Mabenki yaanza kukusanya Tozo za Serikali kwenye miamala wanayofanya wateja

KWENU, National microfinance bank(nmb),hua mnajinasibu na kujifaragua kwamba ukiwa na akaunti ya nmb kutuma pesa kwenda nmb ni bure(Kama nimekosea msomaji mwingine anaweza kunikosoa au kunirekebisha) Sasa Jana usiku mmeniletea ujumbe yakwamba tunakusanya tozo za serikali kutokana na miamala uliofanya.
Miamala niliofanya ni ya kwenda nmb pia,Sasa je Kuna tozo nmb kwenda NMB? Kama lipo mbona wateja hatufahamu?
Kama ndio hivyo ondoeni Ile tangazo kwamba kutuma pesa nmb kwenda nmb ni bureeeeee,
Ni kweli ilikua bure nmb to nmb before hii tozo haijaletwa. Hata sasa nmb bado pia hawana commission wanayopata kwenye hii miamala. Hayo makato yote yanaenda serikalini.
 
hapa tutaibiwa sana na mabenki maana hata hawajasema wanakata shilingi ngapi kwa kiasi gani, mameneja na watumishi wao watatuna mashavu maanaa ni full kujimegemea mabulungutu tu ……..
 
Mwigulu amekuja na kwenye akaunti zetu za ada za watoto... lengo lao ni nini hawa kima
 
Tudai pesa kama mishahara itolewe cash.. siku ya mshahara kila mtu aende na kamfuko kake kulingana na mshahara wake
hapa tutaibiwa sana na mabenki maana hata hawajasema wanakata shilingi ngapi kwa kiasi gani, mameneja na watumishi wao watatuna mashavu maanaa ni full kujimegemea mabulungutu tu ……..
 
Naplan kuweka akiba huko bank kesho, saa itakuaje wajumbe!!!..
 
LEO NIMEPATA SMS KUTOKA NMB BANK IKISEMA IFUATAVYO

Ndugu Mteja, tunakusanya tozo ya serikali kwenye akaunti yako kwa miamala ya tarehe 8 Sep 2021 mpaka 6 Oct 2021. Unaweza hakiki kupitia taarifa ya akaunti.

Ujumbe huo. Watanzania inafika point huna pakupumua kila sehemu tozo bank tozo kwenye simu tozo. Mnataka tuende wapi? Juzi nimetuma crdb to crdb nimeliwa 7500 huku nmb napo wanachukua tozo.

Kwenye simu miamala moto unawaka. Tunaumizana sana nchi hiiii
Huu ni upumbavu uliopitiliza...kwanini Kama ni tozo wasitoe taarifa kwanza ndio waanze kukata? Hyo miamala nisingeifanya Kama ningejua Kuna hayo matozo yenu otherwise kwanini msingebeba huo mzigo wa hayo makato ninyi mnahamisha kwa wateja ambao hamkuwaambia? Huu mi ushenzi sana. Nimeangalia akaunti yangu nimekatwa zaidi ya elfu 50...
 
2025 maamuzi ni yenu twende na serikali ya Tozo au mabadiliko... Tatizo hatujawahi kujitambua wala kuijua nguvu ya umma kila mtu anaiogopa serikali jeshi na mamlaka ilihali wao ndio wanaotutegemea kwa kulipa kodi na Tozo fungukeni acheni uzuzu
 
Huu ni upumbavu uliopitiliza...kwanini Kama ni tozo wasitoe taarifa kwanza ndio waanze kukata? Hyo miamala nisingeifanya Kama ningejua Kuna hayo matozo yenu otherwise kwanini msingebeba huo mzigo wa hayo makato ninyi mnahamisha kwa wateja ambao hamkuwaambia? Huu mi ushenzi sana. Nimeangalia akaunti yangu nimekatwa zaidi ya elfu 50...
Kesho nawafata rasmi wanitolee app zote kwenye simu yangu pamoja na simbanking tuone hizo tozo watamkata Nani..pumbavu sana
 
LEO NIMEPATA SMS KUTOKA NMB BANK IKISEMA IFUATAVYO

Ndugu Mteja, tunakusanya tozo ya serikali kwenye akaunti yako kwa miamala ya tarehe 8 Sep 2021 mpaka 6 Oct 2021. Unaweza hakiki kupitia taarifa ya akaunti.

Ujumbe huo. Watanzania inafika point huna pakupumua kila sehemu tozo bank tozo kwenye simu tozo. Mnataka tuende wapi? Juzi nimetuma crdb to crdb nimeliwa 7500 huku nmb napo wanachukua tozo.

Kwenye simu miamala moto unawaka. Tunaumizana sana nchi hiiii
Ninachoshindwa kuelewa hii miamala inawiana vipi kwa mtu yuleyule ambaye amekatwa muamala wake kwenye simu, kwenye luku na kwenye akaunti ya benki, siamini kama Tanzania tuna data base ya utambulisho wa kama wenzetu wa huko Ulaya au Marekani ambayo inaweza kumtambulisha mtu kila sehemu iwe kwenye mabenki,ajira n.k, sasa kila sehemu unakatwa wakati tayari hayo makato umeshakatwa sehemu nyingine kama vile kwenye miamala ya simu,je wanajuaje kuwa huyu akakatwe au asikatwe sababu tayari ama umeshakatwa kwenye miamala ya kwenye simu. Mimi nadahani serikali ingekamilisha kwanza zoezi la kutoa namba za utambulisho kwa raia wote na namba hiyo ya utambulisho iwe kwenye data ambayo taasisi zozote zinaweza access kwa pamoja. Hivi sasa pamoja na kuwa na vitambulisho vya uraia ,mtu wa benki hawezi access data zako au hata uhamiaji nao hawawezi access hizo data zako hadi unaambiwa kajaze tena form wakati tayari una pasipoti iliyoisha na taarifa zako zipo kwenye faili lako!
 
Kesho nawafata rasmi wanitolee app zote kwenye simu yangu pamoja na simbanking tuone hizo tozo watamkata Nani..pumbavu sana
Pamoja na kutowapenda mabeberu hapo ndio nawaona angalau wanajali sababu haya makato ingekuwa ni majuu tayari benki zingeshtakiwa na hata serikali ingeshtakiwa, pia sielewi hii miamala wanaidhibiti vipi na sisi ''tuliokubali'' hiyo miamala tutajuaje kuwa hiki ndio kiasi kamili kilichotokana na tozo, sababu hizi tozo hazina base ya kuweza kujua kuwa A,B na Z wanatakiwa au wamelipa kiasi gani ni kama vile tunabahatisha tu, nasema tunabahatisha tu kwani serikali haijafanya makadirio sahihi kwa kila anayetumia hii miamala.
 
Hivi hatuna wazalendo kuishtaki serikali kwa.huu uhalifu? Mimi hata sielewi tozo ina misingi ipi ya kisheria na kimaadili. Fikiria mfanyakazi ambaye amekwisha kulipa kodi, msingi wa tozo kwenye miamala anayofanya ni upi?
 
Back
Top Bottom