Mabenki yote Tanzania imarisheni ulinzi kipindi hiki cha uchaguzi

Magezi

JF-Expert Member
Oct 26, 2008
3,341
2,000
Nawakumbusha wamiliki wa mabenki nchini kwamba kila kipindi anapokuja raisi mpya kunakuwa na matukio mengi ya uvamizi wa mabenki. Kumbuka mwaka 2005 tulishuudia benki nyingi zikivamiwa wakati huo Mahita akiwa IGP.

Mwaka 2010 uvamizi haukuwa mkubwa kwa sababu raisi aikuwa na kila dalili za kushinda kwa hiyo system haiparaganyiki. Sasa hivi ni tofauti kwani hata Idara nyeti za usalama hawana hakika nani anakuja kuwa bosi wao ndo maana mengi utayaona kipindi hiki, utadhani idara hizi ziko likizo.

Kwa hiyo ni ombi langu kwa mabenki hasa ambayo yana matawi wilayani waongeze askari kwa muda mmoja. Mfano hivi sasa askari wanne wanatakiwa kuwa nje na wawili ndani ya benki muda wote wa mchana.

Kama hamtatekeleza haya msilaumu eti hatukujua, huu ni ushauri tu kwa nia njema.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom