Mabasi yenye choo ndani

mgungani

Member
May 13, 2022
38
60
Ni wakati sasa wenye mabasi ya mikoani kuweka mabasi yenye vyoo ndani kurahisisha kutosimama njiani na kutoa huduma bora.

Mengi ya mabasi yaliyopo yenye vyoo hawaruhusu kwenda haja kubwa wakati vyoo vipo kwa kuhofia garama za kufanya usafi.

Kumbuka napolipia basi lenye choo nauli nayotoa inahusisha pia huduma ya choo bila kubagua haja ndogo au kubwa.

Kubagua aina ya huduma wakati nimelipia ni kama wizi au utapeli.baadhi ya watu wanaposafiri hupatwa na mchafuko wa tumbo hivyo kuwaweka kwenye hali ndumu.mbona kwenye ndege hawabagui aina ya huduma ya choo.

Naamini kabisa zikija kampuni zenye kutoa huduma zote za choo bila ubaguzi atawashinda wenzake kwa kupata wateja.

Ni wakati pia kwa vyombo husika kuhakikisha kama gari ina huduma ya choo abiria hapangiwa aina ya huduma kama kwenye ndege au treni
 
Kuna walimwengu wana matumbo mithili ya shimo la maji taka, haja kubwa yao ikitoka hali ya hewa inaweza chafuka kiasi cha kutowezekana kusafishwa na Air Freshner yeyote ile.

Sasa jiulize unatoka Dar kwenda Mwanza na njemba moja iliyokesha ikila kitimoto na bia ikaamua kwenda kuharisha mwanzo wa safari tu, halafu siti yako ni ya mwisho kabisa karibu na choo. Unahisi safari yako itakuwa ni ya aina gani?

Tofauti na ndege, tank la haja la basi lipo usawa wa buti tu, hivyo kuwa karibu sana na surface ya basi kwa ndani, hilo vundo lake mnaweza jikuta mnatapika basi zima.
 
ni wakati sasa wenye mabasi ya mikoani kuweka mabasi yenye vyoo ndani kurahisisha kutosimama njiani na kutoa huduma bora.mengi ya mabasi yaliyopo yenye vyoo hawaruhusu kwenda haja kubwa wakati vyoo vipo kwa kuhofia garama za kufanya usafi.kumbuka napolipia basi lenye choo nauli nayotoa inahusisha pia huduma ya choo bila kubagua haja ndogo au kubwa.kubagua aina ya huduma wakati nimelipia ni kama wizi au utapeli.baadhi ya watu wanaposafiri hupatwa na mchafuko wa tumbo hivyo kuwaweka kwenye hali ndumu.mbona kwenye ndege hawabagui aina ya huduma ya choo.naamini kabisa zikija kampuni zenye kutoa huduma zote za choo bila ubaguzi atawashinda wenzake kwa kupata wateja.ni wakati pia kwa vyombo husika kuhakikisha kama gari ina huduma ya choo abiria hapangiwa aina ya huduma kama kwenye ndege au treni
Hivi unaweza kufikiria mzigo wa watu karibuni 70 kwenye basi moja. Atakayekuwa amekaa karibu na mlango wa choo atatamani ashuke aachane safari.
 
Hivi unaweza kufikiria mzigo wa watu karibuni 70 kwenye basi moja. Atakayekuwa amekaa karibu na mlango wa choo atatamani ashuke aachane safari.
msiwe ridid.mbona ulaya mabasi yana vyoo kwa haja zote.mbona ndege na treni unaruhusiwa haja zote.suala la harufu ni usafi tu.mbona kwenye ndege hakuna harufu.lazima twende na dunia.Tanzania siyo kijiji.watu wanakaa nyumba selfu na hakuna harufu
 
Wewe ukipanda hizo basi zenye choo..ukijisikia haja nenda then kata gogo...halafu urudi utupe mrejesho.
 
Mi nikienda huko chooni nakata gogo tu watajua wenyewe huko na abiria aliye jirani na choo atapambana zake huko tena abiria mwenyewe wawe wale maboy wa dar wanaokula biscuits na Mo juice wanaenda kulala mpaka kesho au maduu wa dar wala viepe vya mafuta ya transformer natoa divi la maana mpk nikitoka nimuone kavuta mdomo.
 
ni wakati sasa wenye mabasi ya mikoani kuweka mabasi yenye vyoo ndani kurahisisha kutosimama njiani na kutoa huduma bora.mengi ya mabasi yaliyopo yenye vyoo hawaruhusu kwenda haja kubwa wakati vyoo vipo kwa kuhofia garama za kufanya usafi.kumbuka napolipia basi lenye choo nauli nayotoa inahusisha pia huduma ya choo bila kubagua haja ndogo au kubwa.kubagua aina ya huduma wakati nimelipia ni kama wizi au utapeli.baadhi ya watu wanaposafiri hupatwa na mchafuko wa tumbo hivyo kuwaweka kwenye hali ndumu.mbona kwenye ndege hawabagui aina ya huduma ya choo.naamini kabisa zikija kampuni zenye kutoa huduma zote za choo bila ubaguzi atawashinda wenzake kwa kupata wateja.ni wakati pia kwa vyombo husika kuhakikisha kama gari ina huduma ya choo abiria hapangiwa aina ya huduma kama kwenye ndege au treni
Umenikumbusha mwaka jana nilikuwa natokea Kigoma kwenda mikoa ya kaskazini.
Katikati ya safari tumbo likakumbwa na dhoruba mbaya kabiasa.
Nikamuomba konda anifanyie wwpesi...mzee baba gari ilisimama katikati ya pori nikapewa sekunde chache kushusha mzigo...niliingia porini hata kabla sijamaliza kuvua gari imeanza kupiga honi ...yaani nilitupa mzigo kwa haraka kabla mzigo haujaisha ikabidi nikatishe nirudi kwenye gari
 
Back
Top Bottom