! Au naota tu?
 
Kwa kuwa sisiemu wamekuwa wengi basi nawashauri wapinzani waungane na kumwacha mpiganaji mmoja ili ateiki advantage hiyo!
 
Piga picha ifuatayo ya safu ya hoja Nzitto kwa maslahi ya taifa:

1. Spika - Marando - (Muunda Kamati)
2. Tindu Lissu - Hoja binafsi ya Katiba
3. Mwakyembe - Mwenyekiti wa Tume Maalumu ya Kuunda Katiba Mpya
4. Zitto Kabwe - Mjumbe wa Kamati
5. Halima Mdee - Mjumbe wa Kamati na Katibu wa Kamati
6. Anne Kilango - Mjumbe wa Kamati
7. Freeman Mbowe - Mjumbe wa Kamati
8. Hamadi Rashidi - Makamu Mwenyekiti wa Kamati
.
.
.

Hebu nimalizieni kamati hii ya watu 10 itakayoleta Tanzania Mpya . . . . Mmmh! Au naota tu?

Unaota
 
hapa bunge linweza hata kuvunjika ....si mchezo
 
It is possible bunge lina viti kama 323 hivi hadi sasa wapinzani wana kura(viti) kama 100 bado kama 50, mavuvuzela yakijichanganya kama yalivyoanza kuzomeana kwenye vyombo vya habari yanagawa kura zao kwa chuki wakitahamaki tayari kumekucha.
 
Kama ni hivi baada tu ya wiki rais anavunja bunge.
 
Piga picha ifuatayo ya safu ya hoja Nzitto kwa maslahi ya taifa:

1. Spika - Marando - (Muunda Kamati)
2. Tindu Lissu - Hoja binafsi ya Katiba
3. Mwakyembe - Mwenyekiti wa Tume Maalumu ya Kuunda Katiba Mpya
4. Zitto Kabwe - Mjumbe wa Kamati
5. Halima Mdee - Mjumbe wa Kamati na Katibu wa Kamati
6. Anne Kilango - Mjumbe wa Kamati
7. Freeman Mbowe - Mjumbe wa Kamati
8. Hamadi Rashidi - Makamu Mwenyekiti wa Kamati
.
.
.

Hebu nimalizieni kamati hii ya watu 10 itakayoleta Tanzania Mpya . . . . Mmmh! Au naota tu?

this is too much for you mzee, siamini kama na wewe huwa unajilisha upepo kiasi hiki!!
 
It is possible bunge lina viti kama 323 hivi hadi sasa wapinzani wana kura(viti) kama 100 bado kama 50, mavuvuzela yakijichanganya kama yalivyoanza kuzomeana kwenye vyombo vya habari yanagawa kura zao kwa chuki wakitahamaki tayari kumekucha.

Katika extreme possibilities hili linawezekana ili mradi tu watu wanaangalia maslahi ya nch na si ya chama.

Wakati wa Uchaguzi niliona katika Luninga wapiga kura wa Mwananyamala wanaandamani kuwa waliyemchagua kura zake zimechakachuliwa. Cha ajabu ni kuwa mgombea waliyekuwa wanampigania ni wa CHADEMA na waliokuwa wanaandamani ni wana CCM, CHADEMA na CUF.

Katika extreme possibilities inawezekana Spika akatoka upinzani hasa kwa hoja uliyoitoa.
 
Mtu Mmoja, CCM mpaka sasa tayari wana candiadtes 12 tofauti na miaka yote. Ushindani Mkubwa unaonekana utakuwa kati ya majina makubwa kama: Samuel Sitta; Andrew Chenge. Anna Abdalah na Anna Makinda.

Kama ushindani ukiwa mkubwa na ukaweka makundi ambayo hayavunjika, kuna hatari ya kupiga kura za chuki na kuupa upinzani ushindi.

Hata hivyo hili linaweza kutegemea na upinzani kama utakubaliana kutoa candidate moja.

Kama nilivyosema, kama muujiza huu utawezekana, then Tanzania yenye neema, ile ya Asali na Maziwa inaweza kuzaliwa!

Mkuu Superman,

Ninakubaliana na analysis ya kwako, hapa cha kuomba ni kimoja mipasuko iendelee ndani ya chama ili kuiweka CC kwenye wakati mgumu zaidi. Tatizo la wabunge wengi wa CCM ni wepesi kurubuniwa na mafisadi. Tone ya wabunge siku Lowassa anaachia ngazi ilikuwa kali sana, after few days wengi walishaanza kubadilisha misimamo yao. Lakini kwa misukosuko waliyoipata majimboni hawana uhakika kama 2015 watabahatika tena kurudi mjengoni nina imani watakuwa makini kwenye upigaji kura wao na salaam za wapiga kura za mwaka huu zitawafanya watumie akili kupiga kura.

Marando ana maswahiba wengi CCM na hata kwenye Bunge la Afrika Mashariki walimpa kura nyingi tu, lakini hicho hakiwezi kuwa kigezo, maana wakati huo alikuwa akigombea na watu wengine wa kambi ya upinzani. Kama anagombea na m-CCM mwenzao, ili wampe kura lazima wawe na uhakika kwamba huyo m-CCM ni mchafu au akichaguliwa kuwa Spika atawaharibia mbio zao za kurudi mjengoni ifikapo mwaka 2015.

Nilisikia pia Mh. Hamad Rashid nae alikuwa anafikiria kugombea, nadhani hapo ndipo panaweza kuwa na tatizo. Sina tatizo na wote wawili, lakini wangekaa na kukubaliana ili mmoja kati yao aungwe mkono na Kambi yote upinzani [minus Mrema wa TLP].
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom