Cute Wife

JF-Expert Member
Nov 17, 2023
359
1,365
Upande wa wanyama naelewa, ila hapa kwenye shangazi kaja haijaingia akilini kabisa! Kwamba anayetumia begi/mfuko wa shangazi kaja, huo mfuko unahesabika kama silaha? Au mtu akibeba shangazi kaja anakuwa halipi nauli? Yeye siyo mlipa kodi ambaye pesa yake imechangia kwenye kukamilisha ujenzi wa mradi huu? Au yeye ndio hana hadhi ya kutumia usafiri huu?

Screenshot 2024-07-10 175719.png

Gen Z hilo hapo ndio begi la shagazi kaja

===

Wazee wa kubeba zawadi kwa ndugu jamaa na marafiki hii ni ya kwenu, hasa kwa wale mnatumia mabegi/mifuko hii ya shangazi kaja.

Kati ya vitu vilivyopigwa marufuku kwenye usafiri wa treni ya umeme (SGR) ni mabegi ya shangazi kaja, wanyama wakiwemo wa kufungwa (wazee wa kuagiza kitoweo tumefikiwa), mifuko ya plastiki, silaha, chakula, vinywaji, ndoo na mapipa pamoja na mizigo inayozidi kilo 30.

Kwa mujibu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), kila kinachofanyika kinalenga kulinda usalama wa abiria, kadhalika viwango vya ubora wa treni na huduma kwa ujumla.

Kwa sasa treni hiyo tangu ilipoanza kutoa huduma wiki tatu zilizopita, inafanya safari za kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro na kwamba kufikia Julai 25, mwaka huu safari zitaongezwa hadi Dodoma.

Mwananchi
 
Lazima kuwe na standard, wamechelewa tu, wangepiga marufuku watu kuvaa madela, ndala na kuongea ongea hovyo

Kuna watu hawana ustaarabu kabisa, unalikuta jitu kubwa jinga linaongea na simu kwa sauti kama vile linatoa muhadhara au linafungulia ma-video bila ya kuvaa earphones, ushamba ni mwingi sana Tanzania
 
Upande wa wanyama naelewa, ila hapa kwenye shangazi kaja haijaingia akilini kabisa! Kwamba anayetumia begi/mfuko wa shangazi kaja, huo mfuko unahesabika kama silaha? Au mtu akibeba shangazi kaja anakuwa halipi nauli? Yeye siyo mlipa kodi ambaye pesa yake imechangia kwenye kukamilisha ujenzi wa mradi huu? Au yeye ndio hana hadhi ya kutumia usafiri huu?

View attachment 3038608
Gen Z hilo hapo ndio begi la shagazi kaja

===

Wazee wa kubeba zawadi kwa ndugu jamaa na marafiki hii ni ya kwenu, hasa kwa wale mnatumia mabegi/mifuko hii ya shangazi kaja.

Kati ya vitu vilivyopigwa marufuku kwenye usafiri wa treni ya umeme (SGR) ni mabegi ya shangazi kaja pamoja, wanyama wakiwemo wa kufungwa (wazee wa kuagiza kitoweo tumefikiwa), mifuko ya plastiki, silaha, chakula, vinywaji, ndoo na mapipa pamoja na mizigo inayozidi kilo 30.

Kwa mujibu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), kila kinachofanyika kinalenga kulinda usalama wa abiria, kadhalika viwango vya ubora wa treni na huduma kwa ujumla.

Kwa sasa treni hiyo tangu ilipoanza kutoa huduma wiki tatu zilizopita, inafanya safari za kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro na kwamba kufikia Julai 25, mwaka huu safari zitaongezwa hadi Dodoma.

Mwananchi
Kwasababu halikai kwenye ile overhead luggage compartment
 
Lazima kuwe na standard, wamechelewa tu, wangepiga marufuku watu kuvaa madela, ndala na kuongea ongea hovyo

Kuna watu hawana ustaarabu kabisa, unalikuta jitu kubwa jinga linaongea na simu kwa sauti kama vile linatoa muhadahara au linafungulia ma-video bila ya kuvaa earphones, ushamba ni mwingi sana Tanzania
Ha ha ha ha hao wanao play video za ujinga ujinga kwa sauti huwa natamani nimzabe Kofi!
 
