Mabenki yaanza kukabili wezi wa Kimtandao

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Jumuiya ya Mabenki kutoka nchi mbalimbali za ukanda wa Afrika Mashariki zimeanza mkakati wa kuimarisha Usalama wa fedha katika miamala ya kibenki ili kudhibiti ongezeko la uhalifu wa kimtandao unaotishia kuathiri ukuaji wa uchumi wa Nchi.

Akiongea katika kongamano la 19 la taasisi za kifedha zinaloandaliwa na jumuiya ya Mabenki linalofanyika kwa siku tano katika hotel ya Ngurdoto Nje kidogo ya jiji la Arusha,Naibu gavana wa Benki kuu , udhibiti wa fedha na usimamizi wa Mabenki (Bot), dkt.Bernard Kibesse alisema kongamano hilo linalenga uadilifu na uaminifu kwa watoa Huduma za kifedha kwenye Mabenki na taasisi za kifedha.

Alisema ongezeko la teknolojia katika masuala ya kifedha yamekuwa na faida kubwa katika ukuaji wa uchumi lakini yamekuwa na hasara zake ambapo watu wasio waaminifu wamekuwa wakizitumia katika kuharibu ufanisi wa mabenki.

"Taasisi za fedha hapa nchini zimejipanga vizuri katika kukabiliana na mabadiliko ya mazingira ya Kidigitali katika kuhakikisha wizi wa kimtandao unadhibitiwa" Alisema Dkt Kibesse.

Amesema kuwa kukua na kuimarika kwa huduma za kibenki kwa kiasi kikubwa, ikiwemo miamala ya kifedha ya kielektroniki, kumeenda sanjari na ongezeko la uhalifu wa ki mtandao na kuathiri ukuaji wa uchumi wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo.

Kwa upande wake,Patrick Msusa Mkurugenzi mtendaji wa chuo cha mafunzo ya kibenki Nchini(TIOB),amesema kongamano hiyo limekuwa likiandaliwa na taasisi tatu za Mabenki kutoka nchi za Kenya na Uganda na kuwakutanisha wataalamu wa fedha kutoka wanachama wa nchi za ukanda wa jumuiya ya Afrika mashariki.

Amesema kuwa katika kongamano hilo wamelenga kuangalia maadili katika matumizi ya miamala ya fedha kwa nchi za Afrika mashariki kutokana na matumizi ya mfumo wa Tehama na wamelenga kuboresha Huduma za miamala ya fedha kwa njia ya kielektroniki.

"Uimara wa Huduma za kifedha duniani kote ndio mhimili muhimu katika ukuaji wa uchumi wa Taifa husika"

Alisema mfumo huo unapaswa kuwa salama ili kufikia lengo husika na sasa wataalamu kutoka sekta ya fedha na benki pamoja na wataalum wa Tehama watatoa mwelekeo sahihi juu ya usalama wa fedha kutokana na ongezeko la teknolojia katika utekelezaji wa miamala ya kifedha.

Kongamano hili linazijumuisha nchi kutoka Kenya, Uganda, sudani ya kusini na Tanzania kama mwenyeji

IMG-20190812-WA0009.jpeg
 
Back
Top Bottom