iparamasa
JF-Expert Member
- Nov 14, 2013
- 13,437
- 14,924
Serikali huwa ina utaratibu wa kudhamini watumishi wake ili wapate mikopo katika taasisi za fedha,na serikali hulazimika kuwasilisha makato ya kila mwezi kwenye taasisi hizo.
Mabenki,kabla ya kukopa,huitaka serikali iyathibitishie kwamba mfanyakazi husika KWELI ni mtumishi wa umma na inamtambua,baada ya uthibitisho huo,mabenki humkopesha mfanyakazi husika.
Ni wazi kwamba katika wafanyakazi karibu elfu kumi waliotimuliwa,wapo waliokopeshwa na mabenki kwa dhamana ya serikali,
Mabenki yaliamini kauli ya serikali kwamba hao ni wafanyakazi halali na wanakopesheka,sasa serikali imegeuka na kusema wafanyakazi hao si halali,nadhani ni wajibu wa serikali kuyafidia mabenki haya ambayo mpaka sasa mengi yamekwama kiuchumi.
Kuyaongezea hasara hii,si haki,wao waliaminishwa na serikali na si haki serikali iyatie hasara mabenki
Hii inaenda mpaka kwenye mifuko ya pensheni ambayo kuanzia mwezi May mifuko hiyo itayumba kimapato,SACCOS,VICCOBA.
Ni vyema taarifa kama hizo zikawa detailed kwa kujumuisha madhara ya kifedha,kiuchumi na kijamii
Hatujapata tathmini pia kujua wafanyakazi hewa waligharimu benki hizi kiasi gani cha pesa,kulikuwa na wafanyakazi hewa 19,000, sasa ongeza na hao wenye vyeti feki 10,000,unapata watumishi 30,000
Nataraji mabenki na taasisi ya umoja wao watatoa kauli kuhusu hasara waliyopata na idadi ya watumishi waliokopa
Vinginevyo mtumishi kupata mkopo itakuwa ngumu