Mabenki Tanzania Mnaniudhi sana hata sijui mameneja kwanini hambadiliki

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,574
8,591
Hakuna kitu kinaninyong'onyesha Moyo kama haya mabeki Tanzania na sijui ninani mkemeaji mkuu wa haya mabenki kama ni BOT Basi kazi yao hao waliopewa dhamana kuyasimamia hawajui, labda kingine naweza kusema mabenki ni wababe!

Narudi katika mada unakuta Benki una Teller 8 lakini inafanya kazi 1-2 zingine 7 hazitumiki na msururu wa wateja ni kilomita moja na meneja kakaa bila yakufanya maboresho!

Mfano NMB, CRDB, NBC Ndiyo benki zenye wateja wengi kwakweli hawa watu siju hata wanachokiwaza hata kama wahudumu hakuna kwanini wasiajiri?
na hii foleni ya wateja nikila siku sasa usiombe mwisho wa wiki na mwezi! kweli inasikitisha sana kama BOT Ndiyo wasimamizi fanyeni kwakila linawezekana kukemea huu upuuzi.
 
Tujitahid tu kutumia tigo teller,mpesa teller,zantel teller na airtel money teller wasipotuona kwenye milango yao ya bank watabadilika.HAO BOT,HAWANA TOFAUTI NA TUME YA MAWASILIANO NA TUME NYENGNE MBAL MBAL ZILIZOPEWA KAZ YA KUMSIMAMIA MTZ LAKIN HAZINA MUDA HUO WA KUMTETEA
 
Banks na kampuni za mawasiliano wangefanya mobile banking hadi kudeposit cyo kudraw tuu hela kutoka kwenye bank ac wafanye nakuhamisha pesa kutoka mpesa tigopesa etc kwenda accnt ya bank if its possible hii itapunguza foleni.
 
Hiyo mbona IPO karibia bank zote unaweza kudraw na Ku deposit via simbanking
 
Banks na kampuni za mawasiliano wangefanya mobile banking hadi kudeposit cyo kudraw tuu hela kutoka kwenye bank ac wafanye nakuhamisha pesa kutoka mpesa tigopesa etc kwenda accnt ya bank if its possible hii itapunguza foleni.

Naona technolojia imekuacha mbali, huduma za kuweka hela kwa mitandao ya simu zipo siku nyingi kabisa.
 
nshawahi kupiga simu makao makuu CRDB na NMB mara nyingi sababu hiyo, afu kinachokera unakuta manager anapiga story na clerks wanachekaachekam au jamaa wako wawili mmepanga foleni anashika simu anaanza kuongea...

Nje ATM machine mtu unaweza kutoa hela na kuingiza pesa kiasi chochote kwenye account, kuhamisha fedha kwenda account flani na huduma nyingi sana kupitia kwenye ATM machine ambazo zitapunguza foleni ya kijinga.. Kuna huduma nyingi sana ambazo wange-automate ungekua ukienda benki unakuta foleni watu kumi tu.. hata kutumia Virtual accounts, hivi bongo watu wa IT, Computer science wamelala kufanya kitu kama hicho kupiga hela....
 
Labda bank yangu nayotumia ndo imeachwa corz mtandao naotumia unaniruhusu kununua salio na kuuliza bal na statement kwa bank accnt yangu ts tigo & Nbc.
 
nshawahi kupiga simu makao makuu CRDB na NMB mara nyingi sababu hiyo, afu kinachokera unakuta manager anapiga story na clerks wanachekaachekam au jamaa wako wawili mmepanga foleni anashika simu anaanza kuongea...

Nje ATM machine mtu unaweza kutoa hela na kuingiza pesa kiasi chochote kwenye account, kuhamisha fedha kwenda account flani na huduma nyingi sana kupitia kwenye ATM machine ambazo zitapunguza foleni ya kijinga.. Kuna huduma nyingi sana ambazo wange-automate ungekua ukienda benki unakuta foleni watu kumi tu.. hata kutumia Virtual accounts, hivi bongo watu wa IT, Computer science wamelala kufanya kitu kama hicho kupiga hela....

Mengine mkuu hayawezekani kwenye ATM mfano MTU una cash unataka kuweka kwenye akaunti, hii ni ngumu. Sijajua hii ya m-pesa kwenda benki makato yake yakoje? Suluhisho ni mameneja wa benki kuhakikisha kuwa madirisha yote yanafanyakazi hasa pale kunapokuwa na watu wengi!
 
Haiwezekani kwenye ATM za tanzania, huku una cash ATM inasehemu ya kuweka vizuri tu inaingia kwenye account bila hata shida...
 
Back
Top Bottom