Mabepari walia, mabepari walia, kukatiwa mirija!

hahaa acha bana, enzi za mwalim hapo mmepanga mstari mrefu mnasindikizwa na bendi ya shule ahsante mkuu 4 gud memories.
 
Mwalimu aliwatimua Mwinyi akawarudisha. Mkapa akawakabidhi nyumba na Kikwete sasa yuko bize kuwakabidhi mashamba.
 
si mpaka wakatiwe mirija; sasa hivi wameichomeka kila penye nafasi na wanafyonza kama wana wazimu hivi!
 
Nice song. Isn't it?

Siku hizi hatuna misamiati ya mabepari, mabeberu, ukoloni mamboleo, makabaila, makupe na mabwanyenye kwani tuliwazika Zanzibar mwaka 1992. Siku hizi tuna wajasiriamali, wawekezaji, wadau wa kimaendeleo, wafadhili na utandawazi. Kilichobaki sasa ni kuyafutilia mbali hayo maneno ya kizamani kwenye kamusi zetu za kiswahili.
 
Umesahau na mafisadi
 
@Mwafrika, nami pia, sijakuanmask...
@Chimunguru, those were the old good days...
@Jasusi, ukiwakosoa unatafuta matatizo...
@Mwanakijiji, @Charity, @Tata; siku hizi hizo nyimbo 'zimepigwa marufuku' -- hakuna 'uthubutu' wa kuunanga ubepari
@Masaki, if we joined them, Tanzania ingeamua kufuata ubepari, ingekuwa vizuri, tungejua moja. Lakini kwa mujibu wa katiba, Tanzania ni nji ya ujamaana kujitegemea; matokeo yake umekuwa wa kujimegea bin kujigemea.

Way to go.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom