Mabaya yote yafanywayo na serikali ya CCM yanaweza kuvumilika lakini siyo hili

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,855
401
Ndugu zangu na haswa mashabiki na wapenzi wa chama cha magamba, hili ni onyo kwenu na mkipuuzia ole wenu siku yaja tena inabisha hodi. Katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni imejitokeza tabia ya askari kuua raia wasio na hatia. Tukio la hivi karibuni ni la Nyamongo ambapo raia zaidi ya watano tena wasio na hatia waliuawa. Jambo hili limeanza kuzoeleka miongoni mwetu na kuonekana kuwa ni la kawaida. Lakini ukweli ni kuwa huo ni unyama mkubwa usiovumilika. Inawezekana mimi na wewe msomaji bado hujawa mhanga wa hiyo tabia ya askari lakini piga picha ya watu waliondokewa na wapendwa wao kutokana na risasi za askari wanajisikiaje. Lazima wana hasira sana.

Chama cha magamba kisipokemea serikali yake kuacha mauaji ya raia wake, kitambue kuwa kinajichimbia kaburi. Damu ya watanzania haiwezi kupotea bure. Chama cha magamba kitambue kuwa suluhisho la mtatizo ya watanzania haliwezi kupatikana kwa kupiga risasi na kuua raia. Suluhisho ni kutenda haki na kuwapatia maendeleo wananchi. Trend hii ya kuua raia ikiachwa iendelee, mwisho wake siyo mzuri.
 
kaka hii imekaa sawa , tatizo sidhani kama wathusika wanapitia njia hii na kuona ushauli wa buree kama huu, ambao ni msaada kwao, rais alianza kuzungukia wizara, akawaita dodoma . Juzi kakutana nao tena ikulu , hao hao , nchi imewashinda.
 
Very sad when the bullet that's kill you is from your Tax Money!. And Very sad too when some one is stelling your weath and anakuachia mahandaki na vidawati au vidarasa vya shule tuwili kama mgao wako katika mapato ya rasilimali zako mwenyewe.
Upuhuzi huu uwezi ufanya popote pale Duniani isipokuwa Tanzania tu.
Ee Mwenyezi Mungu tuokoe toka ktk Makucha ya udharimu huu.
 
Gosbert nakubaliana na wewe. Hakuna jambo baya kwa serikali kuua wananchi wake kwa kutumia askari wanaolipwa mishahara inayotokana na kodi ya wananchi haohao wanaouawa. Hiyo ni laana kubwa kuliko zote. Ndiyo maana wenzetu huko ulaya serikali zao hujiepusha na matumizi ya risasi za moto, kadri inavyowezekana hata kama waandamanaji watafanya fujo za aina gani. Hivi karibuni yalifanyika maandamano makubwa sana nchini uingereza ambapo kulikuwa na uharibifu mkubwa wa mali lakini hatukusikia mauaji yoyote ya raia.
 
walianza toka zaman kuuwa watu unakumbuka mkataba wa madini bulyahulu ulisainiwa na kikwete akiwa waziri na baadaye wachimbaji wazawa wakafukiwa kinyama na mabuldoza ya wawekezaji na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi ya wauwaji hao
sio hivyo tu umesahau kitendo cha mgodi wa nyamongo kumwaga maji machafu yenye cynide kwenye mto unaotumiwa na raia na mifugo but hakuna hatua yoyote iliyochukiliwa.
kaka inauma sana this govt is from the leaders by the leaders and for the leaders but one day we shall start a reform movement and change everything...Lord have mercy on us...
 
Hili la North Mara limeniumiza sana. Imagine mauaji yanaendelea mara kwa mara kama vile wanaouawa si binadamu bali ni wanyama pori. Watu wanaandamana kupinga mauaji ya mara kwa mara kisha authorities zinakuja na maelezo ya kipumbavu ndiyo ni ya kipumbavu kabisa kuwa waliandamana kuelekea mgodini kuiba dhahabu.. how. Hivi hawa viongozi sorry I mean watawala tulionao wanadhani watz ni wajinga kiivyo kweli? What I see ni kwamba hizi mamlaka husika zinachojitahidi hapa ni kutengeza bomu ambalo si mbali sana litawalipukia tu. Watch this space
 
Heee....mwashangaa hili...mbona watu kibao walishaga kufukiwa migodini na hukohuko na bado mkawapa ushindi wa kimbunga?..........hii ndiyo ccm baba lao bwana
 
R.I.P marehemu. Naungana na wana Jf wote wanaokemea kitendo hikilakini wakati tukiendelea kuiasa serikali yetu juu ya uonevu huu naomba kutoa angalizo: watz tujifunze kupenda maisha yetu hivyo tuishi kwa welevu, tutambue mipaka ya yetu na ya mali za wenzetu. Tumeshuhudia na tutashuhudia vijana wetu wa kifa vifo ambavyo vingeweza kuepukika. Tafadhari tuepuke kuingia kwenye un-authorized areas.
Hili la North Mara limeniumiza sana. Imagine mauaji yanaendelea mara kwa mara kama vile wanaouawa si binadamu bali ni wanyama pori. Watu wanaandamana kupinga mauaji ya mara kwa mara kisha authorities zinakuja na maelezo ya kipumbavu ndiyo ni ya kipumbavu kabisa kuwa waliandamana kuelekea mgodini kuiba dhahabu.. how. Hivi hawa viongozi sorry I mean watawala tulionao wanadhani watz ni wajinga kiivyo kweli? What I see ni kwamba hizi mamlaka husika zinachojitahidi hapa ni kutengeza bomu ambalo si mbali sana litawalipukia tu. Watch this space
 
me naomba kila mtu apewe bunduki bila mzunguko mkubwa
wa kupata kitu hiyo ili tujilinde wenyewe!
mbona marekani wanaishi vizuri tu bana
 
inasikitisha sana kuona unapambana na binadamu kama unapambana na nyani shambani, hii ni laana na ipo siku ccm hata muongee lugha gani hamtaeleweka.
 
Hakika damu ya Watanzania wazalendo iliyomwagika itakuwa juu ya wale wote wanaohusika(Viongozi walioingia mikataba mibovu/polisi waliofayatua risasi na kuua).Ewe Mwenye Enzi Mungu Baba waangalie na kuwafariji wale wote walioondokewa na wapendwa wao uwape nguvu,pia waangalie na wale wote waliomwaga damu ya ndugu zetu Watanzania......Amen
 
Vyombo vyetu vya usalama sasa tunaviogopa kuliko majambazi.
Hakika vyombo hivi vya usalama SI SALAMA.
 
R.I.P marehemu. Naungana na wana Jf wote wanaokemea kitendo hikilakini wakati tukiendelea kuiasa serikali yetu juu ya uonevu huu naomba kutoa angalizo: watz tujifunze kupenda maisha yetu hivyo tuishi kwa welevu, tutambue mipaka ya yetu na ya mali za wenzetu. Tumeshuhudia na tutashuhudia vijana wetu wa kifa vifo ambavyo vingeweza kuepukika. Tafadhari tuepuke kuingia kwenye un-authorized areas.

Acha kuongea Upupu wewe un authorized areas my Ass.
 
Back
Top Bottom