mr mkiki
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 5,583
- 11,659
Mtaalamu yeyote anayekwenda kinyume na matakwa ya watawala wa Tanzania, huyo anatumiwa na Mabeberu! Hiki ndio kisingizio kikubwa cha watawala wanapotaka kujisafisha kwa 'blunders' wanazofanya; 'Throw a blame to Mabeberu'. Ni moja ya tabia za Dystopian rulers.
Lakini wale wote wanaoenda kinyume na matakwa ya wananchi ndiyo wanapewa nafasi. Sasa hivi wanaosifia na kumshangilia Rais wana nafasi kubwa ya kuteuliwa nafasi za uongozi kuliko wahitimu wa vyuo vya uongozi. Na vijana wameona hiyo fursa na wanaitumia vizuri.
Hii ni hatari sana kwa maendeleo ya nchi huwezi kutumia siasa vibaya kiasi hichi.
Tanzania kama nchi masikini inayojitutumua ili kujikomboa, ingefaa bunge lijae watu makini zaidi, na nafasi za kisiasa zijazwe na watu wenye ufahamu mkubwa na uzalendo. Lakini wengi tuliomo kwenye siasa ni makanjanja, au wapambe, wakereketwa na mahawara wa wateule wetu.
Inategemea umetazama upande gani. Ukiwa na mali nyingi ambazo bado ni ghafi, ardhi kubwa isiyotumika vema, watu wengi wasio na afya ya akili na mwili, utasemaje ni tajiri? Nadhani tuseme nchi ina utajiri, lakini haijawa tajiri.
Shuleni tulifundishwa kuwa taifa linaundwa na mihimili mitatu: Serikali, Bunge na Mahakama. Lakini tunachokiona leo ni Serikali, Serikali na Serikali.
Unasema wewe sio beberu katika nchi yako.
Mwanasiasa akikwambia usiku mwema toka nje.
mr mkiki.