Abiria wafurahia usafiri wa treni Moshi - Dar

elivina shambuni

JF-Expert Member
May 31, 2018
461
295
Ijumaa Desemba 6, 2019 treni ya abiria itakayokuwa ikitoa huduma ya usafiri kati ya Dar es Salaam na Moshi, mkoani Kilimanjaro ilirejea baada ya kupita miaka 25. Treni hiyo yenye mabehewa manane iliondoka Dar es Salaam Ijumaa saa 10 jioni ikiwa na abiria 263 na 24 walipandia njiani.



Ilifika Moshi jana saa 5:30 asubuhi na siku hiyo saa 10 jioni ilianza safari kwenda Dar es Salaam na kufika leo Jumapili Desemba 8, 2019 saa 4:20 asubuhi. Iliondoka Moshi na abiria 241. Teddy Momburi, mmoja wa abiria wa treni hiyo amesema, “nimefika salama na huduma ni nzuri na za uhakika, pia treni ni safi.”



“Nauli ni rahisi ambayo ni Sh39,000, Sh23,500 na Sh19,000 kila mtu anaweza kumudu huu usafiri.” Ramadhani Shomary amesema, “treni ipo vizuri, nimevutiwa na huduma zake. Ni mara ya kwanza napanda treni kutoka Moshi ingawa nimewahi kupanda treni kwenda maeneo mengine.” Jamila Mustafa amesema, “nimependa usalama si kama basi. Pia ukiwa na watoto ni nzuri zaidi maana wanakaa vizuri wanaweza hata kucheza, kulala, kukaa. Mizigo pia unapand nayo mingi zaidi si kama kwenye basi. Kwa kweli ni usafiri salama zaidi.

 
Duh maskini Tz, wanafurahia wakati hayo ni mambo ya kawaida tu, siwalaumu ila nailamu Government
 
Ni hatua muhimu na jambo zuri kwa wakazi wa Mikoa ya Tanga,Kilimanjaro,Arusha na Manyara wanapata options nyingi ama watumie usafiri wa Ndege,Treni au Basi(Anga,Reli na Barabara)
 
Wanaoshangaa wananchi kushangilia mimi nawashangaa wao.

Hii ni hatua kama mzazi wako alivuruga familia yenu wewe ukaja kuiunganisha kwa nini ndg zako wasikuone wa maana na kukupongeza?.

Wengi wenu mnapinga kwa sababu zenu binafsi na ninahisi mna ubia kwenye kuona mabaya zaidi kwa watanzania wa kawaida wanayapata.

Ni jambo zuri kwa kurejesha huduma hii nikitambua shirika limeona upenyo hasa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.
 
NI USIKU AMBAOO WACHAGA WENGI AWAKUAMINI PALE MZIKI WA MAANA ULIPOPIGWAA VINYWAJI VIKIENDELEA KUGAIWA KILA.KONA

HAKIKA WALIFURAHII NA WENGINE KUANZA KUIMBA NYIMBO ZA KUMPONGEZA RAISI WETU DK JPM KWA KICHAGA

WAOARE AWAKUBAKI NAONNYUMA WAKIIMBA NYIMBO ZA KUMPONGEZA DK JPM

MWANZO NIKAHISI N HAFLA TUNAMSUBIRI MH RAISI KUHAMAKI TUKO MOSHI NAONA KIBAO KARIBU KILIMANJARO

KILA MJANJA ANA MJANJA WAKE KWA KWELI HII TRENI ILITUTETSA IMEOATA MJANJA WAKE

DK JP HONGERA SANA NTAKUWA MVIVU WA FADHILA BILA KUTOA PONGEZI

KAMA KWENU AIENDI SUBIRIA PASAKA LABDA MTAKUMBUKWA NA NYIE

SHIKAMOO DK MAGU
GODBLESS U
 
Wamekosekana mambiyetuuu ya sinzaa TI else unakamilisha weekend humohumoo
 
Back
Top Bottom