Kati ya vitu vilivyopigwa marufuku kwenye usafiri wa treni ya umeme (SGR) ni mabegi ya shangazi kaja pamoja, wanyama wakiwemo wa kufungwa (wazee wa kuagiza kitoweo tumefikiwa), mifuko ya plastiki, silaha, chakula, vinywaji, ndoo na mapipa pamoja na mizigo inayozidi kilo 30.

Kwa mujibu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), kila kinachofanyika kinalenga kulinda usalama wa abiria, kadhalika viwango vya ubora wa treni na huduma kwa ujumla.
Nilikuwa na spare parts zangu kwenye bag nikazuiwa, nilichojifunza ni kwamba ile treni ni kwa tabaka fulani la watu
 
Kwa hyo hizo treni watapanda matajiri watupu ndo maana yake.kuna kipindi magufuli alikiwa anataka kufungia mitumba.mimi ni mmoja wapo waliopinga hyo hatua.angalia kwanza wananchi wako Wana Hali gani ya kimaisha?treni inatumika na watu wa Hali ya chini.mwenye hela anakwenda kupanda basi
 
1720634720240.png

Dar es Salaam. Kama umezoea kuamua aina ya begi la kusafiria, kubeba kuku, mbwa na wanyama wengine unapokwenda kupanda basi, hali haiko hivyo kwenye usafiri wa treni ya umeme (SGR).

Kwa taarifa yako, begi la shangazi kaja, mizigo inayozidi kilo 30 na wanyama wakiwemo wa kufugwa si sehemu ya vitu unavyopaswa kuwa navyo unapotaka kwenda kupanda treni hiyo.

Kwa mujibu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), kila kinachofanyika kinalenga kulinda usalama wa abiria, kadhalika viwango vya ubora wa treni na huduma kwa ujumla.

Kwa sasa treni hiyo tangu ilipoanza kutoa huduma wiki tatu zilizopita, inafanya safari za kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro na kwamba kufikia Julai 25, mwaka huu safari zitaongezwa hadi Dodoma.

Sio kama wengi walivyozoea, unapotaka kupanda treni hiyo, yapo mambo ya msingi unapaswa kuzingatia.

Unayopaswa kufanya
Kwa mujibu wa TRC, abiria wanashauriwa kukata tiketi zao kupitia tovuti ya shirika hilo au katika madirisha yaliyopo vituoni angalau saa mbili kabla ya kuondoka ili kuepuka msongamano.

Abiria wakiwa ndani ya treni ya SGR inayofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Morogoro.

Kufika mapema katika stesheni ni jambo lingine linaloshauriwa na TRC kufanywa na abiria, ikisema angalau abiria afike kwenye eneo hilo saa moja kabla ya kuondoka.

Usiyopaswa kufanya
Mifuko ya plastiki, silaha, chakula, vinywaji, ndoo na mapipa si sehemu ya vitu anavyopaswa kuwa navyo abiria anayesafiri kwa treni hiyo.

Kama una mnyama wako awe wa kufugwa au mwingine haruhusiwi katika treni ya umeme.

Wale wenzetu wa mabegi ya ‘shangazi kaja’ treni hiyo haijawafikia, pia si ruhusa kupanda ukiwa na aina hiyo ya mfuko.

Mizigo yenye uzito uliopitiliza pia si ruhusa katika treni hizo, abiria wa daraja la biashara anapaswa kuwa na mzigo usiozidi kilo 30, huku daraja la uchumi usizidi kilo 29.

TRC ilianza huduma za SGR kati ya Dar es Salaam na Morogoro Juni 14, mwaka huu, huku Julai 25 safari zikitarajiwa kuongezeka hadi Dodoma.

Kwa mujibu wa TRC, miongozo hiyo inalenga kuhakikisha viwango vya usalama na uendeshaji vinazingatiwa.

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom