Mabeberu ndio kisingizio kikubwa cha watawala wanapotaka kujisafisha kwa 'blunders' wanazofanya. Hii ni moja ya tabia za "Dystopian rulers"

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,765
2,000
Mtaalamu yeyote anayekwenda kinyume na matakwa ya watawala wa Tanzania, huyo anatumiwa na Mabeberu! Hiki ndio kisingizio kikubwa cha watawala wanapotaka kujisafisha kwa 'blunders' wanazofanya; 'Throw a blame to Mabeberu'. Ni moja ya tabia za Dystopian rulers.

Lakini wale wote wanaoenda kinyume na matakwa ya wananchi ndiyo wanapewa nafasi. Sasa hivi wanaosifia na kumshangilia Rais wana nafasi kubwa ya kuteuliwa nafasi za uongozi kuliko wahitimu wa vyuo vya uongozi. Na vijana wameona hiyo fursa na wanaitumia vizuri.

Hii ni hatari sana kwa maendeleo ya nchi huwezi kutumia siasa vibaya kiasi hichi.

Tanzania kama nchi masikini inayojitutumua ili kujikomboa, ingefaa bunge lijae watu makini zaidi, na nafasi za kisiasa zijazwe na watu wenye ufahamu mkubwa na uzalendo. Lakini wengi tuliomo kwenye siasa ni makanjanja, au wapambe, wakereketwa na mahawara wa wateule wetu.

Inategemea umetazama upande gani. Ukiwa na mali nyingi ambazo bado ni ghafi, ardhi kubwa isiyotumika vema, watu wengi wasio na afya ya akili na mwili, utasemaje ni tajiri? Nadhani tuseme nchi ina utajiri, lakini haijawa tajiri.

Shuleni tulifundishwa kuwa taifa linaundwa na mihimili mitatu: Serikali, Bunge na Mahakama. Lakini tunachokiona leo ni Serikali, Serikali na Serikali.

Unasema wewe sio beberu katika nchi yako.

Mwanasiasa akikwambia usiku mwema toka nje.

mr mkiki.
 

Bana likasi

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
6,950
2,000
Neno Mabeberu hutumiwa na watu wavivu walioshindwa kutatua kero za watu hivo ujificha kwenye kichaka cha kuwatupia wengine lawama
 

mr yamoto

JF-Expert Member
Oct 2, 2016
906
1,000
Chadema kwa sasa ndo chama tawala kwa jinsi CCM wanavyo pambana.

Wanatumia neno Mabeberu kama kinga kwenye Mambo yao ya mauajia.

Alafu hapo hapo wanaomba hela wasamehew. Kima kabisa MACCM
MACCM ni sawa na Nzi
 

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,918
2,000
Humu kuna watu wameanza usifia huku wakiweka contact zao mpaka na CV. Hii tabia awamu zilizopita haikuwepo kabisa
 

Akili 09 Nguvu 01

JF-Expert Member
Jun 23, 2015
591
1,000
Kuna jamaa humu hua anapenda kusema "Tafuta wa Kumlaumu"
Ukitaka kupata ahueni ya matatizo yako basi wewe cha kufanya "Tafuta wa kumlaumu" umbebeshe yeye lawama zako.
Kwaiyo sisi Watanzania Lawama zetu tunawapa Mabeberu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom