Nice song. Isn't it?
Siku hizi hatuna misamiati ya mabepari, mabeberu, ukoloni mamboleo, makabaila, makupe na mabwanyenye kwani tuliwazika Zanzibar mwaka 1992. Siku hizi tuna wajasiriamali, wawekezaji, wadau wa kimaendeleo, wafadhili na utandawazi. Kilichobaki sasa ni kuyafutilia mbali hayo maneno ya kizamani kwenye kamusi zetu za kiswahili.